Makonda yuko sahihi. Kubadili jina kuko kisheria

Makonda yuko sahihi. Kubadili jina kuko kisheria

Kweli buana yuko sahihi,si yeye tu bashite wapo wengi tu walobadili majina ila chadema wamekomalia hii ishu balaaa
Ukiapa na elimu ya mtu inahamia kwako si ndiyo unataka kumaanisha hvyo basi aje kwa waandishi wa habari aseme aliapa mahakamani ili kubadili jina kutoka daudi bashite hadi paul makonda
 
Kama ndo hivi Mimi kesho naapa kutumia jina la pro. Baregu na CV inahamia kwangu, yaani tunahangaisha vichwa kumbe mambo yako shortcut bwaanaa!!!
 
Bashite afungwe miaka 7....Do not touch My anointed ones or harm My prophets...alifikiria Gwajima mwalimu wa Sunday school
 
huyo Paul Muyenge na Paul Makonda ni mtu mmoja
Cheti ni cha Paul Muyenge ambacho huyo Bwana alikichukua kwa hiyo Huyo Bwana akajifanya ndo jina lake halafu akabalibadili hilo jina kisheria na kuwa kondakta!
Ndiyo maana hawezi kuthubutu kuonyesha cheti chake maana hakina jina la kondakta Bali la Muyenge!
 
Je, na kununua cheti inawezekana kisheria?
 
Nimesikia gazeti LA mwanahalisi wiki hii inayoanza kesho wataleta mzigo mzima mbivu na mbichi.

Imagine gazeti LA jamaa ambae bashite alimburuza mahakamani walipocollide kwenye issue ya wafanyakazi mwaka jana ubungo.
Je litambeba au litaua kabisaaa?Tusubiri
 
Kweli buana yuko sahihi,si yeye tu bashite wapo wengi tu walobadili majina ila chadema wamekomalia hii ishu balaaa
Unakosea, sijasikia hii ishu ikitolewa neno lolote na Chama cha CDM. Ni mtazamo wako kwamba kila mtanzania anehoji basi ni mwanachama au mfuasi wa CDM. Na kama ndivyo basi mbona itakuwa CCM ina wanachama wachache sana, huwa wanashinda vipi uchaguzi?
 
Wana JF.
Kubadilisha jina ni jambo la kawaida na linaruhusiwa kisheria ni suala la kwenda mahakamani na kuapa tu kama Paul Makonda aliamua kuchukua jina hilo badala ya Daudi Bashite na akaapa mahakamani hajavunja sharia yoyote ile ni haki yake kisheria acheni hoja za hovyo hovyo.

Mfano kwenye suala la Makonda hii inawezekana
Shule ya msingi ametumia jina la Daudi Bashite

Secondary School akatumia Paul Christian Muyenge

Chuo akatumia Paul Makonda.

Kisheria hii inawezekana kabisa na wala hakuna kosa lolote .
Sio Tatizo Sisi tunataka hicho cheti cha chake cha form four tuone Huyu Paul Christian M alimaliza shule gani ?
Ikiwa alimaliza Pamba secondary itakuwa ameruka kiunzi kimoja.
Baada ya hapo tutaka je alienda mahakamani lini kubadili jina la bashite ikiwa alienda kabla ya kujiunga kidato cha kwanza au kabla hajafanya mtihani wa kidato cha nne sawa.

Tutakuja ilikuwaje mzee wake ajiite mzee makonda siku aliyokuwa anahojiwa Na zamaradi ? Au siku Hizi mtoto skibadili jina Ndio ukoo mzima umebadili?!

Au nae alienda mahakamani kubadilisha jina?

Msitufanye sote mazuzu hapa kuna namna.

Makonda ajilaumu kuyatumia matatizo ya watanzania kupata umaarufu wa kisiasa. Angetekeleza majukumu yake kimya kimya bila kumdhalilisha mtu au kimuonea mtu sifikirii tungefika huku.
 
Wana JF.
Kubadilisha jina ni jambo la kawaida na linaruhusiwa kisheria ni suala la kwenda mahakamani na kuapa tu kama Paul Makonda aliamua kuchukua jina hilo badala ya Daudi Bashite na akaapa mahakamani hajavunja sharia yoyote ile ni haki yake kisheria acheni hoja za hovyo hovyo.

Mfano kwenye suala la Makonda hii inawezekana
Shule ya msingi ametumia jina la Daudi Bashite

Secondary School akatumia Paul Christian Muyenge

Chuo akatumia Paul Makonda.

Kisheria hii inawezekana kabisa na wala hakuna kosa lolote .
Kisheria inaruhusiwa, where is those court orders? Mwaka na mahakama gani alikwenda kubadilisha jina toka Daudi Bashite to Paul Muyenge? Nani alikuwa Hakimu na mashahidi waliokula kiapo cha kusema ukweli? Mwaka na mahakama gani alikwenda kubadilisha jina toka Paul Muyenge to Paul Makonda? Nani alikuwa Hakimu na mashahidi waliokula kiapo cha kusema ukweli? Maisha yetu yote ni science inayokubaliana na ukweli
 
Wana JF.
Kubadilisha jina ni jambo la kawaida na linaruhusiwa kisheria ni suala la kwenda mahakamani na kuapa tu kama Paul Makonda aliamua kuchukua jina hilo badala ya Daudi Bashite na akaapa mahakamani hajavunja sharia yoyote ile ni haki yake kisheria acheni hoja za hovyo hovyo.

