Makapuku Forum

 
1979 - Pablo Aimar anazaliwa.

Staa wa zamani wa River Plate, Valencia, Zaragoza na timu ya taifa ya Argentina.

Wakati anachipukia alitajwa kama Diego Maradona mpya kutokana na uwezo wake mkubwa wa ku-dribble mpira, kumiliki na kutoa pasi zenye macho.

Moja kati ya Wachezaji walioshindwa kufikia matarajio ya vipaji vyao kando ya nyota wengine kama Javier Saviola, Ricardo Quaresma, Joe Cole n.k.
 
1996 - Jean Bedel Bokassa anafariki.

Alikuwa ni Rais wa pili wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Alijiita Rais wa Maisha. Pia alikuwa ni Jenerali katika Jeshi la Nchi hiyo.

Moja kati ya Marais waliotawala kibabe na wenye utata mkubwa.

Inasemekana alikuwa anakula nyama za watu, japo hakuna uthibitisho rasmi.
 
 
Alikuwa tajiri wa kutupwa!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…