Siku hizi watu kusingizia mimba ili wapate vitu vingine mf. hongera, sympathy, off kazini na mengineyo ni jambo la kawaida. Kuna binti mmoja yeye aliwapiga adoption agency kuwa ana mimba na mtoto atamtoa awe adopted, na familia ikapatikana wakawa wanamtunza kwa kumnunulia vyakula organic ale vizuri, wanamnunulia prenatals, wanamlipia mpaka kodi ya nyumba kumbe porojo tu. Zikifika siku za kwenda kwa daktari kupiga ultrasound binti visingizio kibao. Ndiyo baadaye ikajulikana kumbe ilikuwa mimba hewa na sasa kesi inaunguruma mahakamani. Mjini hapa mkuu be careful unaweza kutapeliwa hata emotionally