Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 16,817
- 62,027
Rais Samia alipoingia madarakani kwa kiwango kikubwa alipokelewa vizuri sana na watanzania. Wengi walimuona kama hewa mpya, walimuona tumaini jipya baada ya maisha ya mbilingebilinge ya utawala wa awamu ya tano. Samia alitetewa, kukingiwa kifua dhidi ya critics mbalimbali, akapewa jina la mama ili kuinua soft power yake na kumpa moral authority ya "umama". Na yeye kwa wakati huu akiwa bado hajakizoea kiti, au kuamini kuwa yeye sasa ni rais, aliendelea kuongea lugha za kiungwana, kujaribu kuunganisha watu, kuonyesha anataka maridhiano ya kitaifa. Akafuta kesi nyingi tu za watu, na kujitahidi kuwapa kifuta machozi walionyang'anywa fedha zao kipindi cha utawala wa rais Magufuli. Hapa ndipo watu waliposema "mama anaupiga mwingi". Sasa sijui mdudu gani akaja akatibua muenendo mzuri wa Samia na kuanza kuufanya umma unze kumgeuka. Nitaeleza baadhi ya mambo yaliyofanya watu waanze kumgeuka.
1. Operesheni ondoa wamachinga Dar es salaam
Kama mnavyofahamu mtangulizi wake yaani JPM yeye aliamua kuwekeza nguvu zake za uongozi kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu wa chini. Kwa hiyo kuna makundi ya wananchi aliamua kuyaacha tu yafanye shughuli zao. Bila kujali uzuri au ubaya, uhalali au uharamu wa hatua hizo lakini aliamua tu kuwaacha waendeshe biashara zao mabarabarani. Na pia kama mnavyojua,Ishu ya wamachinga ni kaa la moto toka enzi za mzee Mkapa, na Kikwete. Hawa walikuwa wakifanya operesheni ndogondogo za hapa na pale kudeal na wamachinga wakizidi eneo fulani na haswa kariakoo. Sasa alipokuja Samia, labda akadhani yeye anaweza kumaliza tatizo kwa kudeal na wamachinga physically tena kwa harakaharaka badala ya kudeal na matatizo yanayosababisha umachinga uwepo. Operesheni ile ya almost Jiji zima la Dar iliumiza wamachinga sana, ikaibua hasira kwa wamachinga, na hapa ndo vile vilio vya watu kwenye video wakimkumbuka Magufuli vilipoanza kwa kasi. Mama akawa amejijengea foundation ya kuchukiwa na watu wa chini na naamini hajarecover vya kutosha tangu operesheni ile. Hili la kuwapanga wamachinga linatakiwa lofanywe lakini si kwa operesheni za maguvu wakati huna alternative ya kuwapa watu wanaotegemea msosi wao wa kila siku kwa kubangaiza.
2. Tozo
Akiwa sasa amekaa kwenye kiti, akiwa ameanza kukizoea, Samia akaja na ishu ya Tozo, wananchi wakapiga kelele sana, kelele zilikuwa nyingi sana, mwanzoni aliingilia kati kuutuliza umma, lakini baadae waziri mwenye dhamana akakomaa na tozo, wananchi wakalalamika sana, Samia akaweka pamba masikioni. Waziri wake wa fedha akasema asiyetaka tozo ahamie burundi. Samia na serikali yake hawakuishia hapo, wakaleta kodi ya jengo kwenye LUKU, yaani mpangaji wa nyumba kila akinunua umeme, eti akatwe yeye hela kumlipia mtu mwenye jengo lake. Wananchi wakalalamika Samia akapiga kimya, ila Chuki ya umma ikawa inaendelea kufukuta dhidi yake.
3. Kero za wananchi, Kukatika kwa maji hovyo na umeme hovyo
Kuanzia mwaka 2021 miezi ya mwishoni kumekuwepo na shida ya maji isiyoisha, migao isiyoeleweka, kila mwaka stori za serikali zikawa ni hizohizo mara ooh tunajenga bwawa la Kidunda, mara ooh subirini Bwawa la Nyerere likamilike. Leo bwawa la Nyerere limekamilika, umeme bado siyo wa uhakika na migao ya maji ipo kama kawaida, na wananchi mamilioni huko mikoani hawana maji safi na salama ya kutumia. Kipindi cha Magufuli siyo kwamba migao ya maji na umeme haikuwepo, ilikuwepo lakini kipindi cha Samia ilizidi hata maradufu. Wananchi wakaanza kusema kuwa mbona kipindi cha Magufuli mambo hayakuwa hivi?
4. Kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe
Sasa miongoni mwa vitu vilivyofanya huyu mama achukiwe na umma ni hii kesi ya Mbowe. Umma ulitafsiri kesi ile kuwa ni ya mchongo, kwamba ni kesi ya Uongo. Watu wakaanza kusema kuwa kumbe huyu mama siyo mtenda haki na muungwana kama tulivyodhani hapo mwanzo. Hii kesi ilimuharibia Taswira huyu mama mbele ya umma kwa kiwango cha kutisha, hajawahi kurecover vizuri baada ya hapo. Kwa kweli namshangaa Mbowe ambaye baada ya kutoka Jela huku akiwa na mtaji mkubwa sana wa kisiasa alienda kuuza mtaji huo kiurahisi rahisi tu kwa Samia, wakati angejua thamani ya mtaji aliokuwa nao leo ndo angekuwa mwanasiasa maarufu na mwenye ushawishi kuliko mwanasiasa yeyote nchini. Pole zake.
5. Suala la mkataba wa Bandari
Ule mkataba ulipingwa na umma, na haukuridhiwa na umma hata kidogo. Ule mkataba siyo mzuri hata kidogo. Wananchi waliugomea katakata. Lakini Samia ili kulinda political career yake akaamua maadamu ameshaharibu basi mbwai iwe mbwai hageuki jiwe. Matokeo yake imekodishwa kwa waarabu na umma haukusikilizwa. Sasa chuki na hasira ya umma ndo anakutana nayo mitaani na mitandaoni. Kwa maoni yangu huwezi kuwa rais wa watu, halafu watu wanakwambia hawataki mkataba huo uendelee wewe ukashupaza shingo, hawatokufarahia hata kidogo.
6. Kuanza kuminya Freedoms za watu
Sasa Samia baada ya kuona umma umeanza kuja juu, kumkosoa vikali akaja na ile strategy iliyofeli ya Madikteta ya kujaribu kufungia mitandao ili watu wasipate taarifa au wasiikosoe serikali. Kwa hiyo mtandao kama clubhouse ukafungiwa, na baadae mtandao wa twitter nao ukafungiwa, na siku hizi Polepole akiongea eti wanazima youtube na facebook. Sasa vitu vyote hivi accumulatively vinajenga chuki kubwa ya wananchi kwa serikali yake na yeye kiujumla. Kama angekubali kukosolewa na akatengeneza timu nzuri ya kujibu hoja kwa hoja kungeuwa hakuna haja ya kurudisha watu nyuma huko ambako tumeshatoka.Watu hawataki turejee tena huko.
7. Safari za nje ya nchi
Wakati huo umma unamkumbuka Magufuli ambaye alishawaaminisha kuwa safari hizi hazina tija kivile. Wakati mwingine umma unawaona wasanii kwenye madege wanalipiwa safari na serikali wakiwa wameandamana na delegetion za serikali. ukirudi huko unaanza kununua Magoli ya Simba na Yanga wakati wanaoenda kuangalia mpira mtaani kwao kuna shida ya maji ya kunywa. Hao mashabiki wanafurahia kushinda mechi zao lakini usidhani eti watakupenda kwa sababu umenunua goli. Yaani they don't associate ushindi wao na pesa ulizowapa hadi wafikie hatua wasamehe ukosefu wa huduma bora hospitali wakushangilie wewe. Sasa haya mambo yalijenga taswira mbaya kwa rais na kufanya umma usimuangalie vizuri.
