Makapuku Forum

NUKUU YA LEO


The successful man will profit from his mistakes and try again in a different way

Mwanadamu mwenye mafanikio anafaidika kutokana na makosa yake kwa kuwa atajaribu tena kwa namna nyingine


Haya maneno yalipatwa kusemwa na mwandishi mashuhuri / mkufunzi wa masuala ya utawala Bw. Dale Carnegie aliezaliwa 24/11/1888 na kufariki 1/11/1955




Dale atakumbukwa kwa kazi zake nzuri juu ya utawala na uongozi wa watu. Hadi leo hii kazi zake zinauzwa na zinatumika vyuoni na sehemu mbali mbali duniani kote.

Moja ya kazi zake nzuri ni How to win friends and influnce people na How to stop worrying and start living

Morning motivational

Ili kufanikiwa ni lazima uwe na mipango, mpango mmoja hautoshi wewe kufanikiwa, hivyo lazima uwe na mpango wa ziada (plan b) .

Siku zote binadamu tunajifunza kwa makosa , unapokuwa na ujasiri wa kujaribu pale unapokosea ndio kufanikiwa kunapokuja..

Usikubali kushindwa hata siku moja. Try again and try again !

Binafsi mimi nimesoma vitabu vyake. Nimejifunza mengi na vimenijenga hata kimtazamo..

Try again! Always try again.

Transcend.
 
Asante mkuu....muhimu kujaribu bila kukata tamaa...
 
1922 - Julius Kambarage Nyerere anazaliwa.

Ni mwasisi na Rais wa kwanza wa Tanzania.

Aliipatia nchi hiyo Uhuru mwaka 1961 kabla ya kuwa Rais mpaka mwaka 1985 alipoamua kung'atuka na kumuachia nchi Ali Hassan Mwinyi.

Anajulikana kama " Baba wa Taifa " au Mwalimu Nyerere kutokana na kazi yake ya kufundisha aliyoifanya kabla ya kuwa Mwanasiasa.

Licha ya kustaafu mwaka 1985 bado aliendelea kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania na Afrika kwa ujumla mpaka pale alipofariki mwaka 1999 jijini London alipoenda kwa matibabu.

Kama angelikuwa hai, leo angekuwa anatimiza miaka 95 ya kuzaliwa.
 
1978 - Carles Puyol anazaliwa.

Beki na nahodha wa zamani wa Barca na timu ya taifa ya Hispania.

Alikuwa ni sehemu ya kikosi cha Barca na Spain kilichotikisa soka la Dunia kuanzia mwaka 2008 - 2102 ambapo alitwaa Kombe La Dunia, Kombe la mataifa ya ulaya, ligi ya mabingwa ulaya nk

Mmoja kati ya wachezaji wanaocheza jihadi sana.
 
Nukuu imetulia
.....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…