Makonda na Nchimbi wapendekeza wakuu wa wilaya, mikoa, RAS na DED; utenguzi, uhamisho na utenguzi kufanyika hivi karibuni

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Kila kiongozi anayeingia ofisini kwenye chama jambo la kwanza ni kupendekeza kutengua na kuteua. Tayari wawili hawa wamewasilisha majina ya watu wanaotamani wapewe nafasi waonje keki ya Taifa.

Kufuatia utamaduni huu wa kila mtu kumpa shavu rafiki yake, nawajulisha wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na makatibu tawala kuanza kuwahamisha wapangaji kwenye nyumba zao walizopangisha na kuzipiga rangi wakijiandaa kuondolewa kwenye ofisi na kurejea uraiani

Niwakumbushe pia kuanza kufuatilia bei ya mafuta kwani mashangingi siyo mali yao tena wanakabidhiwa wengine. Waanze pia kujifunza kuishi bila vibarua na walinzi kwani soon hakuna mhudumu wala mlinzi atakayeambatana naye. Kuhusu kuwatumikisha madereva wakumbuke wanatakiwa kuanza kujiendesha wenyewe kwani hawana pesa yakuajiri dereva.

Waanze pia kujinunulia chakula na kupika kwani ni wazi kwamba chakula cha hoteli ni gharama na kinakifu.

Tukumbuke kuwa hautotumbuliwa kwa sababu umekosea bali unatumbuliwa kwa sababu wewe umeshiba na tupo tunagawana mkate. Wasilimieni watu vyeo vinapita
 
1706995871574.jpeg
 
Back
Top Bottom