Makosa ya barabarani tunayoonewa hivi sasa

Makosa ya barabarani tunayoonewa hivi sasa

Sheria inataka kusimama kwenye Zebra kisha uangalie kuakikisha kuwa hamna anayevuka ndio uendelee na safari yako. Hii sharia ukienda nchi nyingi za SADC wanaitumia sana. Tusilalamike bali tutii sharia bila shuruti kumbuka kutojua sheria hakukupi msamaha wa kosa
Mkuu nchi za wenzetu hakuna alama wanaheshimu kama alama ya zebra. Ukifika kwenye Zebra ni lazima usimame hata kama hakuna mtu. Sasa hapa kwetu duuuu kila moja anaharaka.

Mim nafikiri hii alama tuiheshimu au tuione kama mahakama.
 
Kama kawaida yao trafiki hivi sasa wanaendelea kutunyanyasa na kudai faini kwa makosa mbambali mengi y kiwa kubambika kabisa.

Mfano mimi jana nipo barabarani na eneo hilo hakuna watu kabisa nikaikuta ZEBRA na kipindi hicho hakukuwa na mtu yeyote ambae anahitaji kupita ama ambaye yupo jirani nikapita kufika mbele kidogo nikamkuta Trafiki akanisimamisha, akaomba leseni nikampa akakagua gari akaniambia kosa lako ni kwanini hukusimamama kwenye ZEBRA.

Nikamjibu hakukuwa na mtu yeyote ambaye anataka kupita na hakukuwa na watu jirani hapo. Akaniambia ni kosa kupita kwenye ZEBRA bila kusimama.

Jamani wataalamu na naombeni kuelimishwa ili tusionewe.

Pole sana mkuu, mie nilimsikia Afande Musilimu akisema unapunguza mwendo sio kusinama. Pia nilipiga namba ya traffic HQ iliyo katika sticker ya usalama barabarani wakasema wameshaeleza sana kuwa kama hakuna mtu ni kupunguza mwendo na unaendelea na safari. Wakikukamata piga simu hizo waongee wao kwa wao.
 
Mimi nilisimama vizuri katika zebra.Mbele nakamatwa eti kuna mtu alikuwa amekaribia kukata barabara sikumpisha
 
Na mkitoa hiyo 30 mnachukua lisiti? Kama huchukui haiingii kwenye mapato ya serikali1
 
Mikoani huko wanaonewa sana ... Dar usimame kwenye zebra bila sababu utapigiwa honi kama umeua....
umenichekesha, kwa kweli zebra dar hatuzijali kabisa tena ukijitia unajua sana kuzifatilia unaweza ishia kujikuta unagongwa kwa nyuma wakati mwingine wewe unasimama kupisha watu wapite wa nyuma yako ana overtake anapita nusura kugonga watu
 
Mpaka tumestaafu kuazima magari ya watu huchelewi kulazwa central mafaini kibao na wakati gari lenyewe si lako
 
Kama kawaida yao trafiki hivi sasa wanaendelea kutunyanyasa na kudai faini kwa makosa mbambali mengi y kiwa kubambika kabisa.

Mfano mimi jana nipo barabarani na eneo hilo hakuna watu kabisa nikaikuta ZEBRA na kipindi hicho hakukuwa na mtu yeyote ambae anahitaji kupita ama ambaye yupo jirani nikapita kufika mbele kidogo nikamkuta Trafiki akanisimamisha, akaomba leseni nikampa akakagua gari akaniambia kosa lako ni kwanini hukusimamama kwenye ZEBRA.

Nikamjibu hakukuwa na mtu yeyote ambaye anataka kupita na hakukuwa na watu jirani hapo. Akaniambia ni kosa kupita kwenye ZEBRA bila kusimama.

Jamani wataalamu na naombeni kuelimishwa ili tusionewe.
Kwa kweli jambo hili linaboa haswa. Yaani nchi hii sijui kwa nini inapenda kuwa na sheria zake ambazo hata wageni wanatushangaa. Mimi nilisafiri na mzungu mmoja ambaye ana international driving license na ameendesha gari worldwide ila alishangaa sana traffic polisi wetu wanavyofanya kazi.

