Hebu tutumie akili kidogo kupima huo mtazamo wako.hakuna uongo hapo! hakuna ulicho kitunga vyote vimeandikwa kwenye vitabu vya dini.
watu wanahofu kutokana na jinsi dini zao zinavyowaaminisha.Lakini kiuharisia haya mambo ya dini probability kama ni ya kweli ni ndogo sana.
bado siwalaumu waanzisha dini waliona mbali sana walijua hiyo ndio njia ya kuleta amani na ustaarabu ktk jamii .
Mimi na wewe tunajukumu la kusupport dini kuendelea ili jamii isiwe na maovu.Binafsi najiita na dini fulani hata wanangu nitawaambia hivyo ingawaje akilini mwangu najua mimi ni mpagani nafanya yote hyo ili kutaka kujenga maadili mema kwa familia na jamii,ila mambo ya moto,pepo,shetani nk ni hamasa na vitisho ili watu wakae kwenye mstari, binadamu wengine hawana kabisa selfdispline hawawezi kujiongoza wenyewe.
Usipokuwepo wapi sasa? maana kiuhalisia kabla ya wewe kuwepo kuna watu walikuwepo na ndiyo chanzo cha wewe kuwepo,sasa utasemaje usipokuwepo na hakuna kilichopo?Jaribu kuelezea uwepo wa Mungu pasipo wewe kuwepo. Ukishindwa, ujue wewe ndiye mwanzo na mwisho, Alpha na Omega.
Uwepo wako ndio uwepo wa kila kitu. Hakuna JF bila Mimi kuwepo. Hakuna Mungu bila Mimi kuwepo. Hakukaa kuwepo na hatakaa awepo nje ya uwepo wangu.
Sikuwepo, na hivyo hakukuwa na uwepo katika kutokuwepo kwangu. Nipo ndio maana kuna uwepo. Kabla ya kuwepo, sikuwaza kuhusu uwepo. Sikuwa huru kuchagua namna ya kuwepo au kuwasiliana na uwepo au kuamua kutokuwepo.
Mama mjamzito yupo kwa kuwa kuna kiumbe hai tumboni. Wazazi wapo kwa kuwa kuna watoto n.k n.k Mungu yupo au hayupo kwa kuwa tupo. Usipokuwepo, hakuna kilichopo.
Hebu tutumie akili kidogo kupima huo mtazamo wako.
Kuna dini ambazo zina adhabu zake kwa makosa mbalimbali kama vile kuuwa,kuiba,kuzini na mengine mengi tu. Hayo yote yanafanyika hapa hapa na si kwamba ukiiba unaachiwa kwa kutishwa kwa kuwa kuna moto kwa Mungu,sasa wewe unaposema watu wametunga tu hayo mambo ya moto ili kuwatisha watu kufanya maovu,labda ungeeleza ni maovu yapi hayo?
Bado nashindwa kukutofautisha na mwenzako nilom quote wote mmebez kwenye vitisho kuliko kutoa majibu ya mleta mada nadhani ukileta majibu itapendeza zaidiNyie mnaopinga uwepo wa Mungu salama yenu mpinge tu bila kuleta dharau na kashfa dhidi Yake vinginevyo "to hell".
Kuna mgiriki mmoja alikuwepo Kilosa (Morogoro) miaka ya nyuma 70s au 80s, yeye alikuwa anasumbuliwa sana na mafuriko sehemu moja ya shamba lake, siku moja akaamua kufanya ukarabati na kuweka daraja kuyadhibiti maji na akaweka tuta kubwa sana kwa gharama kubwa na alipomaliza akatamba hadharani kwamba:- "hata akija Mungu na mjomba wake hawawezi kung'oa hilo tuta na daraja".
Kesho yake tu ikanyesha mvua kubwa na ikasomba kila kitu na hali ilikuwa mbaya mno kuliko ilivyokuwa siku zote hapo katika mafuriko ya awali,
Watu wakamkebehi yule mgiriki, wakamwambia huyo aliyefanya gharika hiyo ni "mjomba wa Mungu" na Yeye mwenyewe bado hajaanza gharika lake.
Tahadhari:- mnapokanusha uwepo wa Mungu hiyo ni hatua ya awali ya kuelekea kumdhihaki na hapo ndipo mtakapo tambua kwamba Yeye yupo.
Nimetaja moto ni kwa sababu ni jambo la kiimani,suala la kwamba waliyofanya maovu watakuja kuchomwa moto na Mungu ni jambo la imani ambalo linaelezwa kwenye dini.unamaanisha kwamba kitisho pekee ambacho nimekiieleza ni moto Siku ya mwisho? au nimeelewa vibaya? (nifafanulie swali lako kama nimeelewa bibaya)
ila kama nitakuwa nimekuekewa vizuri acha nikujibu kama ifuatavyo "hata hizo adhabu za direct zinazotolewa na binadamu wenzetu ni moja ya vitisho ili watu wasifanye maovu kama kuiba,kuzini na kuua." ukifuatilia post yangu vizuri utaona nimekuwekea kifupi 'nk' nikimaanisha na kadharika.
maovu hayo kama yangefanyika katika jamii kwa kuwa akuna kipingamizi basi dunia isingekuwa salama sana.
