Makapuku Forum

Makapuku Forum

1930 - Mobutu Sese Seko anazaliwa.

Alikuwa ni Rais na Dikteta wa zamani wa Zaire, kwa sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Anatajwa kama Bilionea wa kwanza Mweusi Ulimwenguni.

Alishiriki katika kukamatwa kuuwawa kwa Waziri Mkuu wa wakati huo, Payrice Lumumba.

Alipinduliwa mwaka 1997 na kukimbilia uhamishoni kabla kufariki huko Morocco na kuzikwa hukohuko.
 
1943 - Wafungwa katika gereza la Kijerumani la Sobibor huko nchini Poland waanzisha mgomo na kujaribu kutoroka.

Wafungwa 300 katibya 600 wanafanikiwa kutoroka na kuua askari 11 wa Gereza hilo.

Gereza la Sobibor ni moja ya magereza ya Siri yaliyokuwa yanamilikiwa na Serikali katili ya Dikteta Hitler.
Bora
 
1943 - Jose P. Laurel anaapishwa kuwa Rais wa Philipines.
5b7d15ea2102a5b1b15d4cde44e67c3b.jpg
2fc96dacd46cc92f3da38c86064bc0a6.jpg
IMG_20161014_090407.jpeg
 
1944 - Field Marshal Erwin Rommel katika Jeshi la Nazi la Ujerumani analazimishwa ajiue mwenyewe baada ya kuhusika kula njama za kutaka kumuua Kiongozi wa Nchi hiyo Adolf Hitler.

Baada ya kukiri kuhusika kwake, Hitler anamwambia Rommel ajiue mwenyewe ili kulinda heshima yake kutokana na mchango wake katika Taifa hilo.

Rommel anajiua na inatangazwa kuwa alikufa kwa ajali ya gari na anazikwa mazishi ya kitaifa kwa kupewa heshima zote.
Duuh hii kali
 
1968 - Matthew Le Tissier anazaliwa.

Ni gwiji wa mpira wa klabu ya Southampton unayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Pamoja na uhodari wake wote wa kufunga magoli akiwa na klabu ya Southampton hakuwahi kuchezea timu ya taifa ya England.

Mashabiki wake humuita jina la utani " Le God "
 
1944 - Field Marshal Erwin Rommel katika Jeshi la Nazi la Ujerumani analazimishwa ajiue mwenyewe baada ya kuhusika kula njama za kutaka kumuua Kiongozi wa Nchi hiyo Adolf Hitler.

Baada ya kukiri kuhusika kwake, Hitler anamwambia Rommel ajiue mwenyewe ili kulinda heshima yake kutokana na mchango wake katika Taifa hilo.

Rommel anajiua na inatangazwa kuwa alikufa kwa ajali ya gari na anazikwa mazishi ya kitaifa kwa kupewa heshima zote.
Screenshot_2016-10-14-09-09-17.png
064a85ea119e42753cb3112249212dca.jpg

Alijiuaje?
..........
 
1944 - Field Marshal Erwin Rommel katika Jeshi la Nazi la Ujerumani analazimishwa ajiue mwenyewe baada ya kuhusika kula njama za kutaka kumuua Kiongozi wa Nchi hiyo Adolf Hitler.

Baada ya kukiri kuhusika kwake, Hitler anamwambia Rommel ajiue mwenyewe ili kulinda heshima yake kutokana na mchango wake katika Taifa hilo.

Rommel anajiua na inatangazwa kuwa alikufa kwa ajali ya gari na anazikwa mazishi ya kitaifa kwa kupewa heshima zote.
Aisee, hiyo adhabu ni balaa
 
Back
Top Bottom