Makinda - Posho za wabunge hazitoshi

Makinda - Posho za wabunge hazitoshi

Kweli huyu supika haeleweki anasema posho ya wabunge haitoshi (ziko kati ya 120,000/= hadi 200,000/= kwa siku) ndio maana wabunge wanadai poshi mara mbili. je mtumishi waserikali anealipwa gross salary ya 135,000/= kwa mwezi mbona huyo supika hajamsemea au wale wa Njombe wana scale zao za mshahara. huyu mama hana hata punje ya aibu
 
Kwanza kabisa, tuainishe posho na marupurupu ya Mbunge ni yapi. Tuyajadili kwa kina na baada ya hapo tuanze kazi.
 
hawa watu bwana naona wanajifanya kuwa kama ni vipofu kabisa
hivi hawaoni yanayotokea huko kaskazini?
amakweli sikio la kufa halisikii dawa..
 
Makinda akome kabisaaa!! Posho za wabunge hazitoshi kwa misingi ipi!>??!?!
 
kafeli,keshashtukia jinsi asivyokubalika,na anavyopwaya bungeni kwahiyo kwa kujua wabunge wa ccm wote ni wapenzi wa rushwa kwa hiyo anatafuta kukubalika kwa njia hiyo nani kweli wabunge vilaza wa ccm watamuunga mkono. Ama kweli rushwa hupofushna macho ya wafalme.i.e watawala. Madam hawezi kuona halihalisi ya hata huko kijijini kwake.shame on you k*haba mkubwa wee!
 
Sio tu kwamba hazitoshi lakini wakubwa hawa wamekuwa wanaiibia nchi hii. Sheria ya kodi ya mwaka 2004 inasema hata allowances zinatakiwa zikatwe kodi (Sect 7(2)) . Wabunge hawa wamekuwa wakipokea posho zao ghafi na kutia mfukoni na hakuna hata senti tano wanazochangia kwenye maendeleo ya taifa hili . Cha kujiuliza ni kwamba hawa sio watanzania? Mbona hawataki kuwajibika na ujenzi wa taifa hili kwa kodi zao? Wote tunatakiwa tuchangie maendeleo ya taifa hili pamoja na wabunge pia.
 
Mie nadhani waendelee tu kujiongezea. Kwa kuwa uwezo huu tumeona ni sawa kuwa begani mwao, ni sawa. Ifahamike kuwa nyani akiingia shambani mwako hali kidogo ili kesho ajipatie pa kuendelea, ila kitakacho mtoa ni shibe tu. Hivyo basi ni wajibu wetu kama wenye shamba kutafakari kama ni vyema hawa nyani wakaendelea kuvamia mashamba yetu na kutuachia mabua tu. Nadhani ni wakati wa kubadilika na kukabiliana na matatizo mengi ya muundo wa kiutawala nchini mwetu. Tunamatamanio ya katiba mpya kuwa yaweza kulitatua hili. Je, tutashiriki vipi? Isijekuwa hatima ya haya yakajaachwa tena bungeni
 
Wapinzani Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na wegine mko wapi katika hili la Posho?? Mbona hampigi kelele zipunguzwe? Jamani hela ina shetani hata wale wanaojifanya wana uchungu sana na wananchi leo mbele ya pesa zao Kimyaaaaaaaaaaaaa, nyie wadanganyika nendeni tu barabarani mkavunjwe miguu wakati wenzako wako bizeee kupigania posho zao. Kwa mwezi mbunge anapata 12 millioni net hata zile za maendeleo ya jimbo hawaleti. Nyie wabunge WOTE MAFISADI PAPA
 
Haya yote yatakwisha kama tutakuwa na katiba mpya itakayoweka "governor" marupurupu ya wabunge. hao waliochangia Tsh 37 milioni ni wale walikuwepo kwenye kikao siku hiyo.

Sina uhakika lkn nafikiri Bunge letu lina jumla ya wabunge 350(?) Posho ya mbunge mmoja @day = Tsh 150,000/= Posho tu ya wabunge wanapokaa Dodoma kwa siku moja ni 150,000/ x 350 = 52,500,000/= Maana yake ni kwamba siku ile speaker alipo ahirisha bunge kwa siku moja Sisi walipa kodi tulipoteza pesa yetu Tsh 52.5 milioni.

Bila kuwa na katiba mpya haya yataendelea kututesa kwani hata yule kipenzi wetu speaker aliyepita Mh. Sitta anaye aliwahi kunukuliwa kwamba posha na marupurupu ya wabunge wa Tanzania ni ndogo ukilinganisha na wenzetu wa Kenya, akapendekeza posho na marupurupu yaboreshwa ili yalingane na wenzao wa Kenya. Kitu kikubwa ambacho hawataki kusema hawa MPs Je mishara na posho za watumishi wa serikali ya JMT na wenzao wa Kenya ziko je?

CCM, CDM, CUF, TLP, NCCR Wote wanaangalia matumbo yao tu Si Sitta, si Makinda, Si Zitto Si Regia, Si Hamad, Si Kafulila etc walau hata Dr. Slaa tulikuwa tukimsikia akisema kwamba posho za MPs ni kubwa mno ukilinganisha na wafanyakazi wengine wa serikali na alikuwa kitaja viwango.

Sasa swali langu kwa Mh. Regia mbona Dr. Slaa hakuchukuliwa hatua wakati huo? Au hizo kanuni na sheria zimeanza kutumika juzi tu baada ya wewe kuingia bungeni? Nchi hii ingekuwa na wanajeshi wenye akili nzuri sio vilaza kama akina Shimbo bora tutawaliwe tu kijeshi tujue moja. Wabunge ambao ni wawakilishi wetu mmetutosa.
 
Ikiwa Posho za wabunge hazitoshi, za wanafunzi vyuo vikuu si ndio balaaaaaa:A S 13:
 
Sisi mitanzania ni mijinga sana, hatuna utashi wa kukemea jambo na kusimamaia ukweli. Mie huwa nafika mahali na kuona kuwa hakuna haja ya kuwa na bunge( yaani vikao vya bunge kwa wabunge wote). Huwa nafika mahali na kuona kama vile hizo kamati za bunge ndo zingekuwa zinakutana kuwakilisha maswali, mapendekezo na maoni kutoka kwa wabunge wenzao. Sioni tija yoyote kwa wooote kuwapo mjengoni kwani hata maswali wanayouliza yanakuwa yalisha wasilishwa siiiiku nyingi kwa mawaziri husika na wao kuyatafutia majibu. Kwa maana nyingine wanapokwenda mjengoni ni kufilisi taifa letu kwa posho zisizokuwa na maana. Kwa mawazo yangu naona hakuna haja ya kuwa na bunge la kukutanisha wabunge woooote ili kupunguza gharama.
 
Hii ndio "itikadi ya ccm" Waumize wananchi utakapo pata nafasi serikalini. Makinda na ccm hawaoni aibu na wala tusitegemee wataomba msamaha.
 
Naomba hii kitu iwe hoja kuu katika kikao kijacho,kwanini wanalipwa mara mbili .yaani mshahara ,na posho ambayo inazidi mshahara.kwanini walipwe wakati wabunge wawapo bungeni ndiko kazini kwa kuwakilisha wananchi?kama anavyokuwa jimboni kwake anlipwa posho?ukweli ikifutwa hii kitu utaona mahudhurio yatavyoshuka
 
ahnhaaaa ndio maana vita ya ubunge inakuwa stiff saana kumbe kuna ulaji, hapo ndo tujue wabunge wetu hawana nia ya kutusaidia bali kuganga njaa
 
Gharama ya kujenga Kilomita 1 ya barabara kwa kiwango cha lami ni Shilingi Bilioni 1 (Moja), hivyo Shs Bilioni 900 ambazo zimetengwa katika bajeti ya 2011/12 kwa ajili ya watumishi wa kada ya juu serikalini kulipana posho, tena kwa kazi ambazo wanalipwa mishahara kuzifanya zinatosha kujenga Kilomita 900 za barabara kwa kiwango cha lami.

Kwa kuwa misongamnao ya magari mirefu katika miji ya Tanzania kama vile Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Tanga n.k husabishwa na uduni wa miundo mbinu ya barabara inayoelekeza magari yote kukutana katika njia panda zilizopitwa na wakati (Junctions) k.m katika Jiji la Dar es Salaam njia panda za Mwenge, Ubungo, Bguruni, Tazara, Changombe. Kurasini, Kamata, Veta, Ilala boma, Magomeni, Morocco n.k. Halii huwalazimu wakazi wengi wa jiji hili kudamka Kati ya Saa 10 na 11 alfajiri na kufika majumbani mwao kati ya Saa 2 na 3 usiku; ikiwa na maana ya kutu ia katika ya masaa 4 had 7 barabarani kila siku.

Aidha barabara mbali mbali zinazounganisha barabara kuu mbali mbali katika jiji hili (access road) zimejaa mashimo na hivyo kutopitika kirahisi, hali inayowafanya madereva kushindwa kuzitumia na hivyo kulazimika kujilundika katika barabara kuu chache zenye njia panda zinazosababsiha mlundikano wa magari

Laiti kama kwa mwaka huu wakubwa hawa walamba posho watakubali kusamehe posho hizi kama inavyopendekezwa na wapinzani, fedha hizi zitaweza kutumika kujenga barabara za mzunguko kutoka Bagamoyo Road kuja Morogoro Road hadi Nyerere na Pugu Raod hadi Kilwa road-

Kutoka Bagamoyo Road kuja Manzese hadi Port Access Road hadi Nyere Road. n.k na hivyo kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la mlundikano wa magari katika njia panda zilizopitwa na wakati
 
sasa kwa magamba hii kwao ni ndoto za alinacha, lkn sisi wanamapinduzi hicho kitu ni possible
 
Back
Top Bottom