Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211021-072158_Opera%20Mini.jpg
 
Mtandao wa Facebook umetangaza mpango wa kubadilisha jina la Kampuni hiyo ili kuu-brand Mtandao huo upya kufuatia matukio mfululizo ya habari mbaya na tuhuma mbalimbali ikiwemo kutumika kusambaza habari za upotoshaji na matokeo hasi ya huduma zake kuathiri afya za akili za Watu.

CEO wa Facebook Mark Zuckerberg amesema mpango wa kubadili Jina utafanyika kwenye Mkutano mkubwa wa Kampuni hiyo October 28,2021 na Mtandao huo umepanga kuajiri Wafanyakazi wapya 10,000 ili wafanye kazi ya ubunifu ili kuuboresha.

Kama watafanikiwa kubadili jina Facebook hawatokuwa wa kwanza, Kentucky Fried Chicken walifupisha jina lao na kuwa KFC, Brand ya Magari ya Kijapan ya Datsun ilibadili Jina na kuwa Nissan, Snapchat waliamua kujiita Snap mwaka 2016, Shirikisho la Mieleka Duniani (WWF ) lilibadilika na kuwa WWE.
Screenshot_20211021-122449_Instagram.jpg
 
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza rasmi kuwa hivi karibuni atazindua Mtandao wake wa Kijamii ambao utakuja kuwa Mtandao bora Duniani ambapo amefanya hivi kufuatia kufungiwa kutumia Facebook na Twitter baada ya kudaiwa kuchochea vurugu katika Majengo ya Bunge Marekani January 6 2021.

Mtandao huo utaitwa TRUTH Social na utamilikiwa na Trump Media & Technology Group (TMTG) na unatarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao ambapo kwa sasa tayari upo tayari Apple Store wameanza kuuweka hewani kwa baadhi ya Watu kwa pre - order.

Trump amesema "nimeamua kuanzisha TRUTH Social ili kupiga vita uonevu kwa wanaomiliki Mitandao, tunaishi kwenye Dunia ambayo Taliban wanatumia Twitter halafu Rais kipenzi cha Watu wa Marekani ananyamazishwa hii haiwezekani"
Screenshot_20211021-122647_Instagram.jpg
 
Bujumbura. Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda anatarajiwa kutembelea Kiwanda cha Mbolea cha Fomi mjini hapa, kilichoanza ujenzi wa kiwanda cha mbolea jijini Dodoma, kupitia kampuni yake ya ITRACOM.

Profesa Mkenda ambaye yuko Bujumbura, Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, alisema jana kuwa mkakati wa Serikali ya Tanzania ni kuhakikisha mbolea inazalishwa nchini ili kuondokana na utegemezi wa uagizaji wa mbolea kutoka nje ya nchi.

Katika ziara hiyo, Profesa Mkenda atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa Burundi kuhusu utekelezaji wa mifumo ya utoaji ruzuku kwenye pembejeo za kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Profesa Mkenda alisema takribani asilimia 90 ya mbolea ya Tanzania inaagizwa nje ya nchi.

Pia, alisema ujenzi wa kiwanda hicho utakapokamilika, kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 600,000 za mbolea ambazo ni zaidi ya mahitaji ya tani 400,000 hadi tani 500,000 kwa mwaka.
Screenshot_20211021-122800_Instagram.jpg
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamewasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Alhamisi Oktoba 21, 2021 ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Oktoba 15.

Katika kesi hiyo Sabaya na wenzake watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Screenshot_20211021-122859_Instagram.jpg
 
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limelemewa na deni la Sh403 bilioni ilhali mtaji ilionao ni wa Sh243.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Japhet Hasunga amesema hayo jana Jumatano Oktoba 20, 2021 baada ya kuipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/20 ambapo amesema wamebaini kuna viashiria katika Shirika hilo kutofanya vizuri kwakuwa lina mtaji hasi wa Sh132 bilioni na madeni makubwa kuliko mtaji wake.

“Hicho ni kiashiria kuwa bado shirika haliendi vizuri. Shirika letu linalipa hadi kodi lakini mapato yao hayajaingizwa katika vitabu vyao,” amesema Hasunga.
Screenshot_20211021-122958_Instagram.jpg
 
Jana timu 19 za EPL zikaungana kuishabikia Atalanta BC

Hilo linajulikana na imepigwa comeback ya kibabe sana

Nasikitika sana kuona hata Arsenal alikuwepo kwenye huo mkumbo, yani Arsenal??
Screenshot_20211021-123256_Instagram.jpg
 
AZAM WANAITAKA PYRAMIDS!

