Makosa 10 aliyotenda Mungu

Mtoa mada naona umeshiba ugali maharage sasa umeamua kunya hadharani!
 
Kweli lkn huyu baado hata punje haijai,hivi huyu jamaa na farao nani anaongoza kwa dhiaka?
 
Mbona unahaha sana??? wao kama wamemdhihaki Mungu mimi inanihusu vipi??? Kwani Mungu si anajua mahusiano yake na watu wake??? Kama watu hawana uelewa juu ya Mungu, kwanini awauwe badala ya kuwapa imani na kuwaelimisha???...mimi nahitaji majibu wewe unaniforwadia jumbe zisizo na mashiko....Kwahiyo ambao hawakumdhihaki Mungu waliishi milele???
 
Mtoa mada unajaribu ku-temper na mziki mzito sana, kwa Upumbavu.
Ayubu 1;22
Ayubu 24;12

Mathayo 12:36
Zabur 14:1

Ukatubu.
 
Mtoa mada unajaribu ku-temper na mziki mzito sana, kwa Upumbavu.
Ayubu 1;22
Ayubu 24;12

Mathayo 12:36
Zabur 14:1

Ukatubu.
Umetoa majibu mazuri sana, ila yapo OP na hoja zangu...mf. kwenye zab. 14:1 inasema ''Mpumbavu anasema moyoni mwake hakuna Mungu, matendo yao ni maovu kabisa, hakuna atendaye mema'' Je kunasehemu niliyosema hakuna Mungu??? kama ipo onesha.,,,,Ayubu 1:22 wewe jua kunatofauti kati ya kulaumu na kuuliza, mimi sijalaumu bali nimeuliza, ndio maana niliweka alama za kuuliza. Mathayo 12:36, kwani maswali yangu hayana maana??? mbona Yesu aliulizwa maswali na kujibu??
 
Walevi WA dini hao ndiyo hawajiulizagi wanao wasisitiza waamin uwepo wa mungu., wenyewe ni illuminat wakubwa sana..kiukweli mungu amuondowe shetani Kwa mana naona anamzidi kete aisee.
 
Hakuna mwenye mwili anayeweza kumpima
Mungu kwamba ametenda makosa ama la
Maana ujinga wa Mungu ni zaidi ya weredi wa Mwanadamu.
 
Nimeipenda hii

(whats a Mistake)? a wrong way of doing something,misguided action,inaccuracy!!!!!!!!
=>Kusema Mungu ana makosa ni sawa na kusema hajakamilika(perfection) Kwaio hana tofauti na sisi Jambo ambalo ni kosa,Lucifer Alitenda Hivi Hivi
 
Walevi WA dini hao ndiyo hawajiulizagi wanao wasisitiza waamin uwepo wa mungu., wenyewe ni illuminat wakubwa sana..kiukweli mungu amuondowe shetani Kwa mana naona anamzidi kete aisee.
wanasema tufumbe macho tuite uwepo wa Mungu, wakati biblia inasema Mungu yupo kila sehemu, na kipengele kingine kinasema wakusanyikapo wawili kwa ajili ya neno langu, mimi nipo kati yao.. hii ya kuita uwepo wa Mungu ndo kama ile ya mganga kupandisha mashetani kuwaita WAUNGWANA, hamna tofauti.. sasa kama hizi practice za kiganga zipo hadi makanisani hili ni tatizo pia.. kumuita Mungu angali yupo mahala popote ni sawa na kutafuta peni wakati umeishika mkononi.. HII NI ISHARA YA KUTOKUAMINI NA KUTOJIAMINI.
 
"Ee baba Mungu Wa mbinguni, naomba unisamehe kwa sababu nimefungua Uzi huu nikakuta matusi yanatukanwa juu yako, baba naomba uwasamehe watu hawa kwa sababu hawajui kuwa wewe ndie Mungu ulie waumba, samehe uovu wao.
Wape rehema bwana. Akili hizi sio zao Bali ni akili za yule mwovu.
Ninaomba ktk jina LA Yesu, Amen"
 
Hahahahaa nimecheka sana mkuu....kwahiyo baada ya kukosa cha kujibu umeamua kutiririsha maombi??? lol aya bhana.
 
Watu wawili walipanda kwenda Hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo, na mwingine mtoza ushuru.
Luka 18:11 Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: `Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtoza ushuru.
18:12 Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato langu.`
18:13 Lakini yule mtoza ushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: `Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.`
Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa."

KUWA MPOLE BLAZA.
 
