Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo katika Historia:

1916 - Samuel Goldwyn na Edgar Selwyn wanaanzisha kampuni ya kurekodi filamu ya Goldwyn Pictures.

Kampuni hiyo maarufu baadae ilikuja kujulikana kama Metro- Goldwyn- Meyer ( MGM ).
 
1946 - Nchi za Sweden, Iceland na Afghanstan zajiunga na Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa ulianzishwa mapema tu baada ya kumalizika kwa vita kuu ya pili ya Dunia, ukiwa na jukumu la kusimamia amani na usalama Duniani.
 
1946 - Nchi za Sweden, Iceland na Afghanstan zajiunga na Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa ulianzishwa mapema tu baada ya kumalizika kwa vita kuu ya pili ya Dunia, ukiwa na jukumu la kusimamia amani na usalama Duniani.
 
1950 - Jenerali Dwight D. Eisenhower wa Jeshi la Marekani anachaguliwa kuwa Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Nato huko Ulaya. Kabla ya Uteuzi huo, alikuwa ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani.

Jenerali Eisenhower anafanya kazi nzuri katika majukumu yake hayo ndani ya Nato hali iliyopelekea baadae kuja kuwa Rais wa Marekani.
 
1969 - Edson Arantes Dos Nascimento " Pele " anafunga goki lake la 1000 toka aanze kucheza soka.

Pele staa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil anatajwa kama mchezaji bora wa wakati wote na anashikilia rekodi mbalimbali ikiwemo;

• Kufunga magoli 1000 katika career yake ya kucheza soka.

•Kuchukua Kombe la Dunia akiwa ndio mchezaji mwenye Umri mdogo zaidi wa miaka 17.

•Mchezaji pekee kuchukua kombe la Dunia mara tatu, mwaka 1958 pale Sweden, 1962 pale Chile na mwaka 1970 pale Mexico.
 
1933 - Larry King anazaliwa.

Ni mwandishi mashuhuri na mkongwe anayefanya kazi katika kituo cha CNN huko Marekani.

Moja kati ya vipindi vyake ni Larry King Live.
844ab16bcaaa42464eb4371e739ac6c2.jpg
abb806e0af2c778b8b55c189e68a2213.jpg
 
1965 - Laurent Blanc anazaliwa.

Beki wa zamani wa Barcelona, Inter Milan, Man Utd na timu ya taifa ya Ufaransa.

Alitwaa kombe la Dunia mwaka 1998 na Kombe la Ulaya mwaka 2000 akiwa na kikosi cha dhahabu cha Ufaransa kilichoingozwa na fundi Zidane. Aliunda safu kali ya ulinzi akiwa na Marcel Desailly na Bixente Lizarazu.

Alikuwa na kipara, kabla ya mechi kipa Fabien Barthez alikuwa lazima akibusu kipara cha Blanc.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom