voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,884
Mh Rais wa JMT.
Jana wakati ukizindua na kukabidhi nyumba kwa wakazi wa Magomeni Quarters.
Ulikaririwa ukisema kwamba,watu huko mitaani wanaongea kwamba miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na JPM huenda haitakamilishwa.
Lakini ukautumia mradi ule wa Magomeni Quarters kama uthibitisho wa kauli yako, kwamba miradi yote itatekelezwa na kukamilika kwa sababu ni mojawapo ya ilani ya CCM na serikali yake.
Kisha ukasema "unawasamehe kwa sababu hawajitambuwi"
Sasa swali la wananchi wengi liko kwenye mradi mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa bwawa la umeme wa kutumia nguvu za maji huko mto Rufiji. Nyerere hydroelectric Dam.
Huu mradi ulikuwa umeanza kwa kasi kubwa chini ya serikali ya awamu ya Tano, ambapo wewe ulikuwa makamu wa Rais.
Haukuwa ukipita muda bila kuona kiongozi mwandamizi wa serikali akitembelea site ile ili kujiridhisha kwamba mambo yanakwenda kama yalivyopangwa. Pamoja na kuhimiza bidii ya kazi iendelee.
Ilifikia mahali tena ndani ya bunge, ambapo serikali kupitia waziri uliyemuondoa alitamka bungeni kwamba ujenzi ule ungekamilika kwa tarehe ambayo aliitaja na ilikwishapita.
Lakini tangu ulipoingia madarakani na kufanya mabadiliko ya serikali yako, ambapo umetuwekea waziri Makamba. Umeanza utaratibu wa porojo na ahadi ambazo hazieleweki.
Mara tumemsikia akisema kuhusu kukosekana winchi ya kunyanyulia milango ya maji ya bwawa husika. Akiahidi winchi hiyo kuletwa toka nje.
Baadae wabunge walimbana bungeni ili atowe majibu ya kueleweka lakini akaishia kuwajibu taarabu "kwamba kama shida ni uwaziri wake na urais wako Watasubiri sana"
Baada ya hapo kero ya umeme kukatika imeendelea kwa kasi ile ile ya mwaka 2010 - 2015.
Waziri husika anaendelea na Porojo zake tena kwa kejeli za hapa na pale.
Yeye kwa sasa amegeuka kuwa kama Marketing Minister wa wizara ya Nishati.
Kila uchao yeye ni kusaini mikataba mipya ya mabilioni ya walipa kodi za watanzania. Mikataba ambayo kwa ujumla wake ina utata mtupu, mara Software nk.
Hivi majuzi alikuwa Houston kule Marekani akitafuta soko la gesi yetu ya LPG. (Na huko pia ndio nyumbani kwa Richmond PLY).
Mheshimiwa katika hotuba zako pia hatukusikii ukiongelea lolote kuhusu hizi kero za Umeme.
Sasa basi...tunakuomba utembelee huo mradi ili uweze kusimamia kile ulichokiongea kwa watanzania hiyo jana pale Magomeni.
Rufiji ni karibu sana na Dar es salaam na ni suala la Day trip tu.
Badala ya kumuachia Makamba akitufunga kamba zake kila uchao.
Jambo hilo litawapa ahueni wananchi na kuwaondolea taharuki waliyonayo kuhusu kusuasua kwa mradi huo muhimu kwa uchumi wa Taifa letu.
Kero ya umeme ni kubwa kwa wananchi na inagusa sehemu kubwa ya uchumi wa wapiga kura wako.
Picha za hivi karibuni zilionyesha kama hakuna kikubwa kinachoendelea