Makapuku Forum

Leo katika Historia Orijino:

1946 - Baraza la Ulaya ( The Council Of Europe ) Laanzishwa rasmi mara baada ya Hotuba maarufu ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill.

Churchill alikuwa ni Kiongozi mwenye ushawishi Mkubwa sana sio tu Uingereza na Ulaya bali hadi Amerika na wala haishangazi alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu kwa mara ya pili katika kipindi tofauti.

Huko Marekani alipewa Uraia wa heshima miongoni mwa watu 8 pekee kuwahi kupewa Uraia wa heshima wa Nchi hiyo.

Kwa kutambua mchango wako, alipofariki Dunia akiwa ameshastaafu siasa, Malkia Elizabeth wa Pili alimpa heshima ya Mazishi ya Kitaifa ambapo yalihudhuliwa na Idadi kubwa ya viongozi mbalimbali Duniani.
 
1952 - Marekani yamzuia Mchekeshaji maarufu, Charlie Chaplin kuingia nchini mwao baada ya safari yake ya Uingereza.

Charlie Chaplin anabaki mmoja kati ya wachekeshaji bora wa wakati wote kuwahi kutokea katika Tasnia ya Uchekeshaji.
 
1985 - Tetemeko kubwa kabisa kuwahi kutokea Amerika ya Kaskazini laikumba Nchi ya Mexico na kuua Maelfu ya watu na Majengo takribani 400 yalidondoka.

Cha kushangaza, Tetemeko hilo liliharibu hospitali moja nchini humo, lakini katika wodi ya akina mama waliojifungua lilifika lakini halikuleta madhara kwa watoto wachanga waliokuwa katika wodi ile. Watoto zaidi ya 100 wote walipona bila ya kudhurika.
 

Usalama kwanza
........
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…