Makonda apiga marufuku maandamano Dar

Makonda apiga marufuku maandamano Dar

Mbona ulishajibiwa ndugu?. Katiba iko wazi kwa hicho nilichosema usome na ni jambo linahusu kinga aliyo nayo. Ni mimi nimeshindwa jibu swali au wewe umeshindwa elewa?.

Pia mimi nimejibu na nikatoa way forward. Wewe unazungumziaje hilo?. Maana umekazania yuko juu ya sheria. Lakini hujui kuwa rais wa nchi anaongozwa na katiba?, je hujui kuwa kiongozi wa nchi ana immunity?. Je ni kweli katiba unaisoma au tunaandika tu kwa kile tulicho sikia bila kusoma katiba yenyewe?.

Ndiyo maana inatuwia ugumu sana. Mfano katiba ya sasa wengi hawaijui, hiyo mpya tuitakayo tunaitoa kwenye misingi ipi?.

Vyema tusome. Lakini tusijifunge ufahamu wetu kwa kuangalia leo. Tuitazame kesho pia. Leo tunaongozwa na viongozi ambao kwa namna moja ama nyingine wanafuata katiba.

Je kesho tunajua atakaye tuongoza?, tunajua atatumiaje madaraka aliyo pewa na katiba ya sasa?. Katika hili usiangalie chama.

Ni jamii gani Dunia hii watu husoma Katiba ukiachia wale ambao wanautumia kwenye shughuli zao? Sijawahi kukutana na mtu yoyote yule Dunia hii akisoma Katiba!
 
Sijadili kuhusu kama tunahutaji katiba mpya au la bali najaribu kuelezea wale wanaosema raisi wa JMTZ amevunja sheria za JMTZ wkt hawawezi kumshitaki sasa mtu atavunjaje sheria kama huwezi na hakuna sheria ya kumshitaki kwa hilo kosa?
Labda ambalo umeshindwa wao kuwaelewa ni hiyo haki ya kujikusanya, haki ya kutoa mawazo katika sehemu za wazi. Hiyo ni kitu inaruhusiwa na ni haki ya watu kufanya hivyo ili mradi usivunje sheria za nchi na uzijulishe mamlaka husika kwa ajili ya usalama. Hiyo ni haki kikatiba.

Sasa mtu akivunja haki hiyo kwa mfano kwa mazingira ya kuwa kaivunja kweli, je haitoi uhalali kuwa kweli kavunja?. Swala la kuvunja ni moja na swala la kushitakiwa ni lingine. Na kwa hapo huwezi kumshtaki kiongozi wa nchi.

Sasa kama hali ndivyo ilivyo, wewe kama great thinker unatoa njia gani mbadala/suluhisho?. Je mambo haya yasipo wekwa sawa sasa huoni yatakuja kuwa shida kwa kizazi tulicho nacho sasa?. Kumbuka siasa za 1995 sio hizi za 2016. Kumbuka jamii ya sasa sio jamii ile ile ya kipindi cha Mwalimu na mzee Mwinyi.

Tusiishie kutoa tu majibu mepesi. Tumalizie pia na kutoa njia mbadala ya kufikia malengo kwa amani. Hatupimi watu kwa uwezo wa kuyaona matatizo pekee, bali pia uwezo wa kuja na majibu kwa matatizo tuliyo nayo.
 
Wewe ni Mwanasheria gani usiweelewa? Raisi amesema hajakataza Mikutano ya Kisiasa bali ni kwa wale waliochaguliwa tu, wale ambao hawajachaguliwa hawana cha kutueleza tena kwani walijaribu kutuomba kura tukawasikiliza, kuwapima na kutoa uamuzi wetu ambapo tuliwakataa sasa Mikutano ya nini? Kwa nini wasisubiri kipenga kitakapopulizwa 2020 ndiyo waanze tena?

Kwa nini wale tuliowachagua wasipewe nafasi ya kufanya kazi zao? Ni kwa nini Mbunge wa Hai aende Kahama na siyo Hai? Anafwata nini Kahama? Kwa nini Mbunge wa Singida aende Mwanza inamuhusu nini kwa nini asiende Jimboni kwake? Logic iko wapi? Au Kwenye Sheria huwa hamsomi Mathematics hata utambulisho tu wa kuhusu logic?
Jilin la Dar lipo chini ya UKAWA, una swali?
 
Labda ambalo umeshindwa wao kuwaelewa ni hiyo haki ya kujikusanya, haki ya kutoa mawazo katika sehemu za wazi. Hiyo ni kitu inaruhusiwa na ni haki ya watu kufanya hivyo ili mradi usivunje sheria za nchi na uzijulishe mamlaka husika kwa ajili ya usalama. Hiyo ni haki kikatiba.

Sasa mtu akivunja haki hiyo kwa mfano kwa mazingira ya kuwa kaivunja kweli, je haitoi uhalali kuwa kweli kavunja?. Swala la kuvunja ni moja na swala la kushitakiwa ni lingine. Na kwa hapo huwezi kumshtaki kiongozi wa nchi.

Sasa kama hali ndivyo ilivyo, wewe kama great thinker unatoa njia gani mbadala/suluhisho?. Je mambo haya yasipo wekwa sawa sasa huoni yatakuja kuwa shida kwa kizazi tulicho nacho sasa?. Kumbuka siasa za 1995 sio hizi za 2016. Kumbuka jamii ya sasa sio jamii ile ile ya kipindi cha Mwalimu na mzee Mwinyi.

