Makapuku Forum

1921 - Moacir Barbosa Nascimento anazaliwa.

Golikipa wa zamani wa Vasco Da Gama na timu ya taifa ya Brazil.

Analaumiwa kwa kufanya makosa yaliyopelekea Brazil kupoteza mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 1950 katika ardhi ya nyumbani kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Uruguay katika uwanja wa Maracana.

Goli la pili liligungwa na Uruguay liliyokana na kipa huyu kuzembea kukaa katika eneo sahihi hivyo kuruhusu kupoteza ubingwa huo licha ya Brazil kupewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo.

Mashabiki wa soka wa Brazil hawakuwahi kumsameje Barbosa na daima walimtenga katika shuguli za kijamii kitu kilichomtesa sana kisaikolojia.
 
Amen ubarikiwe
 
1974 - Gaizka Mandieta anazaliwa.

Kiungo wa zamani wa Valencia, Lazio, Barcelona, Middlesbrough na timu ya taifa ya Spain.

Alikuwepo kwenye kikosi cha Valencia kilichoingia fainali mbili mfululizo za Uefa Champions League na kupoteza fainali zote.

Fainali ya kwanza walipoteza dhidi ya Real Madrid mwaka 2000 na Fainali ya pili mwaka 2001 dhidi ya Bayern Munich.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…