Makapuku Forum

Makapuku Forum

10/Afghanistan
a4ab9a30c3f3d2d2896eaf409e6b89a0.jpg

Taifa hili la Kiarabu pato lake ni USD 1072...uchumi wake umeporomoka kwa takriban miongo mitatu mfululizo
Vita vya Soviet pia vimechangia kuporomoka kwake kiuchumi
Hawa wavaa kanzu na kushinda misikitini ndo Waarabu pekee maskini zaidi
Chanzo kikuu ni kuandamwa na vita visivyoisha
......
aisee
 
NABII AFRIKA KUSINI AMTADBIRI UGONJWA KIONGOZI wa UPINZANI TANZANIA

Kiongozi wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering (ECG) la Afrika Kusini, Nabii Shepher Bushiri amemtabiria ugonjwa hatari kiongozi wa upinzani wa Tanzania, akisema maombi pekee na imani yake ndio vitamnusuru asitokewe na “kitu kibaya”.

Nabii Bushiri pia amesema mwaka 2018 utakuwa mgumu kwa Tanzania kuliko wakati mwingine wowote, akishauri wananchi wafanye maombi kuiepusha nchi na hali hiyo.

Bushiri alisema hayo wakati wa ibada ya Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika kanisa lake nchini Afrika Kusini na kurushwa moja kwa moja katika mitandao ya kijamii.

“Tanzania itapata shida ambayo haijawahi kuiona. Sisi kama kanisa, ni jukumu letu kuyaombea mataifa kwa sababu tumeitwa kwa ajili ya mataifa,” alisema Nabii Bushiri akiwa ameshika bendera ya Taifa ya Tanzania mkononi na shingoni akiwa amejifunga skafu yenye rangi za bendera hiyo.

“Tunaiombea Tanzania katika mwaka 2018, huruma za Mungu ziwe juu ya Tanzania kwa mwaka 2018. Tunaomba katika jina la Yesu. Tunaomba ulinzi.”

Wakati akiendelea na maombi hayo katika kanisa lililojaa waumini walioshika bendera za nchi zao, Bushiri aligeuzia maombi kwa ajili ya kiongozi huyo wa upinzani Tanzania.

“Tunamuombea kiongozi wa upinzani, kiongozi wa upinzani. Naona tatizo linaibuka kwenye ini lake. Lakini tunaomba huruma (ya Mungu) nazungumza kijasiri kadri ninavyoweza, kwa sababu najua (hili) linatoka kwa Bwana,” alisema nabii huyo. “Narudia hili. Nililizungumza miezi kadhaa iliyopita, (lakini) narudia kuhusu huyu mtu. Muda mfupi ujao ataanza kuzizima kama mtu anayesikia baridi. Lakini ni shambulizi hatari ambalo linahitaji maombi. Bila hivyo, kitu kibaya kitamtokea.

“Lakini mimi na wewe tunaweza kuzuia kama hata yeye ana imani. Lakini tatizo ni kwamba sioni imani kwake. Tunamuombea na tunaomba ulinzi. Inaweza isitokee sasa, lakini tunaomba ulinzi wa maisha yake.”

Nabii Bushiri ni mzaliwa wa Malawi, lakini anafanya huduma zake na biashara nchini Afrika Kusini ambako amejizolea waumini kutoka mataifa mbalimbali.

Bushiri aliwahi kutabiri kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini Tanzania wakati alipotembelea Dar es Salaam Julai mwaka jana. “Nakumbuka mwezi uliopita, Mungu alinituma Tanzania kwenda kuzuia mauti. Nilikuwa nasali saa 1:00 asubuhi na nusu yake ikageuka kuwa damu,” alisema Bushiri katika mahubiri yake ya Julai 14, 2016 jijini Dar es Salaam.

“Nilimuuliza Mungu, nini maana yake. Na Mungu akaniambia ‘siku ya damu inakuja’. Nikasema hilo ni nini. Niliona watu wakifanya mambo yao na ghafla nikaona damu ardhini. Na Mungu akaniambia ‘iombee Tanzania’.

“Nilipokuwa nikiomba, nikaanza kutetemeka. Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka. Na nikamuuliza Mungu, mtetemeko huu ni wa nini? Na Mungu akaniambia ‘hili ni tetemeko la ardhi. Si Dar es Salaam. Kutakuwa na tetemeko sehemu nyingine ya nchi.”

Katika ibada hiyo, Nabii Bushiri aliwataka waumini wake waiombee Tanzania kuiepusha na janga hilo.
Nilikuwapo DIAMOND JUBILEE na ECG Makongo akitabiri kuhusu tetemeko na kiongozi wa upinzani mwaka jana Julai. Na ibada hiyo. Juzi niliifuatilia live Maombi ni muhimu sana kwani yapo mengi yanayoendelea na ambayo hakika yanaweza kutudumbukiza popote.Mungu atusaidie.
 
9/Madagascar
cf1f4355b38cdbb8bfa2fb557a03b955.jpg

Kisiwa hiki kilichopo Kusini mwa Afrika kipato cho la ni USD 972
Hakijasumbuliwa sana na vita hivyo uchumi wake upo kwenye mielekeo wa kukua maana kuna uboreshaji wa elimu, afya., miundomini n.k hivyo uchumi wao utakuwa km Wa Sizonje
Miaka ya karibuni Uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ulileta kasheshe
.....
 
8/Malawi
5d05310a5f50e273ade6debb8fd2a23d.jpg

Tuwaonee huruma hawa jirani zetu kuhusu Ziwa Nyasa...Janchi wenyewe kamejichokea tayari, kipato chao ni USD 894
Hawa jamaa 85% wanaishi maporini(maeneo ya vijini) tatizo lao kubwa ni ugonjwa wa Ukimwi
Hivyo msijiulize sana kwanini Wanyakyusa wa Kyela wanaongoza kwa Virusi vya Ukimwi huko Mbeya....ni jirani zao!!!!
......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom