Makonda: Walimu kusafiri bure

Makonda: Walimu kusafiri bure

Hao askari pamoja na ubabe wao,uniform na mamlaka bado wanaitwa "maiti' kwani sio hiari yao wenye mabus ndio itakuwa walimu wetu?
Atafute njia nyingine kuliko hiyo ambayo walimu wetu watanyanyaswa, kutukanwa na kudhalilishwa mpaka watauchukia huo ualimu bure!
Wazo lake laweza zuri lakini sio kwa wakati huu
Mkuu hilo ni wazo la kukurupuka tu na kukosa la kuongea,hakuna msafirishaji atakaye kubali kumsafirisha mwalimu kwa agizo la makonda, hilo ni ndoto tu
 
Makonda mbunifu, tumpe mda kabla yakuponda
Hapo kuna ubunifu gani?naona mnaota tu nani akubali kusafirisha walimu kwa agizo la makonda?makonda ni nani ndani ya taifa la tanzania?
 
Umuhimu wa mwalim ni Mkubwa kuanzia kwa mabos was Magar mpaka kwa makondakta wenyewe wali fundishwa na walim na wtt wao wanafundishwa na walim
 
Mimi naona ni Good idea, Kama mwanajeahi au askari anasafiri bure.. Kwa nini mwalimu asidafiri bure na yeye? Wawe na vitambulisho tu... Mwalimu ni mtu muhimu sana ...
Hiyo ya wapiganaji wetu kusafiri bure haikuwa ni agizo la mtu mdogo kama makonda
 
Kwanini wasiwaongezee hela ya nauli ili wajue usafiri gani watatumia....
Na pia kusema kuwa wawahi shuleni wakati wanaishi mbali hata utoe nauli haisaidii kitu
 
Na hii ndiyo solution...kwanza ili eti itawasaidia kuwahi kazini doesn't make any sense; labda hilo la kuwapunguzia ukali wa maisha, ambalo hata hivyo, kama wapo serious, basi wawape transport allowance ya angalau Sh.2000/day kuliko kusema wapande kwenye daladala bure.

Mkuu wa wilaya ya.kinondoni amesema yupo kwenye mpango wa kuwezesha walimu kusafiri bure kwenye daladala kwenda kazini kama njia ya kuwasaidia kuwahi na kuwapunguzia makali ya maisha.

Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mke wa raisi mwl Janet Magufuli ambaye amekiri kuwa kwa sasa anamajukumu mengi hasa yakumsaidia mheshimiwa raisi.

Sasa hapa najiuliza hawa wamiliki wa magari watakubali? Na je walimu watakuwa na unifomu.au watalazimika kila wakati kuonesha vitambulisho? Na je hilo litakuwa suluhisho la kudumu? Na je watumishi wengine wao watajisikiaje ? Source Azam tv- habari ya saa 2 usiku.
Kama sio moja ya solution basi angalau kichwani mtu unaweza ukaona Makonda ana lengo gani, kama mnaona sio solution, unapopinga au kukosoa muwe mnatoa sababu za kupinga na kukosoa kwa kutoa mbinu mbadala.
 
Kama sio moja ya solution basi angalau kichwani mtu unaweza ukaona Makonda ana lengo gani, kama mnaona sio solution, unapopinga au kukosoa muwe mnatoa sababu za kupinga na kukosoa kwa kutoa mbinu mbadala.
Makonda mimi namkubali sana... wakati wengine wanaanza kumkubali sasa mimi nilimkubali tangu kitambo lakini katika hili, hapana! Hapana si kwamba haiwezekani au hawezi ku-facilitate hicho kitu lakini hapana coz' issue yenyewe itakuwa chanzo cha embarrassment kwa walimu! Hata Wajeda wanavyopanda bure makondakta(kazi kwelikweli) huwa wana-mind sana sema ndo vile tena wanawaogopa! Angalau tungekuwa na mfumo wa seasonal tickets; hiyo ingekuwa rahisi kinyume chake watoe Transport Allowance.
 
Awe anawapa gharama za usafiri kwa mwezi hii itawasaidia
 
Kwa kuzingatia mantiki ya madhumuni ya kusafiri bure, heri daktari apewe huo upendeleo kuliko mwalimu. Hao askari wamepewa hiyo fursa kwa sababu ya urgency, wala sio sababu za kiuchumi au kipato. Askari hatakiwi kupanga foleni iwe ATM au barabarani kwa kuwa anawajibika kuangalia usalama as urgent as possible. Hatakiwi kuwa na kikwazo cha kusafiri from point to point. Sasa mwalimu ana uharaka gani wa kuhatarisha maisha immediately? Ndio maana nikasema heri apewe daktari kuliko mwalimu
 
Mwalimu huyu huyu au mwingine? Hakuna kitu kibaya kama kuwa biased, hivi Madaktari na Manesi nao hawastahili? Na wengine je?
Mwalimu kwanza wengine wafuate, hata ww umepata kufahamu kusoma na kuandika kwa kufundishwa na Mwalimu, na hata hao Dr, nurses, Prof. Wote wmefundishwa na Mwalimu!!
 
Mimi naona ni Good idea, Kama mwanajeahi au askari anasafiri bure.. Kwa nini mwalimu asidafiri bure na yeye? Wawe na vitambulisho tu... Mwalimu ni mtu muhimu sana ...
Utasaidia gharama za mafuta,vipuri,posho na MABAO YA TRAFIC?
 
Angesema kila katikati ya mwezi walimu wapewe fedha ya nauli ata 50,000 ningemwelewa,wengine wanaenda sehemu hakuna daladala wanatumia bodaboda.
Polisi pia wasikamate walimu hovyo wanapokua na viusafiri vyao na Tra wasiwaghasi kwani kodi wanayolipa inatosha.
Tabia za makondakta nichafu Sasa tusiwagonganishe na walimu kisa mia tatu tatu,walimu wasijedhalilishwa kuwa hawana hâta miatatu
 
Hata mahospitalini tuliambiwa wazee, watoto na mama mjamzito watatibiwa bure. Lakini leo hii nenda hospitali uone kama watajwa wanatibiwa bure. Utakacho ambulia cha bure ni ishauri wa daktari tu.
 
Angekuwa na akili angewaongezea hela ya nauli huko huko kwenye mishahara yao.
Mzee wa media
 
Back
Top Bottom