Makosa 10 aliyotenda Mungu

CHAMITON,

Maswali mazuri sana.

Tujadili swali kwa swali.

La kwanza:
Job 47:16, Psalm 239:2-4, 147:5, Proverbs 5:21, Isaiah 46:9-10, 1 John 3:19-20, etc zina support kuwa Mungu anajua KILA KITU; kilichokuwa, kilichopo and kitakachokuwa. So ni kweli kabisa, ALIJUA kuwa njemba itaasi and kuleta sheeda kwetu duniani. I agree.

Kwa nini alimuumba despite kujua hili?

Jibu lake:
Ili mpango wake juu ya binadamu utimie.

Ila unazaa swali lingine hapo: Mpango wake juu ya binadamu ni nini? Bila kujua hili sidhani kama utaweza elewa why He did what he did, create the devil.

So probably ili kupata jibu kamilifu la swali la kwanza inabidi kujiuliza mpango WA Mungu ni nini? Angalizo: Sidhani Kama tunaweza jibu kikamilifu hapa maana akili zetu na zake ni kama ... (Isaiah 55:8-9)
Kama shetani anatumika kukamilisha mipango ya Mungu, je tutakuwa sahihi kusema shetani ni mtumishi wa Mungu???
 
Na kingine labda kama adam ha hawa hawakupaswa kugegedana kwanini walikuwa na viungo tofauti vinavyoingiliana na kusababisha raha????
 
Na kingine labda kama adam ha hawa hawakupaswa kugegedana kwanini walikuwa na viungo tofauti vinavyoingiliana na kusababisha raha????
Hawatakujibu, wanakwepa tu.
 
Kwanini haikwandikwa kwa urahisi tukaielewa???

Tatizo sio lugha rahisi bali ni.......

Ufunuo 3:

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Matthew 43:

13 Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.

15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
 
Tatizo sio lugha rahisi bali ni.......

Ufunuo 3:

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Matthew 43:

13 Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.

15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Ndiyo imeandikwa kwa mafumbo, kwanini isingeandikwa kwa lugha nyepesi...ili ieleweke???...mbona silabasi zinaandikwa kwa lugha nepesi na watu wanapata degree???
 
Hivi huwa ukivimbiwa unafanya nini si kutoa vijambo ili mambo yawe sawa ? Hayo matetemeko yanatokea huenda ndio dunia nayo inacheua mambo yakae sawa
 
Kama shetani anatumika kukamilisha mipango ya Mungu, je tutakuwa sahihi kusema shetani ni mtumishi wa Mungu???

Interesting thought.

Nope. Hafanyi yanayompendeza Mungu or aliyotumwa na Mungu therefore sio mtumishi wake.

Ila, katika hali yake ya "ushetani " Mungu anamtumia ili kukamilisha mpango wake juu yetu, mpango uliokuwepo toka mwanzo, kabla ya shetani
 
About male nipples???
Apart from other relevant biological functions what i know about male nipples is Without Nipples the Male Chest Looks Strange. The nipples provide a focus point for the male chest. They direct the eye to the curve of the pectoral muscle.

God needed to make difference between the two of us so we ulitaka wote tunyonyeshe napo ungetaka sababu?
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa.Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ogomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake??? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony???..Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure...God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he didi..sasa waovu wa leo wametoka wapi??? mbona aliuwa watu wengi bila huruma??? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini??? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao??? mbona Gadaffi aliweza???.Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi???...WE HAVE TO BE FAIR!!!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi??? je kuna muda wa kutosha??? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati???

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu??? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema??? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao??? au hakujua???

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwani kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko....Kwani anawauwa watu kikatili hivi???au haya nayo tumsingizie shetani???

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo??? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani???.Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina???

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu??? Kwani hajui kusamehe???Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani?. Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao??? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATING THEM...So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)??? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani??? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia??? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani???