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Azam FC zakazakazi , wachezaji wa klabu hiyo wanataka kushinda mechi ya marudiano dhidi ya Pyramids.

“Kama kuna watu wanataka kushinda mechi hii basi ni wachezaji, wengine wote tunatamani [viongozi, mashabiki] lakini wachezaji wanatamani zaidi kwa sababu kwao itakuwa historia.”

“Pyramids haijawahi kutolewa na timu ya Tanzania japo imeshacheza na timu za Tanzania. Sio kushinda tu, hata kutoka sare kama sisi wenzetu hawajawahi. Kwa hiyo kuitoa kwenye mashindano itakuwa rekodi kubwa zaidi na hicho ndio kitu wachezaji wetu wanatamani.”
Screenshot_20211021-123402_Instagram.jpg
 
Kikosi cha Azam FC tayari kimewasili Cairo, Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC.

Msafara wa Azam FC una jumla ya watu 51 [wachezaji 25, benchi la ufundi na viongozi] wachezaji waliobaki ni Prince Dube ambaye anauguza majeraha na wengine watatu ambao wamesimamishwa.

Zaka Zakazi amesema Azam FC imesafiri na wachezaji wote ambao wako fit hata ambao hawatocheza mchezo wa marudiano ili kujenga umoja kwenye timu. Keneth Muguna amefungiwa mechi nne za CAF [ameshatumikia mechi tatu, mechi ya Pyramid vs Azam itakuwa ya mwisho kutumikia adhabu yake], Ivan Mbala alisajiliwa wakati dirisha la usajili la CAF limeshafungwa.
Screenshot_20211021-123515_Instagram.jpg
 
Gym ziwe nyingi tafadhali tunaweza kuongezeka uzito wakati wowote kuanzia sasa [emoji3]

Mchezo wa 300 kwa Cristiano Ronaldo ndani ya Manchester United
Screenshot_20211021-123654_Instagram.jpg
 
DEAL DONE| SEY [emoji654] Sharkia El Dokhan FC
.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana Stephen Sey (27) amejiunga na klabu ya Sharkia El Dokhan inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri El [emoji1093] akitokea Namungo FC.
.
Ikumbukwe Sey alifunga mabao 5 katika mechi 11 kwenye Kombe la Shirikisho la Afrika msimu uliopita, na kuisaidia Namungo kutinga hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.
Screenshot_20211021-123907_Instagram.jpg
 
“Sadio Kanoute, Sakho na Nyoni wanakuja vizuri na naamini watakuja kuleta vitu vizuri siku za mbele. Najiamini sana kutakuwa na mambo mazuri siku za mbele, wachezaji wote wanabadilika kiuchezaji.”
.
“Tumeanza kubadilika eneo la ushambuliaji. Kiukweli kuondoka kwa Luis na Chama unatakiwa utafute njia nyingine ya kwenye ushambuliaji. Tupo njia sahihi mpaka sasa,”

- Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba SC.
Screenshot_20211021-124029_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Jana yule Bishoo Bruno Fernandes kila akitaka kushika mipira ya faulo kupiga, Mwanaume Cristiano Ronaldo anamwambia "tulia mdogo wangu hizi shughuli za kiume" [emoji1]

Nachokiona huyu Mtoto Bruno anapaswa sasa kutulia atapata presha kubwa kukimbizana na kivuli cha Ronaldo, hizi faulo na penati naona ni wazi Mnyama ameshapewa sasa

Game dume kama hizi ambazo dunia imechukua upande wake basi anakuwepo Cristiano Ronaldo anakuja kukupa utofauti mkubwa na jana aliitengenisha mechi

Namkumbuka Ronaldo dhidi ya Wolfsburg akiwa pale Real Madrid zile chuma tatu alizoweka ilikuwa ni comeback, aliweka tena tatu dhidi ya Atletico tena nusu fainali ya UEFA hiyo, huyo amezaliwa kwa ajili ya mitihani migumu

Jana dakika za mwisho ametenganisha tena maji na mafuta[emoji119] ni muda sasa wa Bruno kuelewa nguvu ya Ronaldo, yani Ronaldo kafunga moja na Bruno kapiga assists mbili, ila kwenye Mchezaji bora wa mechi, Ronaldo kashinda kwa 41% ya kura dhidi ya wachezaji 16

Ronaldo back to the theater of dreams and dreaming again, Manchester United wana timu mbili! Kwanza United na pili ni Ronaldo

Screenshot_20211021-124337_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom