Makosa katika uandishi wa maneno

Mimi pia naomba msaada kwenye vigeregere na vigelegele. Nadhani sahihi ni vigeregere lakini sina uhakika wa 100%. Pia kuna swala na suala, wenzetu wa zenj hutumia sana suala na sisi 'wazanzibara' hutumia swala. Je ni sawa kusema suali badala ya swali?
 
Bubu hapo ndipo mtaalam wa Kiswahili anapotakikana. Nadhani vigelegele ndio neno sahihi, ingawa na mimi sina uhakika 100%. Swala ni neno tata hivyo inategemea na matumizi. Nadhani neno sahihi katika kumaanisha mambo yaweza kuwa suala. Mfano suala la lugha linakuwa gumu. Nadhani tofauti kubwa ni matamshi. Kuhusu Suali na swali, naona kama swali liko sawa kuliko suali.

Pamoja na hayo, matatizo kwenye lugha ya Kiswahili ni makubwa kuliko inavyodhaniwa! NINI WAJIBU WA BAKITA na TUKI? (sijui kama kuna vyombo vingine vinavyohusika na maendeleo ya lugha ya Kiswahili). JE WANATEKELEZA WAJIBU WAO?
 
Nadhani neno sahihi katika kumaanisha majambo kuwa...

"Majambo" sio neno. Wingi wa jambo ni mambo.

Mfano suala la lugha linakuwa gumu.

"Suala" sio neno.

By the way, Mama, huwezi kusema "X ndilo jibu ingawa sina uhakika 100%." Sema "nadhani X ndilo jibu, sina uhakika."
 
"Majambo" sio neno. Wingi wa jambo ni mambo.

"Suala" sio neno.

By the way, Mama, huwezi kusema "X ndilo jibu ingawa sina uhakika 100%." Sema "nadhani X ndilo jibu, sina uhakika."

Kuhani, kila lugha ina matatizo yake, na kwa kawaida makosa katika matumizi yanakuwepo. Matatizo katika hii lugha ni makubwa kuliko inavyodhaniwa. Au ndio kukomaa kwa lugha kunavyokuja hivi?
 
"Majambo" sio neno. Wingi wa jambo ni mambo.

"Suala" sio neno.

By the way, Mama, huwezi kusema "X ndilo jibu ingawa sina uhakika 100%." Sema "nadhani X ndilo jibu, sina uhakika."

Kuhani sasa ina maana wazenj wanafanya makosa katika kiswahili kwa kutumia neno hilo? Maana Wazenj wengi wanadai neno sahihi ni 'suala' na siyo 'swala'. Hapo bado hatujagusa maneno yanayotumiwa na wenzetu marikiti, buku, skuli n.k.
 
Bubu yote tisa, kumi ni maana ya mrefeji na bomba.

Lakini hii ya watu kuchangaya herufi r na l au h na a ndio inayonitia mashaka zaidi.
 
Bubu yote tisa, kumi ni maana ya mrefeji na bomba.

Lakini hii ya watu kuchangaya herufi r na l au h na a ndio inayonitia mashaka zaidi.

Mama mimi kusema kweli sina matatizo hayo ya kuchanganya r na l au h na a kama ikitokea ni kughafilika tu, lakini hili la vigelegele huwa linanichanganya. Neno sahihi ni vigelegele ilibidi niingie kwenye kamusi kupata uhakika wa neno sahihi.
 
Sawa kabisa, na ukishapata hilo neno sahihi tafadhali tujulishe. Natanguliza shukrani.
 
Mama, neno sahihi ni vigelegele na siyo vigeregere.

Mkuu Bubu Ataka Kusema ni kweli kwamba neno sahihi ni Vigelegele na sio Vigeregere kama linavyotamkwa na wengi...Na pia neno suala ni sahihi kama alivyolitumia Mama,kwa namna moja au nyingine linafanana sana maana na neno "jambo" (ukiacha neno jambo linalotumiwa kama salamu).

Neno Swala lina maana ya "Ibada" kwa waumini wa dini ya kiislamu na wale wakristo hutamka "sala",asili ya neno hili ni kiarabu likitamkwa "swalat".hakuna neno suali kwenye kiswahili bali kuna swali.

Maneno/majina Buku,Skuli na marikiti ni maneno ya kawaida mno huko zanzibar/Pemba,lakini hicho sio kiswahili fasaha,ni maneno ya kiingereza yaliyogeuzwa kuwa kiswahili.kama lilivyo jina Glasi ambalo kiswahili chake ni Bilauli(ri).

Waungwana naomba tafsiri ya maneno/majina "Mjasiriamali","Mjasirimali","kikokoteo","kukeketwa","Veranda" na "Ushoroba".
 
Hivi kama mtu anaathiriwa na lugha yake ya asili kwenye ubongo au utamkaji mdomoni pekee....inanishangaza kidogo mtu anatamka masiwa badala ya maziwa lakini pia akiandika huandika masiwa!

Eti 'juice' yaitwaje kwa kiswahili fasaha?
Kitu kama sharubati hivi?

Roya, sina uhakika, ila yawezekana neno hilo likawa 'shurubati'
 
kwa mfano mimi kama mimi mwenyewe binafsi uwaga nafikili akuna hanayejua kua hanakosea adi aambiwe kua hanakosea au hajifunze kujuwa makosa.

Sio uwaga ni huwa
sio nafikili ni nafikiri
sio akuna ni hakuna
sio hanayejua ni anayejua
sio kua ni kuwa
sio hanakosea ni anakosea
sio adi ni hadi
sio hajifunze ni ajifunze
 
haya maneno mara nyingi hukosewa sana kila siku,sasa sijui tuseme ni common mistakes au ni uzembe. Mimi nadhani kuna kauzembe fulani hivi kanako sababisha waandishi wengi kutohoa maneno wasiyo yajua.

Nini maana ya kutohoa? na inamaanisha nini katika ujumbe huu?
 
Sio uwaga ni huwa
sio nafikili ni nafikiri
sio akuna ni hakuna
sio hanayejua ni anayejua
sio kua ni kuwa
sio hanakosea ni anakosea
sio adi ni hadi
sio hajifunze ni ajifunze
Mama ametoa mifano ya baadhi ya maneno ambayo hukosewa mara kwa mara. Hapa ameua ndege wawili kwa jiwe moja. Yaani ametumia maneno hayo hayo yanayokosewa kwa kufikisha ujumbe wake. Au siyo Mama? Au mimi ndio sikuelewa?
 
kutohoa ni kuliazima neno kutoka katika lugha ningine na kulibadilisha kudogo kulingana na hitajio la lugha husika na kuwa ni neno rasmi.

mfano:- MOTOKARI (ah siku hizi wengi hawalitumii) limetokana na kiingereza Motor Car.
FENI kutoka kiingereza FAN na mengine mengi tu.
huko ndiko kutohoa.
Ila alivyolitumia mwenzetu hapo hakika sioni kama amelitumia neno hilo inavyostahili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom