Makapuku Forum

NUKUU NO 1#

Watu na haki ni misingi ya Uongozi ambayo haiachani
Nikisema hivyo siyo kwamba kiongozi asiyechaguliwa na watu hawezi akatenda yaliyo ya haki. Anaweza. Maana yangu ni kwamba walinzi wa haki za watu ni watu wenyewe

Wanaweza wakapata viongozi wazuri, na hiyo itakuwa bahati yao. Lakini wakipata viongozi wabaya watakuwa na bahati mbaya sana, kwa sababu watakuwa hawana dawa ya kuwaondoa.

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,
Yamo katika kitabu chake kinachoitwa TANU NA RAIA alichoandika mwaka 1962.

Mwalimu alig'atuka urais mwaka 1985. Alifariki Dunia Oct 14,1999
 
 
NUKUU NO 2#
Umoja wetu haupaswi kuangalia pande gani ya Dunia, mipaka au utaifa bali tufungamane tushikamane kutoka pande zote za Dunia na katika kila nchi

Maneno haya ya kuhamasisha yalitamkwa na mpigania haki za weusi wa zamani wa Jamaica, Marcus Garvey.
Yamo katika andiko lake linaloitwa African Fundamentalism kwenye gazeti la kale la Negro World.

Garvey alikuwa akihubiri dhana ya weusi wote Duniani kuwa na nchi Yao moja au Bara lao moja ili wawe na fursa ya kuonesha kuwa Wana akili na vipawa sawa na wazungu.

Alizaliwa mwaka 1887 Jamaica na kufariki Dunia mwaka 1940 London
 
Apumzike kwa amani..inaonyesha jamaa alikuwa brave sana huyu
 
 
R.I.P our braviest prezidaa...sio wengine uchwara tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…