Tusiishie kutoa tu majibu mepesi. Tumalizie pia na kutoa njia mbadala ya kufikia malengo kwa amani. Hatupimi watu kwa uwezo wa kuyaona matatizo pekee, bali pia uwezo wa kuja na majibu kwa matatizo tuliyo nayo.

Mimi siyo Mwanasheria lkn logic ya kawaida inaniambia kwamba kama hakuna kifungu cha Sheria cha kunishitaki ina maana sijaivunja hiyo Sheria sasa nashindwa kuelewa logic yako iko wapi kama mnasema raisi kavunja sheria lkn hakuna mahali pa kumshitaki sasa anawezaje kuvunja sheria ambayo haipo?
 
Ni jamii gani Dunia hii watu husoma Katiba ukiachia wale ambao wanautumia kwenye shughuli zao? Sijawahi kukutana na mtu yoyote yule Dunia hii akisoma Katiba!
Sema mimi Barbarosa sisomi katiba. Usiseme jamii nzima duniani hujawahi kutana na watu wanao soma katiba zaidi ya wale wanao itumia.

Sisi tuna hulka tofauti kama binadamu, sasa si vyema kujumuisha watu wote kama wewe husomi. Unaamini kuwa information is power?. Unaamini pia kuna watu wanaamini katika kujiongezea maarifa?. Sasa utabishaje mambo ya siasa kama hivi wakati hata hiyo katiba inayo ongoza nchi huijui?.

Je unafahamu elimu ya uraia?. Kwani hayo ya kujua ngazi za utendaji sijui na mambo mengine uliyo soma shule ya msingi na sekondari unadhani mengine yanatoka wapi?.

Leo hujui kuwa hao wote wanaotupngoza ni kwa mujibu wa katiba?. Sasa unaposoma hujawahi ona mtu anasoma katiba mimi nashangaa. Hujui hayo yote yako kwenye katiba?.

Ukitaka kuongeza maarifa yako vyema muhimu ujiongezee tabia ya kusoma. Si lazima ujue katiba nzima maana katiba ni sheria lakini walau katika kile unacho jadili vyema ujue misingi yake imewekwa/inatoka wapi.
 
Huyu naye anakurupuka kama kawaida yake alimwambia ana uwezo wa kuzuia maandamano ni nani?
Jaribu uone sasa unadhani mchezo weka mguu mbele halafu subiri moto wake.
 
Mimi siyo Mwanasheria lkn logic ya kawaida inaniambia kwamba kama hakuna kifungu cha Sheria cha kunishitaki ina maana sijaivunja hiyo Sheria sasa nashindwa kuelewa logic yako iko wapi kama mnasema raisi kavunja sheria lkn hakuna mahali pa kumshitaki sasa anawezaje kuvunja sheria ambayo haipo?
Mimi mwenyewe sio mwanasheria mkuu. Ila ni mtu napenda jiongezea knowledge walau kwa kusoma na kuelewa mambo. So nawe pia waweza jenga tabia hiyo. Sio katika siasa tu ila katika mambo mengine yanayo weza kunufaisha kimaisha.
 
Yumurudi kwa wale wale 'kalal balozi muafaka.fikra za mwenyeki zidumu hata akisema leo nileteeni wake zenu .basi watasema ndio tunaunga mkono .ivi yule mzee aliesigana katiba pole jangwani baadae akafungwa kwa nini chadema wasitafute akafungue kesi ya madai .maana kwa sasa kama angesigana katiba naona ata asingekamatwa maana sasa inchi inaongozwa kwa matamko na utashi tu
Asee mwendokasi!!!
 
Hivi watu wakiamua kuandamana kila kata hapa Dar ana uwezo wa kuwazuia? Cha msingi muda bado wa kuongea kati ya Watawala, CCM, vyama Vvya UPinzani na Mlezi wa vyama jaji Mtungi ambaye kaambiwa aivue kofia ya ukada wa CCM kwanza. Huu muda si wa kutunishiana misuli busara zitumike na watu wakubali kushaurika. Hii TAnzania si Mali ya mtu au watu wachache.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku maandamano ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Makonda amesema kuwa kufuatia kauli ya Rais,yeye anaitekeleza.

Makonda amesema kuwa kauli ya Rais ni moja ya mambo aliyoapa kuyatii na kuyatenda. Amesema kuwa hataruhusu wala kukubali kufanyika maandamano mkoani mwake.
Makonda ameanza...

Maoni yangu: Kama Mwanasheria sifurahishwi na kuwekwa kando kwa Sheria zinazoruhusu na kuratibu mikutano ya kisiasa na maandamano. Serikali naiomba ifanye tathmini njema juu ya sakata hili.Where are we heading?

Chanzo: Channel Ten

Hivi kwa nini ninyi wanasheria hamfungui kesi kudhibiti hali hii?

Uanasheria wenu una faida gani sasa?
 
Wanasheria wetu wanahitaji elimu elimu elimu,,, usomi wao hauna faida kwa mtanzania
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku maandamano ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Makonda amesema kuwa kufuatia kauli ya Rais,yeye anaitekeleza.

Makonda amesema kuwa kauli ya Rais ni moja ya mambo aliyoapa kuyatii na kuyatenda. Amesema kuwa hataruhusu wala kukubali kufanyika maandamano mkoani mwake.
Makonda ameanza...

Maoni yangu: Kama Mwanasheria sifurahishwi na kuwekwa kando kwa Sheria zinazoruhusu na kuratibu mikutano ya kisiasa na maandamano. Serikali naiomba ifanye tathmini njema juu ya sakata hili.Where are we heading?

Chanzo: Channel Ten

🤣🤣
 
Back
Top Bottom