8. Mambo ya utekaji na kupotea kwa watu
Hii ishu ya wananchi kutekwa na kupotezwa, huku serikali ikijivua responsibility, lakini umma siyo mjinga, wanaona wanaotkwa na kupotezwa ni wale wenye muelekeo wa kuikosoa serikali, basi wananchi wanasema fumbo mfumbie mjinga mwerevu hulin'gamua. Sasa imagine eti akatekwa katoto kadogo kama Deusdedith Soka, anatekwa mtu kama Mdude Nyagali, Akina Mbise, bila kusahau listi ya watu kibao waliotekwa toka mwaka 2021, serikali ipo haichukui hatua madhubuti, hii inawafanya watu waconclude kuwa hii kitu serikali yake inajua A to Z ya mchongo mzima wa haya mambo na ni "INSIDE JOB". Haya mambo yakasababisha umma umchukie Samia mno tena mno. Yeyote aliyempa strategy ya kutawala kwa hofu, akiamini kuwa kwa kufanya hivyo labda watu watamuogopa kama walivyomuogopa Magufuli alimuharibia uungwaji mkono wa kisiasa mbele ya umma kwa kiwango kisicho na mfano. Tena kilichochagiza hali hii ni tukio la kuumizwa kwa Father Kitima na namna alivyodeal na Ishu ya Askofu Gwajima. Damage kwa namna walivyodeal na hizi issues ilikuwa damaging sana.
9. Kesi ya Lissu na Kutumia Mahakama kisiasa
Siku hizi Samia na Serikali yake wakishindwa kujibu hoja za wananchi, au wakipata kibano kikali cha kisiasa, badala ya kujibu hoja, au kufanya siasa basi mahakama inatumika kuwatoa kwenye kitanzi. Mahakama sasa imegeuka kama jumuia ndani ya Jumuia za CCM. Haitendi haki hata kidogo. Na ushahidi wa kwamba haitendi haki ni kuwa hatuoni haki ikitendeka katika maamuzi yake. Akina Mwabukusi, Dr Slaa na Mdude walivyokuwa wakitetea bandari wakapigwa kesi ya uhaini. Leo tunaona Lissu naye kapigwa kesi ya Uhaini. Lakini kila mwenye macho anaona wazi kuwa hamna kitu hapa ni mchongo mchongo tu. Kwamba tumekushindwa jukwaani ngoja tudeal na wewe kwenye kizimba!. Kwamba tumeishindwa CDM huko mitaani sasa tuwazuie kupitia kesi za mchongo. Haya mambo yanajenga chuki kali kwa umma, yanamfanya Samia aonekane ni dhaifu mno kiuongozi na yanamharibia taswira yake ndani na nje.
Mwanzoni nilizungumzia jinsi kesi ya Mbowe ilivyomharibia Samia heshima. Hii ya Lissu sasa ndo funga kazi, watu wanaona kesi yake inavyoendeshwa, wanaona waziwazi abuse ya power, chuki haiendi kwa mahakimu, chuki inarudi kwa yule aliyeifungua. yaani hii kesi imemharibia heshima Samia FIVE TIMES kuliko hata ile ya Mbowe.
10. Uteuzi wake wa kugombea urais ulivyofanyika na mbeleko ya kisiasa
Samia amepanda ngazi nyingi za uongozi kwa kushikwa mkono na wala si kwa kupambana nginjanginja, alishikwa mkono na maraisi waliopita, wakampa nafasi hizi na zile, mwaka 2015 akapewa nafasi ya umakamu wa Magufuli kingekewa tu kwa sababu wazee walisema awekwe yeye, hakuwa mwanasiasa prominent nchini, Mwaka 2021 akaukwaa urais baada ya kifo cha JPM, Sasa safari hii watu walitegemea apate urais kwa kusimama ndani ya taratibu, kanuni na katiba ya chama lakini mentality ileile ya "Kamlete", "mbeleko" ikatumika. Sasa hii inaibua chuki ndani ya CCM na hata nje ya CCM wanapoona mbona mtu anataka uarais sana hadi kufikia hatua za kanuni na taratibu za chama zinavunjwa?, hii nguvu yote ya kukwepa ushindani ya nini?
Kiufupi hayo ni baadhi ya mambo ninayoyaona yamepelekea Samia kuchukiwa na kukosa ushawishi wa umma kwa kiwango kikubwa sana.