Makinda - Posho za wabunge hazitoshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda - Posho za wabunge hazitoshi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Feb 22, 2011.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Akifungua semina ya wajumbe wa kamati inayojishughulisha na ukaguzi wa mashirika na taasisi mbalimbali za serikali, Speaker Makinda amewaonya wasipokee posho mara mbili mbili japokuwa anatambua kwamba posho zao hazitoshi.

  Hivi ni kweli posho za wabunge hazitoshi? Hivi wanataka makusanyo yote ya TRA yaishie bungeni? Selfishness is killing our beautiful country.

  TBC1.
   
 2. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mh.Makinda,spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa posho za wabunge ni kidogo hivyo atajitahidi kuboresha masilahi ya wabunge awamu kwa awamu ili kukidhi mahitaji ya wabunge na kuwafanya wasichukue posho mara mbili yaani kutoka bungeni na kwenye taasisi za umma.

  Amesema hayo katika ufunguzi wa semina ya wajumbe wa kamati za fedha inayoratibiwa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Source:Taarifa ya Habari ya TBC1 YA SAA 2:00 PM

  Maoni yangu:Jana kuna thread niliipost yenye kichwa cha habari 'Mishahara ya Wabunge',lakini kwa sababu nisizozifahamu thread hiyo imetupiliwa mbali na Mods.

  Msimamo wangu:Mishahara na posho za wabunge ni kubwa sana kulinganisha na wafanyakazi wengine katika nchi hii,ambao ndio watendaji wakuu wa kazi za kila siku za serikali,hivyo Anna Makinda kusema posho za wabunge ni kidogo ni dhihaka kwa wananchi.Tuukatae Umwinyi huu.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Inawezekana hazitoshi ila ni kwasababu wanahonga sana wananchi! wala si kwasababu ya kuhudumia!
   
 4. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  huu ni ubinafsi uliovuka mipaka wabunge posho yao kwa siku laki na nusu zaidi ya mara mbili ya kimambo cha chini cha mshahara wa kima cha chini wanatoa wapi ujasiri wa kudai ni mdogo? Shame on them
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nimeshindwa kumuelewa huyu spika wetu jamani......hawa watu mbona hawana huruma...
   
 6. k

  kayumba JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Hivi huyu spika anaishi Tanzania hii ya kwetu au nyingine?

  Mh. Spika unadhani posho ndogo ndiyo inafanya wapokee posho mbili mbili? Kama kweli hiyo ndiyo imani yako basi pole sana na uenda hujui nchi iko wapi kwa sasa!

  Ni juzi tumeambiwa wanapewa bahasha za Lunch zikiwa na milioni moja, sasa swali kwako Madame speaker. Unataka mpewe posho ya zaidi ya milioni au....?

  Nyie wabunge mnadhani ni hakina nani hapa nchini mpaka muwe na uwezo wa kujilipa hela mtakayo, mnaifanyia nini hiyo hela? Mbona tunaishi na nyie mitaani bila kuona tofauti ya mahitaji yenu na yetu?

  Amakweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa!
   
 7. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Hivi ni chombo GANI kinadhibiti masilahi ya wabunge kawa ilivyo kwa wafanyakaza? Hivi wabunge wakiamua wameamua? Kama chombo cha kudhibiti masirahi ya wabunge,tafadhali wadau naomba tuingilie kati kwani sisi ndio waajiri wao,sisi ndio tuamue walipwe Tshs ngapi.Halafu vipi kuhusu income tax,Je, wapunge wanakatwa income tax kwa mishahara yao?
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  hata hizo wanazopewa sasa ni nyingi sana!hawana kazi yoyote wanayofanya zaidi ya kutusomea kanuni za bunge!
   
 9. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Leo hii ametoa mchango wa Ths. milioni 37 ambazo ni mchango wa posho za wabunge na mawaziri za siku moja....
  bado ni ndogo hizo? hata kama wapo walioongeza pesa zao, kiasi hicho hata ukichukua nusu yake ni pesa nyingi sana kwa siku moja tu kutumika.

  Swali>Ze madamu ze spika, ze onarabo madam hizo ni ndogo?
  jibu> teh teh usisikilize redio mbao.

  Ze madamu wasomee watu wasikie mmechanga shilingi ngapi wasidhani mmechakachua.
  Ze madamu anajibu kwa hasira... wewe uliona wapi cheki inachakachuliwa?

  KWELI MADAMU WETU TUNAYE , KAAAZI KWELI KWELI . sWALI DOGO TU ANAG'AKA KAMA SIMBA KASHIKWA MKIANI LOOO.
   
 10. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Amenichefua kweli huyu mama leo.,eti posho hazitoshelezi...Haya ni matusi makubwa kwa mfanyakazi anayelipwa KCC!ama kweli watz tumekuwa tumekubali 'kuchezewa' makalio.
   
 11. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mbunge kimsingi ni mwakilishi wa wananchi, hivyo linawajibika kusimamia maslahi ya wananchi, halina uhalali wowote wa kujipangia lenyewe marupurupu manono yasiyolingana na hali halisi ya watanzania. Hii ni kinyume na utawala bora. Kila mtu anajua hivi sasa linapokuja suala la kujinufaisha bunge na serikali lao ni moja. Hivyo njia pekee ya kukomesha hayo ni kwa wananchi kuyapigia kelele.
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Waache wasaidie kuchochea hasira za nguvu ya umma
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  tunakoelekea watataka bungeni viletwe vitanda badala ya hivo viti maana wamezidi kulala
   
 14. m

  mams JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na kama aliwaahidi mkinipa Uspika nitawapa maslahi zaidi basi hiyo ni ahadi na ahadi ni deni!
   
 15. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  there is some truth on this!
   
 16. M

  Msanya Member

  #16
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Conflict of interest! Wanatunga sheria zinazowa'favour' wenyewe. Labda ni mbinu ya serikali/ mafisadi/corrupt system kuwatuliza. Tupige kelele? Kelele za chura lini zikazuia ng'ombe kunywa maji.
   
 17. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyu spika nina hakika kichwa chake sio kizuri, ina maana anajifanya hajui kuwa posho ya siku moja tu ya mbunge ni mshahara wa mwezi wa mwalimu!!!!!!
   
 18. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Shida tupu! Raha iliyoje unapokuwa na blank check kwenye kuamua mafao yako! Nadhani hapa kuna haraka ya katiba mpya! wakati wabunge wanajadili kuongezewa mafao yoyote wanayota walimu wa shule za kata, zahanati za vijiji hali ni mbaya!
   
 19. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  mkuu tusiishie kupiga kelele tu,bali tunapaswa kuwaonesha kwa vitendo kuwa haturidhishwi na madudu yao.Tufanye migomo nchi nzima.
   
 20. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Babu lao...ASHIBAE.....!
   
Loading...