FurahiDei is Old: Muziki Unatuchekesha
Habari Makapuku, nina imani siku imekwenda vizuri na tunauanza mwanzo wa weekend. Hivi leo ndo siku ya kuvunja jungu eeh au bado?
Maana tunajiandaa na mengi mfungo huu, aidha kwa kukosa au kupata. Yote iwavyo, leo ni ijumaa, furahiday na inabidi tufurahi.
Kwa wapenzi wa muziki na hasa band ambapo unaliskia gitaa kwa uzuri kabisa basi leo tuangalie muziki mchangamfu. Muziki wa kukatika, yaani kunyongorosha kiuno na mapega feni lisingiziwe.
hapa gitaa zinacharazwa kwa umakini utafikiri mwalimu wa nidhamu kashika wiki
naongelea bendi iliyokuwa na fujo miaka ya 90s hapa Africa Mashariki. Nawaongelea Katitu Boys, wana micharazo
Hebu waangalie kwenye clip hii ya YouTube.
Ukimaliza kuwaangalia mimi nitakuwa hapa hapa naangusha moja moja bila kujali nitasema nini baadaye