Makonda aondolewe kwa udhalilishaji wa wanawake. Amewadhalilisha wanawake na rais wetu pia

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
14,036
18,880
Kitendo cha mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda kumdhalilisha afisa wa serikali mwanamke huko Longido mkoani Arusha hakikubaliki.

Makonda akimhoji mtumishi huyo alisikika kumwambia mbele ya hadhara kuwa asiongee kama vile anaposwa na kwamba yeye (Makonda) ana mke mzuri nyumbani.

Kitendo hicho kilionekana kumuudhi mama huyo na kuibua minong’ono katika mkutano huo.

Tayari shirika la kutetea haki za binadamu wamelaani matamshi ya Makonda.

Itakuwa ajabu kama rais Samia hatamchukulia hatua mkuu wa mkoa Paul Makonda kwa Kitendo hiki kinachoonesha udhalilishaji dhidi ya wanawake.
 
sawa ikiwa atachukuliwa hatua, ila na huyo ofisa mwanamke ajue namna ya kujibu anapohojiwa na mabosi wake asijibu kwa kiburi atakutana na maneno ya shombo kama yalivyomkuta. Makonda naye afahamu namna ya kuchagua maneno anapomhoji ofisa anapokuwa ameghafilika na kuudhiwa
 
Kitendo cha mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda kumdhalilisha afisa wa serikali mwanamke huko Longido mkoani Arusha hakikubaliki.

Makonda akimhoji mtumishi huyo alisikika kumwambia mbele ya hadhara kuwa asiongee kama vile anaposwa na kwamba yeye (Makonda) ana mke mzuri nyumbani.

Kitendo hicho kilionekana kumuudhi mama huyo na kuibua minong’ono katika mkutano huo.

Tayari shirika la kutetea haki za binadamu wamelaani matamshi ya Makonda.

Itakuwa ajabu kama rais Samia hatamchukulia hatua mkuu wa mkoa Paul Makonda kwa Kitendo hiki kinachoonesha udhalilishaji dhidi ya wanawake.
Basi dunia inaenda speed. Mwanamke kuposwa ni udhalilishaji, au kumwambia nina mke nyumbani..

Mmmh, hizi ni kelele za ujinga, watu wakihojiwa wamedhalilishwa.
 
Ifike mahala tuache kupitishia chuki zetu kwenye mgongo wa haki za binadam au haki za wanawake, wanawqke nao akijua yeye ni mtumishi wa uma ahakikishe anafanya kazi zake kwa weledi bila kusubiri huruma za wapuuzi kama wewe mtoa mada.
Nyie masalia ya Magufuli hamna nafasi ya kufanya ujinga wenu nchi hii kipindi chenu kimepita
 
M
Ifike mahala tuache kupitishia chuki zetu kwenye mgongo wa haki za binadam au haki za wanawake, wanawqke nao akijua yeye ni mtumishi wa uma ahakikishe anafanya kazi zake kwa weledi bila kusubiri huruma za wapuuzi kama wewe mtoa mada.
Wewe Ndo hukamuelewa mtoa mada,shida ilikuwa wapi Kama angemwacha huyo mtumishi akamaliza kueleza kuhusu ujenzi na pia Kama Kuna matatizo hachukuliwe hatua za kisheria na kuwajibishwa kwa kanuni za utumishi,kwa Nini amwongelee vile mbele ya kadamunasi,fikilia Kama angekuwa mama au Dada yako ungejisikiaje?
 
Kitendo cha mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda kumdhalilisha afisa wa serikali mwanamke huko Longido mkoani Arusha hakikubaliki.

Makonda akimhoji mtumishi huyo alisikika kumwambia mbele ya hadhara kuwa asiongee kama vile anaposwa na kwamba yeye (Makonda) ana mke mzuri nyumbani.

Kitendo hicho kilionekana kumuudhi mama huyo na kuibua minong’ono katika mkutano huo.

Tayari shirika la kutetea haki za binadamu wamelaani matamshi ya Makonda.

Itakuwa ajabu kama rais Samia hatamchukulia hatua mkuu wa mkoa Paul Makonda kwa Kitendo hiki kinachoonesha udhalilishaji dhidi ya wanawake.

Pamoja na kwamba siungi mkono ila
kwa mtazamo wangu kosa alilofanya linastahili tu kukumbushwa kwa taratibu za ndani za kimaadili na wala sio adhabu unayoifikiria. Tunapokuwa na Viongozi vijana, mambo kama hayo hayawezi kuepukika japo hatuyaungi mkono.......
 
Makonda ni yuleyule tu,kwani ni lini aliwahi kuwa na staha? Hata aliyekuwa anamuharibia JPM ni yeye..........japo nayeye alikuwa na weakness zake ila aliyekuwa anampaka matope JPM ni pamoja DAB
 
Yule mwanamke hakujui nafasi ya Mkuu wa mkoa.

Yule mwanamke ana miaka mitatu kazi amekaimishwa idara kwa mwaka mmoja na nusu😳
Ni wale wanaofanana na DC nzega
 
M

Wewe Ndo hukamuelewa mtoa mada,shida ilikuwa wapi Kama angemwacha huyo mtumishi akamaliza kueleza kuhusu ujenzi na pia Kama Kuna matatizo hachukuliwe hatua za kisheria na kuwajibishwa kwa kanuni za utumishi,kwa Nini amwongelee vile mbele ya kadamunasi,fikilia Kama angekuwa mama au Dada yako ungejisikiaje?
Unakumbuka chanzo cha Maghufuri kutaka Kumvua Nyota zote Afisa wa Magereza kule Mwanza...!?

Ni sababu zile zile zilizomfanya Makonda aseme aliyosema....!

Kuna namna yule Dada alikua anaongea utadhani hajui kuwa anaongea na Boss wake, anajibu kishkaji sana.
 
Tupunguze chuki jamani ,,

Hiv kweli Kama kila kosa mtu anapaswa kuondolewa kazin Nani angebak ofisini?
 
Back
Top Bottom