HII IMEKULA KWANGU;
Nilipata oda ya kutengeneza T-shirt za kikundi fulani cha kuzikana, pale Tanga Mjini.._
Nimewatumia jana kulingana na idadi yao, muda huu nimepigiwa simu kuwa hawataki hata kuziskia, licha ya kuziona

! ingawa NI za Ukweli sana
Niliwachagulia 'Black Colour' ili iendane na rangi za Msiba kimazoea, ni fulana Kali nyeusi zenye maandishi safi meupe yanayosomeka:
Umoja wa Kuzikana Tanga sasa shida iko wapi hapo?
ila chini kidogo ya maandishi hayo nili abbreviate kwa maandishi ya herufi kubwa kidogo;
UKUTA
Wamedai hilo ndo tatizo, nimewashauri, niongeze 'M' iwe UKUTAM nikimaanisha
Umoja wa Kuzikana Tanga Mjini wamechomoa, wanadai hapo ndo nitaharibu kabisa, eti itatafsirika kama _"UKUTA Mgumu"
Ushauri Wenu Tafadhali