
ZABURI 122
1.Nalifurahi sana waliponiambia na twende nyumbani kwa BWANA.
2.Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako,Ee Yerusalemu.
3.Ee Yerusalemu,uliyejengwa kama mji ulioshikamana.
4.Huko ndiko walikopanda kabila za BWANA.Ushuhuda kwa Israel.Walishukuru jina la BWANA.
5.Maana huko viliwekwa viti vya hukumu.Viti vya enzi vya mbari ya Daud.
6.Utakieni Yerusalemu amani, Na wafanikiwe wakupendao.
7.Amani na ikae ndani ya kuta zako Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8.Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu,Niseme sasa,Amani ikae nawe.
9.Kwa ajili ya nyumba ya BWANA,Mungu wetu nikutafitie mema