Makonda anageuka super sub inayotoa matokeo

Makonda anageuka super sub inayotoa matokeo

Na huu ujinga ndio mnajiaminisha Sukuma gang, matokeo yake kwenye hizi ziara za hadaa za muhalifu Makonda inatumika nguvu kubwa ya Dola kukusanya watu kuanzia watumishi wa umma nk. Raslimali za umma zinatumika kwa nguvu Ili kufanikisha ziara ya hadaa za chama. Na mlivyo wajinga mnaamini watu wanahadaika na hizo nyomi za kutengenezwa.
Kwa Makonda nakataa kabisa hakuna anayelazimishwa ila kwa Dkt Samia kila alipofanya ziara nakiri kabisa watendaji wa eneo/mkoa husika basi hukusanya watumishi wote tena wanawafungia bila hata maji na mwisho wa siku watu wanakasirika sana. Makonda ni anakubalika!
 
Sikuambii hivyo kwa kubahatisha, Bali nakuambia na ushahidi juu. Twende parahisi kabisa, hizo ni ziara za chama, magari ya serekali ni ya Nini? Tena 95% ni magari ya serekali na sio ya chama. Hapo unapata picha gani?
 
Magari hayana shida wale ni viongozi walielekezwa kuhakikisha mwenezi anapokuwa eneo husika basi viongozi wa CCM wawepo. Ninachosema ni ile mfano Dkt Samia akija Uhuru hapa Dar basi walimu wote wanakaripiwa lazima kwenda mkutanoni, Makonda hana hiyo
 
Hii ya kwamba fulani anapendwa sana ila mitandaoni ndio hapendwi ilikuwa sana wakati wa Magufuli. Ikasemekana Magufuli anapendwa sana, lakini tuliishia kuona uchaguzi wa kishenzi sana Ili yapatikane matokeo yatakayoendana na alichoaminishwa au alichoamini Magufuli. Kama kweli Makonda anapendwa, tume ya uchaguzi iwe huru kisha matokeo halali yatangazwe ukweli ufahamike. Sio mlete picha ya sijui mtaani, halafu Bado mnalazimisha tume iwe chini ya mwenyekiti wa ccm, na uchagu mwingine wa wazi Ili kutoa matokeo yasiyoendana na uhalisia.
Unaandika pumba ukiwa unajiamini kabsa.

MImi nazungumzia suala la ziara za Makonda na namna wanachi wanavyo pokea hyo ziara wewe unaniletea mambo ya Magufuli.

Jifunze kujadili hoja sio kupenda kujadili watu.Hivi wewe kwaakili zako ni kina Mbowe tu ni viumbe walio sahihi kuliko wengine hapa Tanzania.

Siasa zisikupofushe na unaweza kuwa mgeni wa siasa hapa duniani.Sidhani kama ulitegemea Mdee afanye alichofanya au Nassari afanye alichokifanya.

Jifunze kukubali jema la mtu hata kama haumpendi.
 
Magari hayana shida wale ni viongozi walielekezwa kuhakikisha mwenezi anapokuwa eneo husika basi viongozi wa CCM wawepo. Ninachosema ni ile mfano Dkt Samia akija Uhuru hapa Dar basi walimu wote wanakaripiwa lazima kwenda mkutanoni, Makonda hana hiyo

Hicho Cha kupeleka watumishi wa umma ni mchezo sugu wa ccm kwa sasa, na hautakaa uishe labda watoke madarakani. Magari ya serekali kwenye ziara za chama isiwe shida vipi? Ccm inajinasibu ni chama kubwa, na kina raslimali nyingi, Sasa inatumiaje magari ya umma kwenye ziara za chama? Kama inaweza kutumia magari ya serekali, na mafuta ya serekali, hao watumishi ni Nini?
 
Naona tayari wanambipu 🙌

View attachment 2897558
Ila hapo Makonda nimemwelewa sana

Ila huo msemo wa kuewekewa Sumu chumbani kwake amaanishe uwe wa kweli isiwe promo na ikiwezekana siku awaambie kabisa Ile Sumu mliyoniwekea Jana kule chumbani nimeilamba kuthibitisha km kweli ni Sumu au la na Mungu nilishampigia Simu nimeongea nae kashasema haniondoi leo wala kesho

Na huo msemo wa hapa ni wewe tu amaanishe isiwe km ngonjera au mpiga zumari tuone kweli hao washenzi washenzi wanaolipwa malundo ya mishahara ili wawafanyie kazi wananchi alafu wanaishia kuwataabisha wananchi na kuwadhulumu haki zao wanachukuliwa hatua stahiki sio kuambiwa maneno matupu tu wachukuliwe hatua haswa hakuna kucheka nao
 
So my question is? Kwann watu wanakusanyika anapokuwa Makonda?

Maana yake,anachokifanya Makonda wangekuwa wameshafanya ma DC, RC, wakurugenzi, mawaziri, manaibu waziri, jero nyingi zingekuwa zimeshasikilizwa!

Makonda ni wakwanza kufanya hivyo? Hapana! Si wa kwanza? Kwanini ghafla watumishi waliacha kusikiliza kero za watanzania Kwa kuingia field je walikatazwa? Noo big nooo

Tayari yake ni nini? Kiwango cha uwajibikaji,utu na kubeba matatizo yetu kama ya kwao ni hakuna kabisa!!

Atapendwa? Big Yes and big No! Justification on this? Atapendwa na matabaka mawili, tabaka la chini na tabaka la kati, lile tabaka analoligusa hawaezi kupenda anachokifanya na wapo tayari kukwamisha jitihada hizi Kwa gharama ya mauti na magonjwa!

Mwisho, Watanzania hawana haja na ofisi kama hazishughuliki na matatizo yao, anayeweza kusimama akashughulika na kero zao,hapohapo ndipo ofisi ilipo.

Kiu ya watanzania ni nini? Kupitia ziara hizo za Makonda? Mosi watanzania wanakosa haki zao za msingi pili Watanzania wanapenda sana viongozi kuingia field kutatua matatizo yetu tatu ambayo ni ya kwanza, Watanzania wanaweza kuonekana wamenyamaza kumbe mioyo yao inabubujikwa na machozi kama wakidharaulika.

Paul C. Makonda anageuka super sub inayotoa matokeo, huu mfupa sio mlaini ndio maana katika kipindi cha miaka 3, wenezi 3 wametafitwa katika nyakati tofauti tofauti.

Mungu anatukuzwa sana kupitia Paul Makonda, unakata kiu za Watanzania.

With thanks. Veronica France, fb on 5th feb 2024. Copy
ALipokuwa mkuu wa mkoa wa Dsm alimaliza matatizo ya Dsm? Yule anatafuta cheap popularity atamaliza ziara matatizo yako palepale
 
Hao wanao kusanyika kumsikiliza huyo Daudi ni mazwazwa tu alioharibiwa akili na CCM.

Hana jipya ila anaendeleza maigizo ya wala nchi
Hao unaowaita mazwazwa ndio wapo wengi nchini ndio wapija kura wenyewe sasa mbona mnaposhindwa kwenye uchaguzi mnalalamika mmeonewa? Hivi ChawaWaMama hivi unawaelewa wenzako hawa
 
Makonda Hana Jipya Zaidi Yakuwahadaa Wananchi.
CCM haina Jipyq Lakuwafanyia Wananchi zaidi Yakutuma Mtu Wakuigiza Kama Makonda.
Kuna Siku Nimemsikia Makonda Akiwaambia Wananchi Rais Amesikia Kilio Cha MADEREVA wa Transit ,Hawana Uwezo Wakukata Passport Kubwa Kwahiyo Atawasaidia Kulipia Hizo Passport.
Hivi Kweli kilio Cha MADEREVA wa Transit Ni Kushindwa Kukata Passport??
Kama CCM hawana jipya pamoja na Makonda kwanini mikutano yao inajaza watu wengi na hotuba zake nyingi za Makonda zinatrend mno mitandaoni na inaibua mijadala?
 
