Makapuku Forum

Nashindwa kuwachukia liver fans maana wengi ni ndugu
 
Ingekuwa nchi zilizoebdelea Rais kamtumbua IGP kiboyaboya anayeteuliwa anakataa uteuzi pia aliyepigwa chini hakubali kupelekwa kwingine anaandika barua kuomba kustaafu

Wenzetu siyo team njaa njaa
........


...ukiachana na suala la nchi zilizoendelea, ni suala tu la mtu binafsi kujithamini na kujitambua. Kwenye suala la kujitambua huwa inafikia wakati unashindwa kuwatoautisha viongozi wa dini na wanasiasa, wasomi na wasiosoma (kwa maana ya kutokwenda darasani). Ndiyo, inakuwa ngumu sana kama Fela Kuti na nyimbo zake za kisiasa ambapo analaumu baadhi yetu kutanguliza maslahi binafsi na kuyadharau ya wengi.

Nitakupa mfano mwingine wa karibuni tu huko US, ambapo POTUS alipomwaga bosi wa FBI, iliaminika kabisa uchunguzi uliokuwa unafanywa ungefanywa na msaidizi wake anayekaimu lakini aliamua kumpa mamlaka ya kuchunguza mtu asiyhusiana na serikali. Huku kunaitwa kujitambua.

Leo hii Kitila anasema bajeti ya maji inatosha (huku ikiwa imepunguzwa kwa ma-asilimia mengi tu) na kuwashangaa wabunge wanaoamini hii bajeti ni ndogo. kabla ya kupewa ulaji alikuwa ni critic mkubwa tu.

Lakini kama alivyowahi kusema kadinali Pengo, 'je unaichukia rushwa toka moyoni au ni kuwa tu wewe si sehemu ya hiyo rushwa'
 
Umeongea ukweli mtupu Bitoz, angekuwa ni Pasko saa hizi watu wangempa sifa zote.
 
Ingekuwa nchi zilizoebdelea Rais kamtumbua IGP kiboyaboya anayeteuliwa anakataa uteuzi pia aliyepigwa chini hakubali kupelekwa kwingine anaandika barua kuomba kustaafu

Wenzetu siyo team njaa njaa
........
Unajua sababu yake? Wenzetu kule mara nyingi kugombea cheo cho chote ni lazima uwe na pesa za kueleweka. Uwe na vibiashara vyako vinavyoeleweka na kamwe hawategemei siasa ili kuendesha maisha yao. Siasa wanajiingiza ili kupata influence waendelee kupitisha sheria zenye usalama zaidi kwa biashara zao ili waendelee kujinufaisha zaidi na zaidi. Ndiyo maana kwa wenzetu hawa kuachia madaraka na kujiuzulu is no big deal. They are already set for life.

Wakiacha madaraka, hata kama siyo wafanyabiashara wakubwa au matajiri, wanajua kuwa watapiga hela ndefu kwenye vitabu na hata mihadhara ya kualikwa katika taasisi mbalimbali husika. Mkuu wa polisi kama Mangu huko angeweza kutoza hata dola 100,000+ kwa mhadhara mmoja kuhusu mambo ya usalama, madawa ya kulevya na ugaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Akitoa mihadhara 30 kwa mwaka tayari ni pesa ndefu ya kutosha. Directors wengi wa CIA, FBI na hata wakuu wa polisi wa miji mikubwa kama Chicago, Los Angeles na New York hupiga pesa ndefu kwa njia hii ali mradi tu wasifichue mambo ambayo bado yapo classified.

Naamini Mangu ni tajiri tayari na ana mafao ya kutosha lakini kustaafu na kulinda hadhi ya jina lako katika historia bado siyo utamaduni wetu. Watu wako radhi kudhalilishwa na wanasiasa, kujinyenyekeza na hata kupoteza utu wao. Ni aibu tupu!
 
Nimeipenda hiyo sentensi ya mwisho. Ndiyo maana tukaambiwa kwamba kuna tofauti kati ya kula mlenda kwa sababu huna uwezo wa kununua nyama na kula mlenda hata kama una uwezo wa kununua nyama. Mwanasiasa wa Bongo atapiga makelele kupinga rushwa wakati yuko nje ya mfumo lakini akiingizwa ndani ya duara na kuwa sehemu ya mfumo hutamsikia tena. Siasa uchwara!
 
Utashangaa anaenda kuwa Mkuu wa Mkoa au Katibu Mkuu wa Wizara.
Yule Mkuu wa mkoa wa Morogoro aliyetumbuliwa kipindi kile akaanza kulia kuwa anatoka ukoo masikini na ana familia inamtegemea, wakati ana PhD ya kilimo alinisikitisha sana. Wanachukulia vyeo hivi kama ajira za kudumu hata kama wamefisadika vya kutosha. Inashangaza sana!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…