Makonda anageuka super sub inayotoa matokeo

Makonda anageuka super sub inayotoa matokeo

..kiuhalisia kero anazotatua Makonda ni chache sana ukilinganisha na kero na changamoto lukuki walizonazo wananchi.

..ukumbuke Makonda kwa wastani mikutano ya Makonda ktk eneo / wilaya huwa haichukui zaidi ya masaa mawili. Sasa huo ni muda mchache sana kusikiliza kero za wilaya husika na kuzipatia majibu ya uhakika.

..Kitu cha uhakika anachofanya Makonda ni kuwachota wananchi kiakili na kuwadanganya warudishe imani kwa chama na serikali. Makonda anatengeneza hamasa na matumaini kwa wananchi.

..Kama unavyoona wenye shida wanavyofurika kwenye nyumba za ibada kwa matumaini hewa, ndivyo wananchi wanavyofurika ktk mikutano ya Makonda na kukabidhi kesho yao kwake.

..Kwa hiyo ziara za Makonda sio za kubeza. Wapinzani wana kazi kubwa mbele yao ya kuwaelimisha wananchi wasihadaike na ulaghai wa Makonda. Shida na changamoto za wananchi bado ziko palepale ktk maeneo yote aliyopita Makonda.




cc Nguruvi3, Erythrocyte
Wananchi wengi wanakuja kwenye mikutano ya Makonda kama sehemu ya kuburudika tu , wanamjua na wanayajua yote aliyotenda
 
Wananchi wengi wanakuja kwenye mikutano ya Makonda kama sehemu ya kuburudika tu , wanamjua na wanayajua yote aliyotenda

..msimdharau Makonda.

..Na msidharau watu wanaomkimbilia.

..kuna kazi kubwa ya kufanya ya kuwanasua wananchi toka ktk utando wa ulaghai wa Ccm.

..Chadema inatakiwa upite kulekule alikopita Makonda na kuweka wazi upotoshaji na ulaghai aliofanya.
 
Toka tumepata uhuru ni huduma gani ya kijamii ambayo kweli tutajisifu tumefanikiwa kwa 70%.
Maana watawala wetu maisha wanayoishi na kujihudumia ni 100% wamefanikiwa.
Sisi tuna matatizo sugu sio changamoto.
Hata mawasiliano haya unayoyaona na kuyatumia, huoniii
 
Sawa sisi tulio wengi ni mazwazwa!!

Ninyi wachache wenye akili endeleeni kuandamana huku Ruzuku zinajenga mahekalu ya Mbowe!! Mna akili nyingi mnoo
Sawa ruzuku zinajenga hekalu za mbowe, pesa za umma nazo zinajenga hekalu za mbowe? Ama zinafanyiwa nini?
 
Na huu ujinga ndio mnajiaminisha Sukuma gang, matokeo yake kwenye hizi ziara za hadaa za muhalifu Makonda inatumika nguvu kubwa ya Dola kukusanya watu kuanzia watumishi wa umma nk. Raslimali za umma zinatumika kwa nguvu Ili kufanikisha ziara ya hadaa za chama. Na mlivyo wajinga mnaamini watu wanahadaika na hizo nyomi za kutengenezwa.
Viongozi wote wa mkoa husika na watumishi wote wanalazimishwa kwenda kumpokea
 
Hii ya kwamba fulani anapendwa sana ila mitandaoni ndio hapendwi ilikuwa sana wakati wa Magufuli. Ikasemekana Magufuli anapendwa sana, lakini tuliishia kuona uchaguzi wa kishenzi sana Ili yapatikane matokeo yatakayoendana na alichoaminishwa au alichoamini Magufuli. Kama kweli Makonda anapendwa, tume ya uchaguzi iwe huru kisha matokeo halali yatangazwe ukweli ufahamike. Sio mlete picha ya sijui mtaani, halafu Bado mnalazimisha tume iwe chini ya mwenyekiti wa ccm, na uchagu mwingine wa wazi Ili kutoa matokeo yasiyoendana na uhalisia.
Hawezi zaidi ya saaa tupu
 
Hao wanao kusanyika kumsikiliza huyo Daudi ni mazwazwa tu alioharibiwa akili na CCM.

