Makapuku Forum

Asante sana mkuu. Maisha yetu hapa duniani kweli ni kama maua. Juzi nimeongea na schoolmate wangu mmoja akaniambia ana homa homa inamsumbua just now hata sijaamka vizuri napigiwa simu kuwa katangulia mbele ya haki. Jamaa mchacharikaji ndiyo tu kamaliza kushusha mjengo wa kufa mtu huku akiwa tayari sasa kuanza kutafuta mwenza. Just 29 yrs old huyooo tayari keshatangulia.

Tufurahieni maisha hapa duniani lakini kamwe tusisahau kuwa tu wapitaji tu na harakati za kujitafutia mali na raha zingine zisitufumbe macho mpaka tukasahau hata kumkumbuka Mungu katika maisha yetu. Tukumbuke kuwasaidia binadamu wenzetu wanaoteswa na magonjwa na umasikini. Tuwatembelee mayatima. Tuwaliwaze wenye matatizo. Tuwe wanyenyekevu na zaidi ya yote tujiweke tayari kila siku ili tunapojikabidhi mbele yake Aliyetuumba tukawe na kibali machoni mwake kwa kadri ya Neema zake na upendo wake kwetu. Muwe na siku njema makapuku.

Miye kuna dentist kakorofisha jino langu yaani linauma kuliko hata kabla sijaenda kwake. Jino lilikuwa na tobo (cavity) kaliziba sasa ananiambia eti si ajabu nikahitaji root canal. Hovyo kabisa. Leo naona nitashinda tu nimelala nikilisikilizia. Mniombee!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…