Mfano kwenye suala la Makonda hii inawezekana
Shule ya msingi ametumia jina la Daudi Bashite

Secondary School akatumia Paul Christian Muyenge

Chuo akatumia Paul Makonda.

Kisheria hii inawezekana kabisa na wala hakuna kosa lolote .
Hapo kwenye red tu. Ni rahisi sana kumkamata kama akijitetea hivyo.
Akisema shule msingi alitumia Daudi Bashite. Mamlaka zinazohusika zitatafuta kama kuna mtu mwingine huko shule ya msingi alikua na jina Daudi Bashite ambalo mmiliki wake si Daudi Bashite ambaye ni Makonda wa sasa. Bila shaka jina lingine la Daudi Bashite litakosekana na hivyo mamalaka zinazohusika zitahitimisha kua, kwakua jina la Daudi Bashite lilikua moja tu shule ya msingi, hivyo basi mwenye jina la Daudi Bashite kttk elimu ya msingi mwaka fulani, ndiye huyo huyo Daudi Bashite ktk elimu ya sekondari ktk shule ya fulani. Hapo atakabidhiwa jina lake la Daudi Bshite pamoja na SIFURI yake , kisha kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria kutokana na uhalifu wake wa kununua cheti cha mtu na kukitumia.

Akisema alitumia jina la Paul Muyenge akiwa sekondari, litatfutwa jina la Paul muyenge huko shule ya msingi, kisha zitafutwe data zake za muunganiko na sekonddari aliyosoma. Paul Muyenge alikua na akili hivyo alichaguliwa na serikali kujiunga na sekondari. Hapo itaonekana Paul Muyenge ambaye ndio jina la Makonda la kwenye cheti, aliyetoka shule ya msingi fulani na hapo awali huyo Paula Muyenge alikua Paul Muyenge na sio Daudi Bashite. Hapo Maakonda atanyanganywa jina la Paul Muynge na atakabithiwa jina lake la Daaudi Bshite pamoja na SIFURI yake, kisha atahukumiwa kwa mujibu wa sheria kutokana na uhalifu wake wa kununua cheti cha mtu na kukitumia.

Kiufupi Bashite hana pakuchomokea zaidi ya kukubali kua yeye ni Daudi Bashite tangia shule ya msingi hadi sekondari, na alinunua cheti cha Paul Muyenge cha sekondari.
 
Tutakuja ilikuwaje mzee wake ajiite mzee makonda siku aliyokuwa anahojiwa Na zamaradi ? Au siku Hizi mtoto skibadili jina Ndio ukoo mzima umebadili?!

Au nae alienda mahakamani kubadilisha jina?
Njia ya muongo ni fupi. Alisema "mimi ni mtoto wa mzee Makonda mwenyewe". Tena neno wenyewe alilisema kwa woga kiasi, kwani moyo ulikua unamsuta. Hilo neno mwenyewe lina ukakasi. hivi kuna mtu anaweza kua mtoto wa mzee Makonda, ila sio mzee Makonda mwenyeye?
 
Kubadilisha jina sio tatizo kisheria. Mtu yeyote anaweza badilisha jina lake na kwenda kula kiapo mahakamani. Tatizo sio jina la Makonda bali vyeti vyake na tuhuma alitumia vyeti vya mtu mwingine kuendelea na masomo, na ndio akajifanya yeye ni Paul. This means jamaa ametumia false and misleading information kuendelea kimasoma which is illegal by Law. And if this is the case:

- Immigration pia inabidi waangalia ametumia vyeti gani vya kuzaliwa kupata passport. Kama ni cha Daudi Bashite, wazazi wake wameshamkana kwenye mahojiano na Zamaradi. Kama ni cha Paul Makonda akionyeshe
-Rita also need to investigate hivyo vyeti vya kuzaliwa-jamaa anatumia kipi
-NECTA nao need to investigate kwenye maswala ya elimu na kutumia majina ya mtu mwingine

Jamaa anastahili kufungwa, sema Tanzania yetu na siasa za undugunization ni ndoto tu. Ila ushahidi ukipatikana watu wapeleke ubalozi wa Marekani na UK. Jamaa watamuoji vizuri kwa undani akienda kuomba visa. those guys dont f*** about kwenye masuala ya false information
 
Sijawahi kutegemea kama huyu mwamba siku moja atamwaga machozi na kilio ch kwikwii.....
Analilia tonge la serikali, Bwana RC Bashite siyo mwajiriwa wa serikali akitumbuliwa kwenye cheo chake cha kisiasa serikali atabaki kuisikia kwenye bomba....maana serikali kamwe haiajiri mtu wa darasa la saba.....
 
Back
Top Bottom