Makapuku Forum

Makapuku Forum

f4d256c4537d7ced0475d2ec0bb24e5c.jpg
da9df397a7f1e427d496b2f18ad202f7.jpg
9d5f6e912c18105151662f4e131bf61e.jpg

Aliniboa alipokubali serikali ya mseto wakati uchaguzi alishinda halafu akafanyiwa figisu
Waafrika hatujitambui
...
Kuwa kiongozi mzuri na kudumu katika siasa HASA HIZI ZA AFRIKA ni pamoja na kusoma alama za nyakati na kujishabihisha nazo. Ukiwa ngangari sana wakati mwingine unaweza kupoteza uoni hata ukasahau lengo halisi la harakati zako. Mfano mzuri ni Savimbi. Alipewa umakamu wa rais akakubali lakini baadaye akageuza gia angani akaamua kurejea msituni kupigana. Kumbe upepo ukawa umebadilika na wafadhili wake wa Kimarekani wakawa hawana umuhimu naye tena kwa sababu tayari Do Santos alikuwa amekubali kuwauzia mafuta Wamarekani na vuguvugu la vita baridi lilikuwa limekwisha. Matokeo yake akaishia kuuawa na kuzikwa kama mbwa, na leo hii yupo huko anajiozea katika shimo la historia.

Hata huyu naye angeendelea kuwa ngangari si ajabu angeishia kuuawa au kukimbilia uhamishoni. Alifanya vyema kuchukua uwaziri mkuu na nadhani lengo lake ni kuwasha moto wa kiharakati tena baada ya Mugabe ku-RIP. Tatizo, kama ilivyo kawaida ya viongozi wengi wa Afrika, naye tayari anatajwa katika kashfa kadhaa za ufisadi mzito. Keshashiba sasa na si ajabu akaachana na siasa jumla. Mianasiasa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom