Disclaimer:
I don’t care what two or more consenting adults do with regard to the choice of lifestyle they want to lead.
Now that we got that out of the way, please make it make sense!
LGBTQ rights are now the sociopolitical hot potato in these neck of the woods [ East Africa].
Raia wanatoa povu balaa. Kila mwenye kujiona ana umuhimu na kila mwenye kudhani akifungua mdomo wake na kutoa kauli, basi watu watamsikiliza, naye anatoa kauli yake ya msimamo wake kuhusu ushoga.
Maoni ya watu ni mengi na ni anuai. Kutoa maoni ni jambo jema kabisa.
Nilichokiona ni kwamba, kauli na sauti za kupinga mapenzi ya jinsia moja, ni nyingi na kubwa.
Ambacho sikielewi, hususan kwa wale wanaopinga hayo mapenzi, upingaji huo unaishia wapi?
Upingaji huo unaanzia na kuishia humu humu ndani ya mipaka ya nchi, au?
Kuna dhana inayoaminika kwamba mataifa ya nchi za magharibi ndiyo yanayo promoti hayo mambo ya ushoga huku kwetu.
Sasa katika kuukataa huo ushoga, inakuwaje kwa mfano, watu waendelee kutumia bidhaa za makampuni ya hizo nchi za magharibi ambayo yanajulikana kupromoti hayo mapenzi?
Mfano, iPhone zinapendwa sana Tanzania. Kampuni inayotengeza hizo bidhaa inajulikana wazi kabisa kuwa ina promoti hayo mambo.
Kampuni ya Apple ina mashoga wengi sana. Kuanzia juu kabisa [CEO] mpaka ngazi za chini, mashoga wapo.
Mtu hapa Tanzania unawezaje kuupinga ushoga kwa nguvu zako zote halafu kwa wakati huo huo utumie bidhaa za kampuni ijulikanayo kuongozwa na shoga bila ya kuwa mnafiki?
Please make it make sense….