Makapuku Forum

Screenshot_20211022-052525_Instagram%20Lite.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi ametoa mifuko 100 ya saruji kwa kijiji cha Makayo , Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe ili kuunga mkono nguvu za Wananchi katika ahadi ya ujenzi wa Zahanati ya kwanza katika kijiji hicho.

Basilla ametoa msaada huo mkubwa katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa baada ya jamii hiyo ya kabila la Wamasai kumualika kama mgeni rasmi katika hafla ya kimila ya kusimikwa Viongozi wa kimichezo 'malwaiganani' miezi miwili iliyopita.

Wananchi hao walitoa changamoto hiyo ya ukosefu wa Zahanati , sambamba na kuomba msaada huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe ambaye alishiriki rasmi kuzindua kuchimba msingi wa zahanati hiyo na wananchi kwa ramani ya Halmashauri na kuwaahidi kama ilivyotaratibu Halmashauri itakwenda kumalizia ujenzi huo wa Zahanati ili ukamiliike na huduma ianze kutolewa kwa Wananchi katika kijiji cha makayo.

"Wananchi walifurahia sana na kushiriki zoezi hilo kwa matumaini makubwa kwa viongozi imara walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan" ———
Screenshot_20211022-141102_Instagram.jpg
Screenshot_20211022-141127_Instagram.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma, ambapo amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula, Ndayishimiye yupo nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu.
Screenshot_20211022-141315_Instagram.jpg
 
Application ya Nala money iliyotengenezwa na Kijana Mtanzania Benji fernandes imeibuka kuwa Mshindi wa kitaifa kwenye Tuzo za TEHAMA za mwaka 2021 kama kampuni bora Tanzania inayochipukia kwenye teknolojia (BEST ICT Startup)

Kwenye picha anaonekana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Benjamin Fernandes Tuzo hiyo mpema leo kwenye Mkutano wa TEHAMA uliofanyika kwenye ukumbi wa AICC Arusha.

Ushindi wa Tuzo hii umekuja siku chache baada ya millardayo na kutangaza habari kubwa ya Application hiyo ya Nala Money kuanza kufanya kazi na kuwezesha mamilioni ya WanaAfrika Mashariki waliopo Nchini Uingereza kutuma fedha moja kwa moja kutoka Uingereza kuja Tanzania, Kenya na Uganda
Screenshot_20211022-141652_Instagram.jpg
Screenshot_20211022-141816_Instagram.jpg
 
Serikali ya Uingereza imeanza kuchukua hatua za kulinda haki za Wanyama wanaofugwa Majumbani ikiwemo Mbwa, Paka na Ndege ambapo sasa Wamiliki wanaweza kufungwa hadi wiki 51 au kulipa faini ya Euro 20,000 (Tsh. milioni 53) kama tu hawatowalisha vyakula sahihi Wanyama au Ndege hao.

Mamlaka inayosimamia haki za Wanyama nchini Uingereza ya Blue Cross imesema Mbwa wanapaswa kupewa diet nzuri inayotakiwa hususani vyakula vyenye protini nyingi kama nyama na kusema kinyume na hapo Watu watakuwa wanavunja Sheria ya Ustawi wa Wanyama ya Mwaka 2006.

Hii imekuja baada ya utafiti kuonesha kwamba Wamiliki wengi wanawalisha Mbwa mbogamboga za majani na sio nyama kama inavyotakiwa ambapo Mamlaka hiyo imesema kama Mtu anajiona hataki kula nyama labda kwakuwa anafanya diet ni uamuzi wake lakini asilazimishe mbwa wake kula vyakula vyake alivyoviandaa bali anapaswa kumundalia mbwa vyakula vingine vizuri anavyostahili.
Screenshot_20211022-142043_Instagram.jpg
 
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita imeahirishwa baada ya shahidi wa Jamhuri kudai bado anaumwa.

Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ramadhan Juma alitegemea kutoa ushahidi wake leo Ijumaa Oktoba 22, 2021, lakini Wakili Mwandamizi wa Serikali, Felix Kwetukia aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iahirishe kesi hadi Oktoba 27, 2021 kwa kuwa shahidi huyo afya yake bado haijaimarika.
Screenshot_20211022-142222_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom