Makapuku Forum

Unakumbuka lile gori alilofungwa bathez kipindi kile cha club bingwa ya Dunia
 
Siku hizi símşikii kàbisà
Katika kazi yo yote bila nidhamu na kujituma huwezi kufika mbali. Japo ana pesa za kutosha (kama alizitumia vizuri) alilewa sifa mapema akapoteza moyo wa kujituma. Tunawaonea wivu wanamichezo hawa kutokana na pesa nyingi wanazolipwa lakini ili kufanikiwa inabidi uwe na nidhamu ya hali ya juu na work ethic nzuri. Ni maisha ya kufanya mazoezi kila siku na ukizembea kidogo tu watu wanachukua nafasi yako.

Kwa sasa nadhani yupo (D)evelopmental League akijaribu tena kuonyesha kama anafaa kwenye real league (NBA). Tatizo ni kwamba wachezaji wengi wanaoshushwa kwenye D league, ni chini ya asilimia moja ndo huweza kurudi tena kwenye NBA. Na umri wa kimichezo nadhani utakuwa kidogo umeenda (ukivuka 25 au 30 kulingana na kipaji chako na level ya fitness basi unahesabiwa kuwa umeanza kuzeeka). Yote kwa yote dogo alitutangaza vizuri mpaka na Kiswahili akakisahau na kuanza kuongea kama nigga kutoka ghetto za Baltimore!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…