Hahahahaa nimecheka sana mkuu....kwahiyo baada ya kukosa cha kujibu umeamua kutiririsha maombi??? lol aya bhana.
Hata baada Ya Yesu kusurubishwa msalabani, aliwaombea msamaha wale waliomtesa.

Nami pia nakuombea Mungu akusamehe ktk huu Uzi uliouleta.
 
Mimi ni mpole, pia ninalotumaini kuu ndani ya kristo Yesu.
Na nimemkiri Yesu kama Bwana na mwokozi Wa maisha yangu.
 
Hamna shukran nyie watu!! Hivi magufuli afanye kipi ndo mshukuru?? Mi najua hata rais akifanya mazuri 100% bado mtamkosoa tu. Sijui shida yenu nini hasa??
 
Mimi ni mpole, pia ninalotumaini kuu ndani ya kristo Yesu.
Na nimemkiri Yesu kama Bwana na mwokozi Wa maisha yangu.
tatizo ni kuelewa huu uzi unataka nini..sistaajabu sababu hata maswali ya short notes watu huandikaga essay.. bado hujatoa elimu, umehukumu.
 
Mkuu usiwe mkali sana na jaribu kupunguza ukali wa maneno hata kama hauamini uwepo wa Mungu.
Pascal aliyetengeneza Pascal programming language alisema "ni bora kuamini kuna Mungu ili hata usipomkuta utakuwa hujapoteza ila ukiamini hayupo then akawepo ni hasara kwako".
Mkuu unachotakiwa kujua Mungu ana utaratibu wake ,ili atende jambo kuna taratibu unatakiwa ufuate.
Wewe unakimbilia kwa wangojwa lakini mbona kuna mambo mengi tu makanisa wanahangaika kutafuta fedha za ujenzi kujenga makanisa kwa ajiri ya kukutana na Mungu.Mungu amgeweza kutenda muujiza wakapata pesa wakajenga lakini kwa nini anaacha watu wanajenga makanisa kwa shida na kuhangaika?
Pole sana kwa yote ambayo umekuwa unaandika lakini ni kwa sababu hujui mwisho wa yote ni nini?Naamini wewe ni msomi na wasomi na wengi hapa JF wasio amini uwepo wa Mungu ni wa somi kwelikweli akiwemo Kiranga.lakini nataka nikwambie kila jambo lina wakati wake kuna mtu amekumention anataka umsaidie kuhusu ndoto aliyo ota.Mimi jambo lile naliangalia tofauti.
Njia sa Mungu si kama za mwanadamu na mawazo yake si kama mawazo yako.Tatizo hamfatilii mambo,kwa mfano tunasema Mungu ni mtakatifu,neno matakati au holy kwa kiebrania maana yake ni "separated"
The Hebrew word for holy is “qodesh” and means “apartness, set-apartness, separateness, sacredness”
Mungu yuko juu sana ya ufahamu wa mwanadamu so nilishawahi kuandika hapa ya kwamba huwezi kuprove uwepo wa Mungu kwa kutumia njia za kianadamu.Hili jibu si langu Mungu mwenyewe alitamka kupitia watumishi wake nikiwa mahali pale.
Nakupa pole kwa sababu hujui nini kinakuja mbele yako kama ambavyo wewe ukimwelezea mtu wa kijijini ambaye hajasoma hata primary athari za global warming au weapons of mass destruction hawezi kukuelewa kwani hana ufahamu wa mambo hayo.The more you become educated the less happy you become,hatujisikii vizuri wewe na wengine wa jamii yako msioamini kwamba kuna Mungu ingawa si lazima uamini ninacho amini mimi you have your rights .
Shetani ni mjanja wewe unataka kutumia elimu ya kibinadamu kuprove kwamba Mungu yupo hiyo ni sawa na gari reprove kwamba kuna mwanadamu yupo wakati mwanadamu ametengeneza gari au robot iprove kwamba kuna mtu.
Ushauri wangu kwako kuwa makini na muda mwingine ni bora kukaa kimya,wanasheria wanasema kutokujua sheria si kigezo cha mtu kusamehewa akivunja sheria.Hii principle ilianza na Mungu whether umelisikia neno lake au la utahukumiwa kwani sheria zake alisha ziandika kwenye mioyo ya wanadamu tangu zamani.Shetani hajalala ,ile njia ni nyembamba na imesomngwa na miiba,waionao ni wachache.
Ukifika muda wa Bwana kukuokoa wewe atakuokoa ,wanadamu hata wakuambie vipi hata tuelezee vipi kama muda bado utaendelea kuwa hivyo ulivyo.Nakuambia haya kwa sababu nnimemwona katika maisha yangu.
 

Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…