Makapuku Forum

1994 - Wakala wa CIA, Aldrich Ames na Mkewe wanashtakiwa na Serikali ya Marekani kwa kosa la kukubali kuuza siri za Nchi hiyo na kufanya kazi shirika la Ujasusi la Urusi KGB.

Aldrich Ames baada ya miaka 31 ya utumishi wake ndani ya CIA alijikuta akiwa " Double Agent " wa KGB jambo ambalo ni kosa la jinai.

Kwasasa anatumikia kifungo cha Maisha katika gereza lenye ulinzi mkali la Allenwood.
 
1921 - Jean Bedel Bokassa anazaliwa.

Kiongozi wa zamani wa Afrika ya kati ambapo alikuwa ni Rais wa Pili wa Nchi hiyo.

Alikuwa ni dikteta aliyejitangazia Urais wa Maisha katika Nchi hiyo.

Alipinduliwa mwaka 1979 kwa msaada wa Majeshi ya Ufaransa.

Alifariki mwaka 1996.
 
1932 - Ted Kennedy anazaliwa.

Alikuwa ni seneta wa Massachusetts. Alishikilia wadhifa wa useneta kwa miaka 47.

Alikuwa ni mdogo wake Rais wa zamani wa Marekani John F. Kennedy.

Alifariki mwaka 2009 akishikilia rekodi ya seneta wa 4 kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…