Makongoro Nyerere apata ajali ya gari Babati

Jana.Makongoro alipokuwa anarudi Arusha baada ya kutoka Dodoma,amemgonga ng'ombe amepata ajali. Hakuumia. Alikuwa peke yake ndani ya gari.Nasikia ameweka picha katika Whatsup lakini sijaziona.

========

Babati. Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere amenusurika katika ajali baada ya gari lake kuwagonga ng’ombe saba kwenye eneo la Makatanini, Babati mkoani Manyara.

Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anatoka Dodoma kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho kwenda Arusha.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Francis Massawe amesema ajali hiyo ilitokea saa 1 usiku jana na kuwaua ng’ombe saba na kondoo mmoja.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo haikuwa na madhara ya binadamu, ni mifugo hiyo kuvushwa barabara sehemu isiyo na kivuko rasmi cha mifugo na katika tukio hilo. Mchungaji wa mifugo hiyo, William German alikimbia baada ya ajali hiyo.

Chanzo: Mwananchi
.........Nasikia ameweka picha katika Whatsup lakini sijaziona.........Endrew Nyerere akiongelea ajali aliyopata Makongoro Nyerere !!! Hawa si ni mtu na mdogo wake, kwa nini asimpigie simu na kuthibitisha au kama simu ya Kaka yake haipatikani, ampigie Shemeji yake !!!
 
Acha kukariri wewe, kwahiyo na kazi kwelikweli utasema job true true?
Mzee wa kukurupuka haujambo? Ukimwambia mtu: Usinywe na kuendesha maana yake umemkataza asifanye vyote viwili. Ukimwambia usiendeshe ukiwa umekunywa maana yake anaweza kunywa na kuendesha isipokuwa hatakiwi kuendesha akiwa amekunywa.
 
1469519138539.jpg
 
Jana.Makongoro alipokuwa anarudi Arusha baada ya kutoka Dodoma,amemgonga ng'ombe amepata ajali. Hakuumia. Alikuwa peke

Babati. Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere amenusurika katika ajali baada ya gari lake kuwagonga ng’ombe saba kwenye eneo la Makatanini, Babati mkoani Manyara.

Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anatoka Dodoma kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho kwenda Arusha.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Francis Massawe amesema ajali hiyo ilitokea saa 1 usiku jana na kuwaua ng’ombe saba na kondoo mmoja.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo haikuwa na madhara ya binadamu, ni mifugo hiyo kuvushwa barabara sehemu isiyo na kivuko rasmi cha mifugo na katika tukio hilo. Mchungaji wa mifugo hiyo, William German alikimbia baada ya ajali hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Wakuu:
Hivi TSPCA bado ipo hapa Tanzania?
 
Amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo haikuwa na madhara ya binadamu, ni mifugo hiyo kuvushwa barabara sehemu isiyo na kivuko rasmi cha mifugo na katika tukio hilo. Mchungaji wa mifugo hiyo, William German alikimbia baada ya ajali hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Huyo Mchungaji sasa hilo jina ni la ukoo au?
​
 
Ajali nyingine zimesababishwa na mwendo kasi wa dereva na anashikiliwa na jeshi la polisi kwa maojiano zaidi. Nyingine zimesababishwa na ng`ombe na mchungaji kakimbia anatafutwa na jeshi la polisi kwa maojiano zaidi. Nchi hii ni zaidi ya ujuavyo.
 
Nimesoma tena hiyo habari kwa makini zaidi
Kwenye ajali hiyo AMEUA ng'ombe 7 na kondoo 1
.alikuwa anaendesha fuso?
.alikuwa spidi ngapi?
 
Ajali nyingine zimesababishwa na mwendo kasi wa dereva na anashikiliwa na jeshi la polisi kwa maojiano zaidi. Nyingine zimesababishwa na ng`ombe na mchungaji kakimbia anatafutwa na jeshi la polisi kwa maojiano zaidi. Nchi hii ni zaidi ya ujuavyo.

Kaazi kweli kweli. Double standard katika ubora wake. Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni.

Palikuwa na haja ya kuwafanyia Vetting hawa polisi ambao weledi kwao ni ziro. Mbona wanajulikana?
 
Back
Top Bottom