Makapuku Forum

Makapuku Forum

592d672efd6e06319769fbb279c6d664.jpg
c397b0cc5a5dd615cb729a797c671c1b.jpg

Ila Hitler baada kugundua wana IQ kubwa na nguvu akaamua kuwapunguza kwa kufanya mauaji kibao
....
So bad
 
NUKUU YA LEO
“Nibora kuishi na fikra hai kuliko kuishi na fikra zilizo kufa”
“Unaweza kuwadanganya watu wote kwa muda fulani na baadhi ya watu wakati wote ila uwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote”

hayo maneno yaliwahi tamkwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa letu

Alizaliwa tarehe 13/4/1922 na kufariki tarehe 14/10/1999

Ameacha mke mmoja mama maria nyerere na watto 7 mtto mmoja alifariki

muwe na siku njema.
b8ef4335a05a6e1b898e5e1b5e0f15da.jpg
4079e0cf9f822a1f08bbad9c25b69be6.jpg
Asante kwa Nukuu Shunie Ubarikiwe Nyerere anaishi milele.

APUMZIKE KWA AMANI J.K NYERERE


Unajua Shunie,hauko peke yako kipenzi,mama zetu wako mbinguni tuendelee kuwaombea ,Mungu atakapotuita,watakua wenyeji wetu hatutahangaika.

Naomba nikutie moyo ,Omba sana kwa ajili ya mama,futa machozi,jitie nguvu na moyo mkuu,zidisha maombi juu yake,yeye anakuona na anatabasamu na anakupenda sana ila Mungu aliamua maana alimtengenezea makao mengine,Mungu alikua na kusudi na mpendwa mama.

PUMZIKA KWA AMANI MAMA SHUNIE

PUMZIKA KWA AMANI MAMA BLESSEDHOPE

PUMZIKA KWA AMANI WAMAMA WOTE WA MAKAPUKU WALIOTANGULIA

PUMZIKA KWA AMANI MAREHEMU WOTE


TUNAWAPENDA SANA
 
Heshima kwa Mama.

'Nani kama mama?' Hii huwa ni kati ya sentensi chache za Kiswahili ambazo zinajieleza kama swali na wakati huo huo zikijieleza kama taarifa (rhetorical question). hakuna asiyejua nafasi ya Mama katika malezi ya wengi wetu. Mama ni mama na hakuna wa kufananishwa naye.

Je, kila mama ni mama? Kwa mtizamo wangu kuwa Mama ni zaidi ya ile hali ya kunizaa, Mama ni mama pale majukumu ya umama yanapotekelezwa inavyotakiwa kwa nia kubwa moja tu ya kujali na kulinda maslahi ya mtoto. na kwa kulinda maslahi haya ndipo tunaposema huyu ni mama.

Siku hii ya mama kimataifa inaenda kuwa ikipata umaarufu miaka ya hivi karibuni na wengine kudhani kuwa ni siku mpya kabisa, la. Siku ya Mama imekuwepo wakati wote na hata sisi Watanzania na Waafrika kwa ujmla tumekuwa tukiikumbuka kila wakati tofauti na wenzetu ambao kwa kuiona kuwa ni fursa ya kutengeza pesa wameamua kuibiasharisha hii siku Ccommercializing Mother's day.

Tumekuwa tukiwasaidia mama zetu kwa mambo kadhaa kuanzia ya kifedha hadi ya hali, kuleta maji nyumbani, kubeba kuni alizokata, kumsomea meseji za simu (kwa wale waliowanunulia simu za tachi, mnajua nasema nini ), kumpeleka kliniki anapohitaji na mambo kadhaa.

Kama unadhani umama unaishia kwenye kuzaa tu basi tafuta maarifa zaidi, hivi unajua mwanaharakati aliyeipatia siku hii umaarufu mkubwa huko USA, bibie Anna Jarvis hakuwahi kuolewa wala kuzaa?

Umeshawahi kukisoma kitabu cha Brecht (1944) kinaitwa The Caucasian Chalk Circle, hapo utajua kuwa mama ni zaidi ya kwenda 'leba' kuwa mama ni lazima uwe na "umama" ndani yako. Na hivi ndivyo ilivyotokea pale Grusha, mjakazi (housegirl) alipopewa heshima ya kuwa mama wa mtoto Maiko ilhali mama halisi (biological mother), ambaye ni mke wa gavana akinyimwa haki hiyo.

Ukiona mtoto anamuita bibi yake mama na mama yake anamuita kwa jina lake basi utajijibu nani ni mama wa kweli.

Nani kama Mama. Na ndiyo maana wengi wetu tuko hapa JF na Makapuku forum kwa sababu nyuma yetu yupo au alikuwepo Mama ambaye alihakikisha tuna tabia na mienendo inayopaswa kufuatwa.

Mama kaimbwa sana, kuanzia Dear mama (2pac) Mama (boyz2men), Thank You Mama (Sarafina), God spend a little more time on you, mama, nani kama Mama' na nyingine nyingi.

Tunaposherehekea huku dunia ikiwa imevaa kimini (mihangaiko ya maisha imetupeleka mbali na kina mama) basi tuchukue nafsi japo ya kuandika barua, ujumbe mfupi au kupiga simu dakika tatu na kusema asante mama.

Binafsi nitapiga simu (nina simu ya tachi FYI) na nitamwambia Mama, "Mayu nimekukumbuka"
Nakuacha na Christian bella na Dimpoz wakijiuliza swali elezeshi, Nani Kama Mama"

Nakupenda kapuku mwenzangu

Najua nimeandika marefu na nashukuru kwamba umesoma kufikia hapa


HAKUNA KAMA MAMA LOVE YOU MAMAYANGU HUKO ULIKO PUMZIKA KWA AMANI,NAKUPENDA SANA MAMA,NAYAFANYA YOTE ULIYOYAFANYA KWANGU KWA WAJUKUU ZAKO,NAJISIKIA FAHARI KUWA BINTI YAKO..TUTAONANA TENA MAMA KIPENZI LOVE YOU MUM...LOVE SWEETIE MUM..LOVE YOU ALWAYS .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom