Ishi na watu kwa wema utafurahia muziki
Najua tumekuwa na wakti mzuri na tunapoenda kuimaliza Jumatano hii basi kama kawaida Makapuku nawakaribisha katika ka-kipengele haka ka ala za muziki na hasa tukijikita katika udonoaji na wadonoaji wa gitaa.
Kwa wapenzi wa muziki wa dansi miaka 20 nyuma, na wanaofuatilia miziki ya bakulutu, bendi ya Maquis Original ni bendi yenye umaarufu mkubwa hapa nchini ikiundwa na wanamuziki wengi toka Kongo na mmoja wao ni mpiga gitaa maarufu Dekula Kahanga almaarufu Vumbi. Mitindo kama Zembwela na Sendema haiwezi kukutoka kiurahisi.
Sikiza vibao cha
Ngalula, Mayanga, Makumbele, Karubandika na vingine vingi katika mitindo ya Sendemaa na Zembwela. Gitaa utakalosikia linamuongoza muimbaji awe ni Tshimanga Assossa au Kasaloo basi ni la nguli Dekula Kahanga.
Bado yupo na anafanya muziki wake nchini Sweden akiwa na band yake ya Dekula Band.
Hapa nakuwekea baadhi ya nyimbo alizoweza kuzicharaza na kuzifanya zikavutia zaidi.
FYI: Upigaji wake mzuri umechangiwa zaidi na kufuatisha mipigo ya Nguza Viking (yupo jela sasa akitumikia adhabu ya maisha gerezani)
Dekula anaamini katika kuishi vizuri na watu, kwani huwezi kujua maisha yatakupeleka wapi.
hapa najiuliza nikuache na Ngalula au nitupie clip ya YouTube ambayo anacharaza baadhi ya nyimbo zake, isiwe ishu, nakuacha na zote mbili, suala la kukumalizia MB zako mpenzi msomaji liko nje ya uwezo wangu (joke)