Makosa 10 aliyotenda Mungu

Labda nukuulize unajua kama mpaka sasa hakuna anaejua muda?
Ngoja nikuthibitishie hilo leo siku gani na tarehe ngapi?
Kaka wewe ndio huujui muda. Kabla sijajibu swali lako,nataka ukiri ya kuwa wewe na wa mfano wako ndio huujui muda.

Ukikiri hilo,mimi nakuja na faida kadhaa kuhusu muda.
 
"WA IDHAA JAA AKA LADHIYIINS YU-UH MINUUNA BII AYATIINA FAQUL SALAM ALEYKUM"
"Na wanapokujia wanaoziamini ishara zetu waambie,Amani iwe juu yenu" Al anaam 6:54
Bro nilikukanya kuhusu huu mtindo wa kuandika aya za Qur'an kinyume na asili yake,jambo hili lina chukiza sana na linaondoa asili bali hata maana ya aya.

Sasa makinika kwalo,ili usizidi kukosea.
 
"WA IDHAA JAA AKA LADHIYIINS YU-UH MINUUNA BII AYATIINA FAQUL SALAM ALEYKUM"
"Na wanapokujia wanaoziamini ishara zetu waambie,Amani iwe juu yenu" Al anaam 6:54
Bro unanipa simanzi sana. Unanukuu aya halafu unasema hakuna anae jua MUDA ?

Nahisi hauko serious.
 
Thibitisha Mungu yupo.
Kwanza lazima ujue kuwa Mungu hatumuoni kwa macho bali
tunamfahamu kwa akili zetu katika
kuchunguza dalili mbali mbali
zilizotuzunguka.

Kingine matumizi ya kwanza ya akili
tulizotunukiwa ni kuyakinisha kuwepo kwa
Muumba na sifa zake. Msisitizo wa
matumizi ya akili na fikra zetu katika kazi
hii ya kumjua Mungu na sifa zake kwa mujibu wa uislam kupitia Qurani unabainishwa katika aya zifuatazo:

"Na katika ishara zake, (za kuthibitisha
kuwepo kwake na uweza wake) ni kuwa
amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu
ili mpate utulivu kutoka kwao, naye
amejaalia mapenzi na huruma baina yenu.
Bila shaka katika haya zimo ishara kwa
watu wanaofahamu" (30:21)

"Na katika
ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni
kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana
lugha zenu na rangi zenu na (mengine
yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo
huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo
ishara kwa wenye ujuzi". (30:22).

"Na
katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na
(kuamka) mchana, na kutafuta kwenu
fadhila yake. Hakika katika hayo zimo
ishara kwa watu wanaosikia." (30:23)
"Katika kuumbwa mbingu na ardhi na
mfuatano wa usiku na mchana ziko hoja
(za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu ) kwa wenye akili". (3:190).

Pia Na katika watu na wanyama wanaotambaa
na wanyama (wengine), pia rangi zao ni
mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah
miongoni mwa waja Wake ni wale
wataalamu (wanazuoni).
 




Alas, why quoting the Qur'anic verses for an agnostic atheist to ponder over them??

He consistently denies His (God) existence how can he then incline to His words??

The only thing,I suppose, he should be made to understand is the surrounding nature and its embodiments including himself, he needs be made conscious of himself as the most complex being to ever be made-------- be made by WHO?? , Can his complexity just came into being be a chance??, is the whole creation the game of chance or the game of chess?? and etc.
 
Mkuu Tumia Lugha ya Kiswahili .
 
Mkuu Tumia Lugha ya Kiswahili .



Samahani sana mkuu,

Nilikuwa nasema hivi huyo ndugu hakubali kabisa uwepo wa Mungu na wewe umenukuu aya za Qur'an ili azisome, lakini hatari ninayoiona ni kwamba atazipuuza tu kwani kama Mwenye hayo maneno (Mungu) anakataliwa na kupingwa kwamba hayupo vipi maneno yake yatakubaliwa kwamba yapo??😁😁

Nadhani Kinachotakiwa kwa watu kama hao ni kurejea ishara za mazingira tunamoishi na maumbile yetu sisi wenyewe tumjulishe kuwa mwanadamu ndiye kiumbe "the most complex" akiwemo na yeye mwenyewe----- sasa ni nani kamuumba binadamu na complexity yake??, nani kaumba ulimwengu wote?? nk.

Hayo ni maoni yangu tu.
 
Kwanza lazima ujue kuwa Mungu hatumuoni kwa macho bali
tunamfahamu kwa akili zetu katika
kuchunguza dalili mbali mbali
zilizotuzunguka..

