BWANA YESU APEWE SIFA
JIONI HII MUNGU ANASEMA NAWE/NAMI YAKUWA
USIOGOPE/NISIOGOPE
1.....maana nimekukomboa;nimekuita kwa jina lako,na wewe u wangu.
2 upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe;na katika moto,hautateketea;wala mwali wa moto hautakuunguza
3.maana mimi ni BWANA MUNGU WAKO,Mtakatifu wa Israel,MWOKOZI wako.....
ISAYA 43:1-3
HALELUIYA
Hakika hatupaswi kuogopa jambo lolote wala kitu chochote MAANA MUNGU YU PAMOJA NASI KUTULINDA
Jambo muhimu ni kumtii
Wakati mgumu,kukosa kazi,kuachwa,kudharauliwa,kukosa kuoa au kuolewa,kukosa watoto ,kuugua,mazingira magumu ,kuuguza isiwe sababu ya kuacha kumwabudu Mungu.
Mungu anatupenda na kamwe hatatuacha.TUSIOGOPE
TUOMBE
MTAKATIFU MTAKATIFU MTAKATIFU BWANA MUNGU WA MAJESHI ASANTE KWA YOTE UNAYOTUTENDEA TUNAKUSHUKURU KWA UPENDO NA WEMA WAKO KWETU,ASANTE KWA ULINZI WAKO NA AHADI ZAKO ZA MILELE TUNAOMBA UTUIMARISHE KIROHO HATA TUNAPOPITIA CHANGAMOTO YOYOTE TUKUONE WEWE,ASANTE BABA KWAKUA UMETUAHIDI ULINZI DAIMA
TUNAOMBA NA KUSHUKURU
AMEN
MBARIKIWE