Sawa sisi tulio wengi ni mazwazwa!!

Ninyi wachache wenye akili endeleeni kuandamana huku Ruzuku zinajenga mahekalu ya Mbowe!! Mna akili nyingi mnoo
Kwa mujibu wa Chadema wanasema CCM inasapotiwa na watu wenye elimu ndogo sasa najiuliza kama CCM inasapotiwa na watu wenye elimu ndogo ambao ndio wapo wengi nchini kwanini wanaposhindwa uchaguzi wanalalamika wanaibiwa kura? Hili swali imekuwa sijibiwi au ndugu yangu ChawaWaMama unamajibu sahihi yakuwasaidia
 
  • Thanks
Reactions: Tui

Kwanza hicho chama hakipo kilishakufa kimebaki kikundi cha magaidi. Na hao waliobaki kwenye hicho kikundi hawa akili.
 
Umeme ni technical kwa hiyoo suala liko jikoni linatatuliwaa. Halafu kumbuka hakuna nchi wala taifa lolote lililomalizachangamoto za wananchi.
Toka tumepata uhuru ni huduma gani ya kijamii ambayo kweli tutajisifu tumefanikiwa kwa 70%.
Maana watawala wetu maisha wanayoishi na kujihudumia ni 100% wamefanikiwa.
Sisi tuna matatizo sugu sio changamoto.
 
Hao unaowaita mazwazwa ndio wapo wengi nchini ndio wapija kura wenyewe sasa mbona mnaposhindwa kwenye uchaguzi mnalalamika mmeonewa? Hivi ChawaWaMama hivi unawaelewa wenzako hawa
Una uhakika hao mazwazwa huwa wanapiga kura ya ndiyo?

Mwenyekiti wa tume kateuliwa na mtu anayegombea urais unadhani mgombeaji huyo wa urais atashindwa kutangazwa na huyo mwenyekiti wa tume ili kulinda cheo chake?

Nchi yetu inaongozwa na wala rushwa tangu enzi ya Nyerere hadi leo viongozi huhonga ili watangazwe kuwa wameshinda uchaguzi.
 
Toka tumepata uhuru ni huduma gani ya kijamii ambayo kweli tutajisifu tumefanikiwa kwa 70%.
Maana watawala wetu maisha wanayoishi na kujihudumia ni 100% wamefanikiwa.
Sisi tuna matatizo sugu sio changamoto.
Huu mtandao unaotumia
 
Sawa sisi tulio wengi ni mazwazwa!!

Ninyi wachache wenye akili endeleeni kuandamana huku Ruzuku zinajenga mahekalu ya Mbowe!! Mna akili nyingi mnoo

..kiuhalisia kero anazotatua Makonda ni chache sana ukilinganisha na kero na changamoto lukuki walizonazo wananchi.

..ukumbuke kwa wastani mikutano ya Makonda ktk eneo / wilaya moja huwa haichukui zaidi ya masaa mawili. Sasa huo ni muda mchache sana kusikiliza kero za wilaya husika, na kuzipatia majibu ya uhakika.

..Kitu cha uhakika anachofanya Makonda ni kuwachota wananchi kiakili na kuwadanganya warudishe imani kwa chama na serikali. Makonda anatengeneza hamasa na matumaini kwa wananchi.

..Kama unavyoona wenye shida wanavyofurika kwenye nyumba za ibada kwa matumaini hewa, ndivyo wananchi wanavyofurika ktk mikutano ya Makonda na kukabidhi kesho yao kwake.

..Kwa hiyo ziara za Makonda sio za kubeza. Wapinzani wana kazi kubwa mbele yao ya kuwaelimisha wananchi wasihadaike na ulaghai wa Makonda. Shida na changamoto za wananchi bado ziko palepale ktk maeneo yote aliyopita Makonda.

cc Nguruvi3, Erythrocyte
 
Back
Top Bottom