Makongoro Nyerere ampasulia JK! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makongoro Nyerere ampasulia JK!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwame Nkrumah, Nov 26, 2011.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Uamuzi huo ulikuwa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na maoni shawishi ya mmoja wa Wenyeviti wa Mikoa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, Charles Makongoro Nyerere, aliyesema watu wa kawaida walikuwa wakishangazwa na CCM kuendelea kukumbatia watu waliokuwa wakionekana wanashiriki katika ufisadi.
  Akichangia wakati huo katika tathmini na mapendekezo ya Kamati Kuu ya kutaka Chenge, Lowassa na Rostam wawajibike, Makongoro Nyererealisema isingewezekana Chenge, Lowassa na Rostam kuendelea kuwa na nafasi za uongozi ndani ya chama.
  Alisema wakati huo mtoa habari wetu: “ Kwanza alianza kwa kumwambia Mwenyekiti kwamba japo yeye ni Mwenyekiti wa Taifa, yeye (Makongoro) naye ni Mwenyekiti wa Mara na kwamba NEC ndio waajiri wa Mwenyekiti Taifa.
  “ Akasema anapokaa Mwenyekiti wa Taifa ni mahala patakatifu na kwa ajili hiyo pasingeweza kusogelewa na shetani, hata kama siku moja Mungu alipata kukutana na shetani barabani.
  “ Akasema kule site (kwenye eneo la ujenzi ambako yeye ndiko anakoshinda akichanganya zege na kupiga bati) wanasema na wanataka watuhumiwa wote wa ufisadi watoke kwenye nafasi zao.
  “Lowassa ni ndugu yangu.Sina matatizo naye.Najua ananipenda, nami nampenda.Lakini kule site wanasema hapana.Atoke. Tena nawe Mweyekiti ulipokwenda Monduli, ukainua mkono wake juu, ukasema hujapata kuona kama yeye (Lowassa), kule site wakauliza, sasa hii ndiyo nini?
  “Rostam simfahamu vizuri. Ninakotembelea yeye hawezi kuja na mimi siwezi kwenda anakotembelea. Sina ugomvi naye.Lakini kule site wanasema naye hapana. Ulipokwenda Igunga ukamuamsha mkono ukasema ni kama timu ya mpira iliyokamilika watu kwenye site wakauliza sasa hii ndiyo nini?
  “Nasikia Chenge wanamwita Mzee wa Vijisenti. Ni ndugu yangu. Sina hakika kama anavyo vijisenti kiasi hicho. Lakini kwenye site, si mimi, watu wanasema naye hapana, “ alikaririwa akisema Makongoro.

  SOMA ZAIDI HAPA: Raia Mwema | Lowassa apambana

  Lowasa ana nguvu kiasi gani mpaka wanachama milioni 4 wa CCM wanashindwa kumtoa?
  JK hawezi kumtoa Lowasa hata siku moja, kwa kutoa siri zao kidogokidogo ni kama vile Lowasa anamwambia JK angalia sana, nina mengi zaidi ya kusema. JK ameshikwa mateka na Lowasa. Lowasa hana cha kupoteza kama ataongea yote.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Je baada ya haya maneno JK alisema nini maana lazima atakuwa kasema kitu kama kawaid yake.Am curious .
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  JK alitaka kujitutumua na kamtandao kake, kameshindwa na sasa anampigia magoti Lowasa aliyemwita gamba!!! Wananchi pekee ndiyo walioachiwa jukumu hilo la kuling'oa gamba hilo kupitia urais 2015 endapo atagombea!!!
   
 4. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,315
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Game bado taff
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  chama cha wanafiki. Nalog off
   
 6. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Huyu Makongoro sijui Makhirikhiri ni uharo tu anaouongea.
  Baba yake alimshika mkono Mkapa na kutuambia kuwa Mkapa ni mtu safi.

  Sasa ana usafi gani kwa mali alizojilimbikizia yeye na mkewe?
   
 7. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 867
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  nahisi hutumii ubongo kufikiri,usimlaumu nyerere kumuita mkapa msafi.ni kweli mkapa alikua msafi kabla ya kifo cha nyerere na utofauti wa jk ni kuwa aliwapigia kampeni watuhumiwa wa ufisadi na wote tuliona,nyerere asingethubutu kuwapigia kampeni na ni kuwa nyerere angehamia Chadema haraka.
   
 8. m

  maselef JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nafikiri sasa tumeanza kupata picha halisi ya Chama cha Magamba. Inanikumbusha moja ya mistari katika Biblia "Asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe huyu mama". Mara wote wakatawanyika
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ngoma inoge sasa!!
   
 10. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hata shetani alikùwa malaika. "Just thinking."
   
 11. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  Kule Site Wanasema CCM ni wanafiki
   
 12. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Hakuwahi kuwa malaika bali aliishi na malaika "Just reminding"
   
 13. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...he! Kama nani?
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  sema kaka! jamaa hawa na wafuai wao ni wanafiki
   
 15. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #15
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  mmmh! alikuwa malaika mkuu
   
 16. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jamani hii habari ni ya lini? Makongoro aliyasema hayo katika kikao kilichoisha jana (25/11/2011) ni katika kikao kile cha mwezi Aprili, 2011? Naona humu JF tumeanza mtindo kulishana habari kama vile ni habari mpya kumbe ya zamani. Hata kama habari ni relevant ni vizuri ikawekwa sawa kwamba ni lini na wapi yalisemwa hayo.
   
 17. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hii habari ni muda mrefu wala si mpya
   
 18. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Naliongea hili nikiwa sina maslahi kabisa na magamba! Mkuu usisahau wakati ule kiuongozi walau Mkapa alikuwa nafuu kuliko, Lowassa. Vichwa aina ya rostam ndo walimchakachua akili yake kuelekea 2005.
   
 19. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Aisee hizi dini, kila moja na mtazamo wake kuhusu Rucifel, mweeeee!
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Ni malaika hadi leo, na ataendelea kuwa hivyo milele. sema tu yeye ni malaika alolaaniwa
   
Loading...