Kassim Majaliwa: Marufuku Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa na mabaunsa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Wakuu wa mikoa na wilaya wameelezwa mambo kadhaa ambayo hawatakiwi kuyafanya katika utekelezaji wa majukumu yao, ikiwemo kutumia walinzi binafsi ‘mabaunsa’ na matumizi ya magari binafsi yanayowekwa nembo ya Serikali.

Vilevile, wametakiwa kuacha kutumia vibaya Sheria inayowapa mamlaka ya kumuweka mtu rumande kwa saa 48.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alieleza hayo jana, wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa Wakuu wa Mikoa na makatibu tawala wa mikoa yanayofanyika jijini hapa.

Majaliwa alionya kitendo cha kutumia amri ya kumuweka mtu ndani kwa saa 48, kwamba imekuwa ikitumika vibaya na viongozi hao.

“Amri hii inataka kumuweka mtu ndani kama kuwepo kwake nje kutaleta madhara, kama kudhuriwa au wananchi kuumizwa na uwapo wake nje. Lakini si kwamba mwananchi mmoja amebisha maelekezo yako au anahoji sana, unatumia sheria hiyo kumweka ndani,” alionya Majaliwa.

Kwa miaka ya karibuni, baadhi ya wakuu wa mikoa walikithiri kwa kutumia sheria, ambapo hata baadhi ya watumishi, watendaji na hata viongozi wa kisiasa waliingia katika mkumbo huo wa kulazwa ndani.

Hali hiyo ilisababisha malalamiko kutoka kwa wananchi, viongozi wa siasa na pia wanaharakati dhidi ya viongozi hao waliokuwa wanakwenda kinyume na misingi ya utawala bora.

Walinzi binafsi

Majaliwa pia aliwataka viongozi hao wa mikoa 26 ya Tanzania Bara kuacha tabia ya kuajiri walinzi binafsi au wasaidizi binafsi na kwamba kazi ya kuwapata walinzi au wasaidizi inafanywa na katibu tawala (RAS) wa mkoa husika.

“Kama unataka msaidizi muombe RAS. Unaweza ukamuambia akuletee majina hata matatu na wewe ukachagua mmoja, siyo mbaya lakini siyo kuchukua watu mitaani ambao hawana hata maadili ya utumishi,” alisema Majaliwa.

Kauli ya Majaliwa inakuja wakati ambapo baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakitembea na walinzi binafsi, maarufu ‘mabaunsa’.

Majaliwa alisema kuwa na wasaidizi binafsi nako kunachangia kuvuja kwa siri za Serikali kwa kuwa hawana maadili ya utumishi wa umma.

Miongoni mwa viongozi waliowahi kulalamikiwa kwa suala hilo ni aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya ambaye waliokuwa wanadaiwa kuwa walinzi wake ndio anaoshtakiwa pamoja nao katika mashtaka yake ya jinai.

Katika hatua nyingine, Majaliwa aliwataka viongozi hao kujua itifaki kwa kuheshimiana, ikiwamo wakuu wa wilaya kuwaheshimu wakuu wa mikoa wanapokwenda kwenye maeneo yao.

Alisema kuna baadhi ya wakuu wa wilaya wamekuwa hawawaheshimu wakuu wa mikoa wakijiona kwamba na wao ni wateule wa Rais.

Waziri Mkuu aliwataka vilevile waheshimu itifaki kwa kutambua kwenye maeneo yao ya kazi kuna viongozi wengine wa Serikali, wakiwamo mahakimu, majaji na viongozi wengine wa kisiasa ambao wanatakiwa waheshimu majukumu yao.

Pia, aliwataka viongozi hao wawaheshimu viongozi wastaafu, wakiwamo marais, mawaziri, wakuu wa mikoa na hata wakuu wa wilaya wanapotembelea kwenye maeneo yao ya kazi.

Magari binafsi

Majaliwa pia alizungumzia matumizi ya magari ya Serikali kwa viongozi hao, hasa wakuu wa mikoa akisema hawatakiwi kutumia magari binafsi pale magari yao yanapoharibika.

“Haiwezekani gari lako limeharibika unatoa namba kwenye gari la Serikali unaweka kwenye gari lako binafsi tena (Toyota) Mark II au unaweka kwenye gari kubwa la kifahari,” alisema.

Majaliwa alisema viongozi wana utaratibu wao wa magari na kwamba kama gari la RC limeharibika anaweza kuchukua gari la RAS ili akatekeleze majukumu yake ya kikazi.

Suala la matumizi ya magari binafsi liliwahi kuzua gumzo mitandaoni wakati Paul Makonda akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, alipoonekana akitumia magari kadhaa yanayoaminika hayakuwa ya Serikali, kama Ranger Rover, Lexus na BMW yakiwa na nembo ya RC na Bendera ya Taifa.