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!!!
Hujui wewe ndiye unayesababisha yote hayo Hivi unafikiria kipi kiliwafanya waisraeli wasifike kanaani Hivi unafikiria kipi kilimfanya mungu kuja duniani hivi unafikiria kipi kilimfanya shetani aje duniani na upi mpango wa mungu Kwa shetani
 
USIMDHIHAKI MUNGU HATA KIDOGO, huwezi kufanya conclusion ya kuwa hakuna Mungu kwa kufanya reference ya kitabu kimoja cha DINI, wakati duniani Kuna DINI nyingi sana, UISLAM, BAHAYI, HINDI, nk na bado huwezi kusema Mungu hayupo wakati kunasayari nyingi sana ULIMWENGUNI,vipi kuhusu viumbe wanaoishi sayari nyingine wanamuabudu Nani ? Inamaana wewe unaakili nyingi sana kuliko watu wote wanaomuabudu MUNGU ALIYE HAI, TANZANIA, AFRICA, DUNIANI na SAYARI ZINGINE. Embu achana na hii habari ya MUNGU BABA, ongea kitu kingine.
Ni wapi nimesema hakuna Mungu???...Ni sayari ipi nyingine yenye watu???
 
Wakati Mungu anamuumba hakujua kama atakuja kuasi...si anajua mambo ya mbeleni???
Mungu alijua kuwa shetani ataasi na alimuumba kwa sababu ya upendo wake. Na siku alipoasi na yeye alipewa mda mrefu wa kujutia maovu yake lakini shetani hakufanya hivyo na ikabidi atimuliwe lakini pamoja na hayo Mungu hakumnyanganya uwezo na nguvu ya kimalaika. Madai ya shetani ni kuwa Mungu ni katili hana huruma wala upendo. Mungu aliacha kumteketeza ili kupisha upendo na huruma zake mbele ya raia wa mbinguni na wa ulimwengu ili wathibishe hayo madai. Ndo maana shetani na wafuasi wake wanatanua mpk Leo
 
Hapo nimetania tu. Kikubwa ni kwamba hakuna Mungu na hakujawahi kuwa na Mungu na hakutakuja kuwe na Mungu.

Ishi tu vizuri na watu wenzako huku ukijua huyo anaeitwa Mungu aliumbwa na wanadamu kwenye mind zao.

HAKUWEZEKANI KUWE NA MUNGU MSHENZI NAMNA HIYO
Ndugu yangu hata kama unaamini Mungu hayupo sio vizuri kumwita kwa majina uliyasema hapo chini ,acheni matusi kwenye imani za watu wengine
 
Mungu alijua kuwa shetani ataasi na alimuumba kwa sababu ya upendo wake. Na siku alipoasi na yeye alipewa mda mrefu wa kujutia maovu yake lakini shetani hakufanya hivyo na ikabidi atimuliwe lakini pamoja na hayo Mungu hakumnyanganya uwezo na nguvu ya kimalaika. Madai ya shetani ni kuwa Mungu ni katili hana huruma wala upendo. Mungu aliacha kumteketeza ili kupisha upendo na huruma zake mbele ya raia wa mbinguni na wa ulimwengu ili wathibishe hayo madai. Ndo maana shetani na wafuasi wake wanatanua mpk Leo
Umejibu kinadharia mno...ila akitubu leo ataenda mbinguni???
 
Ujuaji huu wote ni kwa sababu mwenyezi Mungu kakupa uhai leo!!? Unafikiri wewe upo kwa sababu ya malengo yako? Visa vyote ulivyotaja vinaashiria ni jinsi gani Mungu alivyo mwenye upendo mwingi sana,
Mungu hachunguziki kama umebaini na kuamini juu ya hayo unayoita MAKOSA KUMI... je, kama hayupo hayo makosa uliyoyataja yatakuwa ya nani sasa badala yake? Je, unaamini kuwa wewe unauelewa mkubwa kuliko sababu(Mungu) iliyokufanya uwepo?

Ruhusu mawazo yako yamtambue na kumkiri mwenyezi Mungu, kwa maana wewe u mwanadam na siku zako zahesabika hapa duniani.
Hivi shetan kaumbwa nanan! Nakama aliumba malaika wote wema huyu alieasi huu uasi alijifunza wapi labda tukubali mungu pia ameumba dhambi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom