Maktaba ya taifa Dodoma rekebisheni kasoro hizi

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Nilifika Maktaba ya Dodoma siku saba zilizopita, ni maktaba nzuri sana kwa kuangalia jengo.

Kuna kasoro ambazo lazima zirekebishwe haraka.

1. KELELE NJE YA MAKTABA
Viongozi wa maktaba lazima wazingatie ukweli kuwa maktaba ni eneo lenye kuhitaji utulivu sana kama ilivyo mahakamani na hospitalini.

Haiyumkiniki kuwa upande wa nyuma wa maktaba kumejaa machinga wenye vispika ambao wame set kelele za kutengenesha line za simu, offer za charge za simu na mauzo ya matunda....matangazo hayp yanaathiri sana usomaji kwenye maktaba hiyo ya Taifa.

Hili ni swala ambalo mtawwza kulitatua kwa kushirikiana na halmashauri ya JIJI la Dodoma. MaKTABA NA IHESHIMIWE.

2. KUFUNGWA KWA CHOO CHA WANAUME CHA GHOROFA YA KWANZA.
Nilipofika mwanzoni nilidhani ni choo kibovu ila kumbe kinafunguliwa wanapokuja watu wa mikutano tu. Ni aibu kumshusha mtu ground floor wakati angeweza kujisaidia huko huko juu.

3. Hakuna ingizo jipya la vitabu.
Shelves nyingi zimejaa vitabu chakavu na vya kale ambavyop havifai kufanyia rejea kwa machapisho ya wakatyi tuliopo.

Hongereni kwa usafi wa jengo na wahudumu wenye ushirikiano , ingawa mnachapakazi sura zenu zinaashiria

Kukosa motisha na posho kama walivyo wafanyakazi wa sekta zingine.

NAWATAKIA KAZI NJEMA
Dodoma Public Library.jpg
 
Ni kweli, ikiwapendeza huu utakuwa ufumbuzi wa kudumu, maana zile kelele za maroli, machinga, bodaboda na alarm za magari yaliyopaki ofisi za jiji Dodoma zinalifanya liwe eneo lisilofaa kusoma, kujisomea wala kufanya tafakuri za kitaaluma.
 
Ni kweli, ikiwapendeza huu utakuwa ufumbuzi wa kudumu, maana zile kelele za maroli, machinga, bodaboda na alarm za magari yaliyopaki ofisi za jiji Dodoma zinalifanya liwe eneo lisilofaa kusoma, kujisomea wala kufanya tafakuri za kitaaluma.
Hospital ya Makole.
 
Back
Top Bottom