Majaliwa aliwaambia viongozi hao kuwa waadilifu kwa kuanzia mavazi, namna ya kula kwenye mkusanyiko wa watu na wawe na uhusiano wenye maadili na watumishi wa chini yao.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa alizungumzia utaratibu wa ma-RC kupeperusha bendera ya Taifa kwenye maeneo yao ya mamlaka kwamba panapokuwa na viongozi wa kitaifa hawaruhusiwi kufanya hivyo.

Alisema kwa mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma, kwa kuwa mikoa hiyo ina viongozi wa kitaifa muda mwingi, wao hawatakiwi kupeperusha bendera kabisa.

Katika hatua nyingine, Mchengerwa alisema hadi jana jumla ya watumishi 128,700 walikuwa wamepanda madaraja, ikiwamo kulipwa fedha zao.

Alisema pia watumishi 29,629 waliokuwa wanadai malimbikizo yao ya Sh53.9 bilioni yamelipwa na wengine 18,170 waliokuwa wakidai Sh32.2 bilioni uchambuzi wa madai yao unaendelea.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu alisema ni muhimu kwa viongozi hao kutumia mapato ya ndani yanayotokana na halmashauri kuwekeza katika miradi ya maendeleo.

Chanzo: Mwananchi
 
Kweli kila zama na zama zake jiwe angekuepo angewasifu wakina sabaya na Makonda, ila jiwe hayupo ni mwendo wa kuwaponda. Wanasiasa ni kama bendera.
 
Vilevile, wametakiwa kuacha kutumia vibaya sheria inayowapa mamlaka ya kumuweka mtu rumande kwa saa 48.
Wangepunguza kutoka masaa 48 hadi masaa 6 ili kuonea huruma Wananchi wasiopenda kupelekeshwa na Watawala ambao hawajachaguliwa Kidemokrasia.

Na baadae kuabolish Vyeo vya Ukuu wa Mikoa au Wilaya au kuvifanya vya kuchaguliwa na Wananchi wa eneo husika.
 
KISIWAGA
Hivi, kwa nini mnaruhusu shetani atawale maisha yenu? Matusi haya kwa binadamu anayhangaika na ustawi wenu japo katika dunia hii ya sasa iliyojaa mashaka, yanatokana na roho gani hii? Mungu Yupo na anawaona. Acheni tabia hizi mbaya vijana. Huwezi kutukana mtu ambaye hujawahi kukutana naye hata kumtafuta umwambie yeye ni tatizo gani kwako.

Acheni tabia hizi mbovu, tena nasema acheni. Mtakuja kujuta sana kama hamtanisikiliza. Shetani hatawasaidia siku ya kujiliwa kwenu.
 
Leo ndiyo unasema haya!!!! Watu walilalamika sana awamu ya tano mlikaa kimya!!! Mliweka pamba masikioni na mlivaa miwani myeusi sana mlikuwa hata kuona hamuoni! Hii inaonyesha tuwe makini sana tunapochagua viongozi wa kutuongoza. Leo hii tusingepata raisi ambaye ana ubinadamu hilo katazo lisingetoka kabisa!
 
Wakuu wa mikoa na wilaya wameelezwa mambo kadhaa ambayo hawatakiwi kuyafanya katika utekelezaji wa majukumu yao, ikiwemo kutumia walinzi binafsi ‘mabaunsa’ na matumizi ya magari binafsi yanayowekwa nembo ya Serikali.

Vilevile, wametakiwa kuacha kutumia vibaya sheria inayowapa mamlaka ya kumuweka mtu rumande kwa saa 48.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alieleza hayo jana, wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa yanayofanyika jijini hapa.

Majaliwa alionya kitendo cha kutumia amri ya kumuweka mtu ndani kwa saa 48, kwamba imekuwa ikitumika vibaya na viongozi hao.

“Amri hii inataka kumuweka mtu ndani kama kuwepo kwake nje kutaleta madhara, kama kudhuriwa au wananchi kuumizwa na uwapo wake nje. Lakini si kwamba mwananchi mmoja amebisha maelekezo yako au anahoji sana, unatumia sheria hiyo kumweka ndani,” alionya Majaliwa.

Kwa miaka ya karibuni, baadhi ya wakuu wa mikoa walikithiri kwa kutumia sheria, ambapo hata baadhi ya watumishi, watendaji na hata viongozi wa kisiasa waliingia katika mkumbo huo wa kulazwa ndani.

Hali hiyo ilisababisha malalamiko kutoka kwa wananchi, viongozi wa siasa na pia wanaharakati dhidi ya viongozi hao waliokuwa wanakwenda kinyume na misingi ya utawala bora.

Walinzi binafsi

Majaliwa pia aliwataka viongozi hao wa mikoa 26 ya Tanzania Bara kuacha tabia ya kuajiri walinzi binafsi au wasaidizi binafsi na kwamba kazi ya kuwapata walinzi au wasaidizi inafanywa na katibu tawala (RAS) wa mkoa husika.

“Kama unataka msaidizi muombe RAS. Unaweza ukamuambia akuletee majina hata matatu na wewe ukachagua mmoja, siyo mbaya lakini siyo kuchukua watu mitaani ambao hawana hata maadili ya utumishi,” alisema Majaliwa.

Kauli ya Majaliwa inakuja wakati ambapo baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakitembea na walinzi binafsi, maarufu ‘mabaunsa’.

Majaliwa alisema kuwa na wasaidizi binafsi nako kunachangia kuvuja kwa siri za Serikali kwa kuwa hawana maadili ya utumishi wa umma.

Miongoni mwa viongozi waliowahi kulalamikiwa kwa suala hilo ni aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya ambaye waliokuwa wanadaiwa kuwa walinzi wake ndio anaoshtakiwa pamoja nao katika mashtaka yake ya jinai.

Katika hatua nyingine, Majaliwa aliwataka viongozi hao kujua itifaki kwa kuheshimiana, ikiwamo wakuu wa wilaya kuwaheshimu wakuu wa mikoa wanapokwenda kwenye maeneo yao.

Alisema kuna baadhi ya wakuu wa wilaya wamekuwa hawawaheshimu wakuu wa mikoa wakijiona kwamba na wao ni wateule wa Rais.

Waziri Mkuu aliwataka vilevile waheshimu itifaki kwa kutambua kwenye maeneo yao ya kazi kuna viongozi wengine wa Serikali, wakiwamo mahakimu, majaji na viongozi wengine wa kisiasa ambao wanatakiwa waheshimu majukumu yao.

Pia, aliwataka viongozi hao wawaheshimu viongozi wastaafu, wakiwamo marais, mawaziri, wakuu wa mikoa na hata wakuu wa wilaya wanapotembelea kwenye maeneo yao ya kazi.

Magari binafsi

Majaliwa pia alizungumzia matumizi ya magari ya Serikali kwa viongozi hao, hasa wakuu wa mikoa akisema hawatakiwi kutumia magari binafsi pale magari yao yanapoharibika.

“Haiwezekani gari lako limeharibika unatoa namba kwenye gari la Serikali unaweka kwenye gari lako binafsi tena (Toyota) Mark II au unaweka kwenye gari kubwa la kifahari,” alisema.

Majaliwa alisema viongozi wana utaratibu wao wa magari na kwamba kama gari la RC limeharibika anaweza kuchukua gari la RAS ili akatekeleze majukumu yake ya kikazi.

Suala la matumizi ya magari binafsi liliwahi kuzua gumzo mitandaoni wakati Paul Makonda akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, alipoonekana akitumia magari kadhaa yanayoaminika hayakuwa ya Serikali, kama Ranger Rover, Lexus na BMW yakiwa na nembo ya RC na Bendera ya Taifa.

Majaliwa aliwaambia viongozi hao kuwa waadilifu kwa kuanzia mavazi, namna ya kula kwenye mkusanyiko wa watu na wawe na uhusiano wenye maadili na watumishi wa chini yao.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa alizungumzia utaratibu wa ma-RC kupeperusha bendera ya Taifa kwenye maeneo yao ya mamlaka kwamba panapokuwa na viongozi wa kitaifa hawaruhusiwi kufanya hivyo.

Alisema kwa mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma, kwa kuwa mikoa hiyo ina viongozi wa kitaifa muda mwingi, wao hawatakiwi kupeperusha bendera kabisa.

Katika hatua nyingine, Mchengerwa alisema hadi jana jumla ya watumishi 128,700 walikuwa wamepanda madaraja, ikiwamo kulipwa fedha zao.

Alisema pia watumishi 29,629 waliokuwa wanadai malimbikizo yao ya Sh53.9 bilioni yamelipwa na wengine 18,170 waliokuwa wakidai Sh32.2 bilioni uchambuzi wa madai yao unaendelea.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu alisema ni muhimu kwa viongozi hao kutumia mapato ya ndani yanayotokana na halmashauri kuwekeza katika miradi ya maendeleo.

mwananchi

Kwani katiba inasema je?
 
Ndio maana jamaa kauliza juu walikua wapi hawa makoko!..wote Sawa Tu ..
 
Nadhani yule mfanyabiashara wa Hai alitoa ya moyoni mbele ya WM Majaliwa. Since then nilijifunza viongozi nao walikua wanamuogopa jiwe. Haiwezekani mambo yote yaanze kurekebishwa na kusemwa wakati huu😁
 
Back
Top Bottom