Making money online - Maswali na Majibu.

leoleo-tu

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
1,268
3,511
Je, ni kweli unaweza kufanya kazi na kupata pesa kupitia mtandao?

Ndiyo, inawezekana kufanya kazi na kupata pesa kupitia mtandao.

Je, ni kazi gani mtu anazoweza kufanya kupitia mtandao?

Ni kazi nyingi karibu kila kazi inayoweza kufanywa ukiwa mbali (remotely) inaweza kufanyika mtandaoni na ukalipwa. Hii inajumuisha masuala ya kisheria, accounts, tafsiri, ukalimani, uundaji wa tovuti, maudhui, manunuzi kwa niaba ya mtu, ujazaji wa tanzudata, n.k.

Je, mtu anaweza kupata kiasi gani kwenye mtandao kwa kila mwezi?

Inategemea na mt una wateja anaowapata. Kuna ambao hawapati chochote na kuna ambao wanapata sana. Kama una wateja na uzoefu wa kutosha unawza kupata kuanzia $200 hadi hata $5,000 na Zaidi kwa mwezi kutegema na aina ya kazi unayofanya. Pia mapato hubadilika kulingana na msimu na kazi maana kazi nyingi si endelevu. Hivyo kuna msimu mapato yanaweza kuwa mengi na kuna msimu mapato yanashuka. Ila watu wengi mapato yao ni kati ya dollar 200 hadi 1000 kwa wmezi. Dollar 2000 na kuendela hao ni wachache hapa Tanzania.

Je, nitakuwa na uhakika gani kwamba nitalipwa?

Kwanza, fuata kanuni na masharti yaliyowekwa na jukwaa husika ulikokutana na mteja wako. Kama hukuktana naye kwenye jukwaa, fanya utafiti kidogo kujua kama ni genuine. Akianza kukwambia kwamba toa pesa ndipo akulipe basi hiyo ni red light.

Pia kama mteja ni genuine atakuwa anataka kujua maendeleo ya kazi yake. Lakini ukifaya kazi na mtu anakupa kazi hata hakuulizii umefika wapi, basi huenda ukajikuta unafanya kazi na hulipwi.

Zingatia your gut feeling sana. Maana kuna wateja wengine ni genuine lakini huwezi veify hilo.

Je, wateja nitawapata wapi?

Kuna mitandao ambapo kazi zinakuwa posted na mtu anaweza kuomba. Mitandao mashuhuri Zaidi ni Feelancer, Upwork, Fiveerr.

Pia wateja wengine unafanya Google searching kwa kutumia keywords utawapata kwenye mitandao mingine ambayo si mashuhuri. Sometimes unaapproach agencies pia.

Je, siwezi kupata mteja wa jumla mtandaoni?

Unaweza kupata kazi ikawa kama ajira. Kwa mfano, ukawa online tranlstor unalipwa dollar 5 kila saa utakayokaa online na kwa siku unakaa saa 9 whether ulifanya kazi au hukufanya. Japo rate ni ndogo lakini ni nzuri kwa sababu unakuwa unajua kila mwezi nitapokea $800, yani ni kama mshahara as compared na zile za leo zipo kesho hazipo ambapo malipo huanzia dollar $12 hadi hadi $100 kwa saa. Hii unaweza kupata leo na ikapita hata miezi hujapata.

Sometimes ukifanya pia kazi na agencies online basi kuna muda wanakufanya uwe labda recruiter au wanakuajiri kabisa. Mifano ninayo ya kutosha na unaweza sasa kuwekwa kabisa ofisini. It depends na performance yako na demand.

Je, online tasks zinaweza kuwa chanzo cha my income na nikajenga Maisha?

Absolutely, inaweza kabisa kukufanya ukaishi Maisha mazuri ya middle class kwa hapa Tanzania, ukamiliki makazi, usafiri na kuendesha Maisha. La msingi uwe na nidhamu ya pes ana uwekeze because kazi haziko guaranteed.

Je, ninahitaji kuwa na skills gani ili kuweza kufanya kazi online?

Skills zozote japo demand ya skills na malipo yanatofautiana. Skills nyingi mtu anazidevelop mwenyewe lakini ni afadhali ukawekeza kwenye zile skills ambazo una uhakika kuwa hautakuwa good but the best. Tumia muda kujifunza mambo mengi Youtube na mtandaoni maana kuna kila kitu.

Je, ni kazi inayoweza kufanywa na kila mtu?

Sidhani kama duniani kuna kazi inayoweza kufanywa na kila mtu. Kama ambavyo kuna watu wametajirika kupitia kilimo na wapo wengi amabo walijaribu ikashindikana, hata huku pia ni the same. It is not for everybody. Inahitaji uvumilivu na passion kufanikiwa maana wengi wanaishia njiani na wengine wanahisi huku hakuna kitu.

Ninaweza kusema ukiachilia mbali skills, na experience, hata bahati inahusika kabisa.

Je, ninahitaji nini ili kuanza?

Unahitaji PC na internet ili kuanza kuearn online.

Je, ninaweza kulipia kujifunza kufanya kazi online?

Sishauri mtu atoe pesa yake kufundishwa kumake money online maana mwisho wa siku it won’t work. Jikite katika kutafuta skills it takes time eventually you will make it. Hakuna easy money online na wala usiwe za ndoto utaingia leo upate pesa leo leo japo like I said, kuna watu wana bahati zao wanaingia ndani ya week wanapta pesa ya maana.
 
Back
Top Bottom