Hapa hujathibitisha Mungu yupo, umeandika tu Mungu hatumuoni.

Sijaomba unioneshe Mungu kwa macho, nimekutaka uthibitishe Mungu yupo.

Hapa umefanya tamko ambalo halijatakiwa na wala halina sababu, kwa kuwa hakuna chochote nilichoandika kilichotaka unioneshe Mungu, kwa kifupi, umeandika kitu irrelevant.

Kama ungepewa idadi maalum ya maneno ya kutumia kunithibitishia Mungu yupo, ungeipunguza idadi hiyo kwa maneno hayo 19 ya juu bila sababu.

.
Hii ni abracadabra tu, matumizi ya kwanza ya akili ni yapi? Unayajuaje haya ni ya kwanza? Unatumia nini kujua matumizi ya kwanza ya akili? Yanayakinishaje kuwepo kwa Mungu na sifa zake? Sifa gani? Unajuaje yanayakinisha kuwepo kwa Mungu tu na si kitu kingine chochote?

Qquran ina contradictions kibao, unajua hilo? Unajua kwamba kitabu kilichojaa contradictions hakiwezi kuangaliwa kama kitabu kinachoweza kutuambia ukweli kuhusu uwepo wa Mungu?


Hujathibitisha Mungu yupo, unahubiri kutoka kitabu kilichojaa uongo na contradictions.

"Na katika
ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni
kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana
lugha zenu na rangi zenu na (mengine
yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo
huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo
ishara kwa wenye ujuzi". (30:22)..

Huu si uthibitisho kwamba Mungu yupo, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?


Nina shaka kama hata unaelewa uthibitisho ni nini.

Pia Na katika watu na wanyama wanaotambaa
na wanyama (wengine), pia rangi zao ni
mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah
miongoni mwa waja Wake ni wale
wataalamu (wanazuoni).

Allah angekuwepo asingewanyima wanayama akili za kujua mambo mengi, wakafanywa watumwa wa watu.

Wwanyama kuwa hivyo si haki, Mungu wa haki asingeumba hivyo.

Kuwepo kwa tofauti hii ni uthibitisho kwamba Allah hayupo, ni hadithi tu.
 
Wewe umejuaje makosa wakati umeshindwa kutengeneza hata kimoja wapo hapo
 

Bro hivi uthibitisho kwako wewe ni nini ? Yaani ili mtu akuthibitishie jambo au suala fulani inabidi atimize vigezo gani ?

Mimi nina jua uthibitisho ni nini. Ila nataka wewe useme ili ukithibitishiwa usilete talbisi za ibilisi.

Ndio maana kule nilikuwekea masharti ili tuende sawa.
 

Unarudia rudia tu maswali yale yale, tushajadili haya.

Awali kabisa, uthibitisho ni lazima uweze kupimika. Usipoweza kupimika hauwezi kuwa uthibitisho.

Pili, uthibitisho ni lazima uwe logically consistent. Sio uthibitisho hauna logical consistency. Sio nakuuliza kuthibitisha kwa njia inayoweza kuwa falsified, wewe unahubiri kwa ushairi vague ambao hausemi lolote linaloweza kuwa fasified.

Tatu, uthibitisho ni lazima usiwe self contradictory, usiwe na elements zinazojipinga zenyewe. Sio tunathibitisha wewe umeoa, unaniambia umeoa, halafu hapo hapo unniambia wewe ni bachelor huna mke.This is a special case of lacking logical consistency.

Nne, uthibitisho ni lazima uweze kutabiri vitu specific, kwamba vitatokea mbeleni, katika muda specificna realistic, kwa namna specific,vinayoweza kupimwa, katika maisha yetu haya na si habari za baada ya kufa ambako hatujui hata kama tutaweza kupima chochote.

Tano, uthibitisho ni lazima uwe na ushahidi usiopingika kimantiki katika fremu yenye kukubalika na pande zote. Sio unathibitisha mambo kwa mistari ya Quran, wakati Quran yenyewe kwangu ni kitabu chenye makosa mengi sana ya kujipinga chenyewe.

Hayo ni machache tu kwa sas.
 
Ndugu jipe muda angalao dakika moja kuwaza wakati mgumu waliopitia watu waliozama na kivuko huko Ziwa Victoria. Hakuna Mungu mkatili kiasi hicho. Eti tunasema ni mapenzi ya Mungu. Dhana ya Mungu ni ukomo tu wa kufikiri. Hakuna kitu Mungu ndugu, ni dhana inayowakilisha fikra za watu tu.

