Makapuku Forum

1971 - Pambano baina ya Joe Frazier dhidi ya Muhamad Ali lafanyika huko Madison Square.

Pambano hilo lililopachikwa jina la " Fight of the Century " liliwakutanisha mabondia ambao hapo awali hawakuwa wamepoteza mapambano yoyote.

Mohamed Ali alipoteza pambano hilo baada ya raundi 15 za kukata na shoka.

Inasemekana hakuna pambano la ngumi lilikuwa kali na la kuvutia zaidi ya hili.

Hata waliporudiana katika pambano lililojulikana kama " Thrilla in Manilla " ambapo Ali alishinda bado pambano hili halikufua dafu kwa lile la kwanza.
 
1990 - Asier Illarramendi anazaliwa.

Kiungo mkabaji wa zamani wa Real Madrid ambaye kwasasa anakipiga Real Sociedad na timu ya taifa ya Hispania.

Ndio mchezaji mdogo wa Hispania kununuliwa kwa kiasi kikubwa cha pesa na Real Madrid akitokea Real Sociedad kabla ya kuchemsha vibaya na kurudi tena Real Sociedad.

Alifananishwa na mkali wa zamani wa Real Madrid, Xabu Alonso kwa aina yake ya uchezaji.

Alitwaa Uefa Champions League akiwa Real Madrid mwaka 2013/2014.
 

Siku hizi kuna ngumi laini laini
.....
 
- Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Ni siku inayoadhimishwa Dunia nzima, kupinga ukatili na unyanyasaji wa Wanawake.

Ilianzia Urusi baada ya Wanawake wa Urusi kuchoshwa na unyanyasaji dhidi yao huko Viwandani , hali iliyopelekea kuanza migomo na maandamano ili kutetea haki zao.

Harakati hizo zilipelekea kutokea kwa Mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…