Hana jipya ila anaendeleza maigizo ya wala nchi
Hata hao mazwazwa hayaendi yenyewe. Yanapelekwa na mabasi. Wengine ndio wanapita sasa hivi Migoli kwenye fuso yakitokea Iringa mjini kwenye ziara ya makonda.
 
Sawa sisi tulio wengi ni mazwazwa!!

Ninyi wachache wenye akili endeleeni kuandamana huku Ruzuku zinajenga mahekalu ya Mbowe!! Mna akili nyingi mnoo
Nakuunga mkono na uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu nendeni kwa hao wenye akili wawape kura. Kwani nyinyi wenye akili ndio majority.
 
Nakuunga mkono na uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu nendeni kwa hao wenye akili wawape kura. Kwani nyinyi wenye akili ndio majority.
Kwani kura ndio zinazoamua mshindi hapa kwetu, ama maagizo toka juu?
 
Kwani kura ndio zinazoamua mshindi hapa kwetu, ama maagizo toka juu?
Hata kura za wabunge wenu ziliamuliwa kutoka juu?Au haki inatendeka mkishinda tu mkishindwa mmeibiwa?
 
Hata kura za wabunge wenu ziliamuliwa kutoka juu?Au haki inatendeka mkishinda tu mkishindwa mmeibiwa?

Umewahi kuona wapinzaniwanasema haki imetendeka? Wapinzani hushangaa wakitangazwa washindi. Na ushahidi wa chaguzi kuchezewa uko wazi peupe.
 
So my question is? Kwann watu wanakusanyika anapokuwa Makonda?

Maana yake,anachokifanya Makonda wangekuwa wameshafanya ma DC, RC, wakurugenzi, mawaziri, manaibu waziri, jero nyingi zingekuwa zimeshasikilizwa!

Makonda ni wakwanza kufanya hivyo? Hapana! Si wa kwanza? Kwanini ghafla watumishi waliacha kusikiliza kero za watanzania Kwa kuingia field je walikatazwa? Noo big nooo

Tayari yake ni nini? Kiwango cha uwajibikaji,utu na kubeba matatizo yetu kama ya kwao ni hakuna kabisa!!

Atapendwa? Big Yes and big No! Justification on this? Atapendwa na matabaka mawili, tabaka la chini na tabaka la kati, lile tabaka analoligusa hawaezi kupenda anachokifanya na wapo tayari kukwamisha jitihada hizi Kwa gharama ya mauti na magonjwa!

Mwisho, Watanzania hawana haja na ofisi kama hazishughuliki na matatizo yao, anayeweza kusimama akashughulika na kero zao,hapohapo ndipo ofisi ilipo.

Kiu ya watanzania ni nini? Kupitia ziara hizo za Makonda? Mosi watanzania wanakosa haki zao za msingi pili Watanzania wanapenda sana viongozi kuingia field kutatua matatizo yetu tatu ambayo ni ya kwanza, Watanzania wanaweza kuonekana wamenyamaza kumbe mioyo yao inabubujikwa na machozi kama wakidharaulika.

Paul C. Makonda anageuka super sub inayotoa matokeo, huu mfupa sio mlaini ndio maana katika kipindi cha miaka 3, wenezi 3 wametafitwa katika nyakati tofauti tofauti.

Mungu anatukuzwa sana kupitia Paul Makonda, unakata kiu za Watanzania.

With thanks. Veronica France, fb on 5th feb 2024. Copy
Hivi tangu aanze ziara zake katatua kero ngapi zinazoonekana. Watu wanahombana kwenye ndoa wanamsubiri makonda awatatulie changamoto yao!
Kumtawala mtanzania rahisi sana.
 
Back
Top Bottom