Andrew Nyerere
JF-Expert Member
- Nov 10, 2008
- 3,007
- 2,469
Jana.Makongoro alipokuwa anarudi Arusha baada ya kutoka Dodoma,amemgonga ng'ombe amepata ajali. Hakuumia. Alikuwa peke yake ndani ya gari.Nasikia ameweka picha katika Whatsup lakini sijaziona.
========
Babati. Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere amenusurika katika ajali baada ya gari lake kuwagonga ng’ombe saba kwenye eneo la Makatanini, Babati mkoani Manyara.
Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anatoka Dodoma kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho kwenda Arusha.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Francis Massawe amesema ajali hiyo ilitokea saa 1 usiku jana na kuwaua ng’ombe saba na kondoo mmoja.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo haikuwa na madhara ya binadamu, ni mifugo hiyo kuvushwa barabara sehemu isiyo na kivuko rasmi cha mifugo na katika tukio hilo. Mchungaji wa mifugo hiyo, William German alikimbia baada ya ajali hiyo.
Chanzo: Mwananchi