Bado nashindwa kukutofautisha na mwenzako nilom quote wote mmebez kwenye vitisho kuliko kutoa majibu ya mleta mada nadhani ukileta majibu itapendeza zaidi
Thibitisha Mungu hayupo
Kuna mtu kathibitisha Mungu yupo?
Au longolongo za kila siku tu?
Unajua kusema hauwezi kuthibitisha kisichokuwepo kwa sababu hakipo,ni sawa na kusema haina haja ya kuthibitisha kuwepo kwa kitu kwa sababu teyali kipo?kisicho kuwepo hakithibitiki huwezi kukithibitisha kwa kuwa hakipo wewe unayesema kipo ndio unayetakiwa ukithibitishe kama kipo
Kama ambavyo wewe ulivyoshindwa kueleza tu ni vp akili iwe na power ya ku control watu,ila bado unaamini hadithi za kwamba et akili ina power.Hawawezi kuthibitisha kwakuwa hayupo ni hadithi tu hizo
Huwezi kujua kuwa watu na vitu vilikuwepo kabla ya kuwepo kwako. Hata mzazi haitwi mama au baba hadi awepo (mtoto) wa kumwita hivyo.Usipokuwepo wapi sasa? maana kiuhalisia kabla ya wewe kuwepo kuna watu walikuwepo na ndiyo chanzo cha wewe kuwepo,sasa utasemaje usipokuwepo na hakuna kilichopo?
Kiuhalisia ili apatikane huyo mtoto lazima kwanza mwanamke na mwanaume wafanye tendo la ndoa na mimba iingie,kama ni hivyo basi lazima ukubali kuwa watu walikuwepo kabla yetu sie.Huwezi kujua kuwa watu na vitu vilikuwepo kabla ya kuwepo kwako. Hata mzazi haitwi mama au baba hadi awepo (mtoto) wa kumwita hivyo.
kisicho kuwepo hakithibitiki huwezi kukithibitisha kwa kuwa hakipo wewe unayesema kipo ndio unayetakiwa ukithibitishe kama kipo
Yawezekana understanding yako ikawa ndogo, au umetia kufuli akili yako kisiingie chochote kinachothibitisha uwepo wa Mungu,in that case however hard someone tries to make you understand the concept of God existence you will never ever grasp it deliberately. Mark the words of wisdom 👇🏻
"Huwezi kumuamsha mtu aliyejifanya kulala, lakini unaweza kumuamsha mtu aliyelala kiukweli".
Mnakazania tu:- " thibitisha kama Mungu yupo"----- ilhali ukiulizwa toa sababu ya wewe kuwepo hapa duniani jibu ni sufuri halafu mnakimbila maswali yaliyojuu ya akili zenu na hata mkijibiwa mnashindwa kuelewa majibu.
Kama huna jibu la sababu gani wewe upo hapa duniani basi huna tofauti na Mbuzi, Ng'ombe nk, kwa sababu wanyama hawajitambui, they are driven by instincts and not conscious mind. Wewe ulisikia wapi Mbuzi au Mbwa anazungumza juu ya kuwepo kwa Mungu?. Sasa hatuwezi kuishi kama Mbuzi nk.
Unajua kusema hauwezi kuthibitisha kisichokuwepo kwa sababu hakipo,ni sawa na kusema haina haja ya kuthibitisha kuwepo kwa kitu kwa sababu teyali kipo?
Kama ambavyo wewe ulivyoshindwa kueleza tu ni vp akili iwe na power ya ku control watu,ila bado unaamini hadithi za kwamba et akili ina power.
Kuwa kwenye uhalisia kwa maana ipi?Kuwepo na kutokuwepo kipi kipo katika uhalisia?
Na watu wa dini nao wangekuwa wanasema kama unadhani kungekuwepo hata hii mijadala?Sijashindwa kukuelezea ila nilitaka kukuonyesha kuwa ukitaka kuelewa vizuri nikupe reference za ukweli uchambue hapa tunapeana njia hatuwezi kujifunza au kueleza yote humu
Kuwa kwenye uhalisia kwa maana ipi?
Unajua kwanza kuwa hakuna mwenye kutaka mthibitishe kitu ambacho hakipo bali mnatakiwa mthibitishe kutokuwepo kwa hicho kitu? Unaposema haiwezekani kuthibitisha kisichokuwepo kwa sababu hakipo,huwa unakusudia kuonesha kitu ambacho hakipo na ndiyo maana unasema haiwezekani.Namaanisha kuna mmoja kati hivyo vitu viwili anamtegemea mwenzake kuwepo kwake yaan hawezi kukaa pekee yake
Ngoja nukupe mfano ili tuelewane vizuri nini maana ya giza