1. Over speeding: Kitendo cha mtu kujificaha porini na kujifanya anamulika magari yanayotembea over the limited speed na kwenda kusimamishwa 30 km ahead is totally unacceptable. Kwa sababu, accuracy ya information unazopewa ni doubtful. Huwezi kumwambia mtu madhalani alikuwa anatembea speed ya 95 km/h ndani ya eneo ambalo spped ni limited to 50km/h bila kumwonesha kuwa kweli alikuwa ndani ya eneo hilo. Sasa hivi anakuonesha picha ya gari lako tu bila vibao vya speed limit kuthibitisha kosa lilifanyika ndani ya eneo lenye speed limit

2. Pedestrian crossing lines:- hapa ndiyo hata huelewi nini kinaendelea manake kila mtu anatafsiri yake,- matokeo yake kumeongeza msongamano usio na sababu.
 
Dodoma ndo balaa trafiki akiona chombo cha moto anakua na hasira balaa mpaka kero!
 
Mimi nilisimama vizuri katika zebra.Mbele nakamatwa eti kuna mtu alikuwa amekaribia kukata barabara sikumpisha

Nami pia hivyox2 hawa jamaa wa OVYO sana, wanatafuta sifa. Kuna tetesi kuwa wanawekewa kiwango kwa siku, yaani ni shida.
 
Hiyo hela yakiwi inatia hadi kichefuchefu ni aina flani yarushwa.Nikuwekewa kosatu
 
Mbeya wanatutesa Sana kwa hii sheria, utakuta foleni ndefu kwa sababu ya zebra na mara nyingi hakuna mtu wa kuvuka.
Upo sahihi mkuu!
Niliwahi kusafiri toka Dar kwenda Tunduma, nilipofika Igawa nikakumbana na hii kadhia. Mpaka nikahisi nipo nchi nyingine yaani mpaka kufika Tunduma akili ilikuwa imenikaa sawa! Kuvuka kwenye zebra bila kusimama Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Songwe ni kosa kubwa sana!!
 
Hawa trafic nasikia kwa cku huwa wanapangiwa makosa 5au 3 kulingana na mkoa ,mi nishukuru hata mambosasa kutoa tamko,nimefika kenya trafiki hawana ujinga huu,trafiki wa tz njaa kali,halafu kwanini wanakaa muda mrefu kuwa trafiki wangukuwa wanabadilishiwa vitengo mara mfano ffu,au cro,siyo kinakuwa kitengo cha kudumu,ndo maana wana dharau,mtu anahonga ili apate kitengo cha utrafiki lengo lake akapate nini?
 
Mbeya wanatutesa Sana kwa hii sheria, utakuta foleni ndefu kwa sababu ya zebra na mara nyingi hakuna mtu wa kuvuka.
b5e253e7d613e2bb59b9d181c9c51939.jpg
 
Sheria inataka kusimama kwenye Zebra kisha uangalie kuakikisha kuwa hamna anayevuka ndio uendelee na safari yako. Hii sharia ukienda nchi nyingi za SADC wanaitumia sana. Tusilalamike bali tutii sharia bila shuruti kumbuka kutojua sheria hakukupi msamaha wa kosa
Kifunga cha Sheria namba 65 kifungu kidogo10 cha makosa ya barabarani
e910c587ba779a1f6b58d8d6f3d43c87.jpg
kinasema ukikaribia zebra Punguza mwendo hukuukiangalia pande zote mbili kama kuna yeyote anayetaka kuvuka kama yupo simama avuke na kama umeona hakunadalili ya mtu kutaka kuvuka unaweza endelea na safari si lazima kusimama askari wetu wanatumia mwanya huo kutubana kwa wale tusioijua hii Sheria vizuri
 
Back
Top Bottom