Mungu anayesujudiwa hapaswi kuwa mkatili namna hiyo. Watu 200 wanakufa kwenye ajali ya ndege. Is God doing organised deaths to save time? Haiingii akilini. Hakuna kitu Mungu ambacho watu wanajenga picha kipo mahali fulani kinaratibu maisha ya kila kiumbe. Hakuna. Ni kwa kuwa tu tumejipa ukomo wa kufikiri.
 
Mkuu Baba Swalehe.

Hata mimi nakuunga mkono unaposema kuwa Mungu yupo, lakini unaposema kwamba kuna watu wanaozaliwa wakiwa wajinga hapo sikuelewi hata kidogo,je waweza kufafanua hapo ??!!.

[emoji523]Elimu ni bahari[emoji523]
Ikiwa watu wanazaliwa wakiwa wajinga, kosa ni la nani? Muumbaji, siyo? Kwa hivyo yeye ndiye atakuwa na ujinga kwa kushindwa kutumia uwezo wake kuumba watu werevu. Simple logic.
 
Bro hapa hujaeleza kuthibitisha na vigezo vya kuthibitisha.

Umezungumzia mantiki,suala la mantiki tulishalijadili kadhalika. Mantiki haiwezi kuingia latika vigezo vya kuthibitisha sababu ya misingi yake kwayo imejengeka. Mantiki imejengeka katika ujumushaji wa hoja mbili katika msingi usio sahihi tena wa dhana. Mfano tukisema Mdudu ana uhai,jiwe halina uhai. Kwa kauli hizo mbili,hitimisho la kimantiki litakuwa "Jiwe si mdudu". Kwani nani alikwambia ya kuwa jiwe ni mdudu ?

Kaka hatuwezi kujenga ithibati kwa kutumia dhana. Unaposema suala la Qur'an kujipinga yenyewe huu ni uongo,kwa sababu huwezi kuleta hoja yenye nguvu juu ya madai hayo.

Kuna mfano mmoja umeutoa unaonyesha ni jinsi gani ulivyo dhaifu katika suala la kutoa mifano. Hawezi kutoa mfano isipokuwa mtu mwenye maarifa machache juu ya suala husika. Umesema kwa mfano mtu akiambiwa wewe umeoa halafu akakubali kisha akasema yeye ni bachelor,Bro hayasemi haya isipokuwa mjinga juu ya suala hilo.

Kaka haijawahi hata siku moja tangu kuumbwa kwa dunia na mbingu ya kuwa jambo kama haliingii akilini mwako basi likataliwe.

Naendelea.......
 
Inakuwa ngumu mtu kukuelewa mkuu ikiwa hujavunja hoja za misingi ya hiyo dhana,ukiishia tu kupinga yale yenye kuelezwa kuhusu Mungu bila kupinga msingi wenyewe wa hiyo dhana inakuwa sawa na bure.
 

Hili suala la kuingia akilini ndio tatizo la wengi. Mfano kaka mkubwa umesisitiza suala la uwepo wa Mola muumba ni matokeo ya fikra za mwanadamu,ukweli ni kwamba haya ni madai tu,katu huwezi kuyathibitisha.

Narudi katika kulalama kwako. Mola wetu ni muadilifu sana,alipoumba uhai akaumba na kifo,na akasema na mpaka tusivyovijua ameviumba katika hali ya uwili,huu ndio ukamilifu wake.

Jalia ya kama ni kweli suala la Mola muumba ni kutokana na uoga wa binadamu,utasemaje kuhusu suala la elimu ya tiba,sababu haya ni matokeo ya binadamu katika kutafuta utatuzi,ina maana ni sahihi kuibatilisha elimu ya tiba kisa ni matokeo ya binadamu kuogopa kifo na maradhi ? Ndio maana akatafuta tiba ya maradhi ?

Sasa mnaposema uwepo wa Mola muumba ni matokeo ya fikra za mwanadamu,huwa mnawaza nini ?

Mola wetu yeye ndie amemba muda na kutuwekea hali za kudhibiti muda,ametuwekea usiku na mchana kujua idadi ya miaka na kuthibiti hesabu.

Akaumba Kifo ili kutimia kwa uumbaji wake. Kaka wewe mbona hulalamiki leo kwanini amekupa uhai na unaendelea kumkana ?

Huoni kama yeye ndie anaekupa rizki na ukazidi kumkufuru badala ya kumshukuru ?

Naendelea...
 
Umesema kwanza awali uthibitisho lazima uweze kupimika,lakini hujasema ni ipi mizani ya kuipima hiyo ithibati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…