Makapuku Forum

SEHEMU YA MWISHO
“Karibu sana Kalebbe,” Zulekha akamkaribisha Amata huku akimsubiri ateremke katika boti. Kwa mwendo wa taratibu walitembea katika mchanga mweupe wa pwani ya kisiwa hicho na kufika kwenye kijumba kidogo tungekiita kibanda. Zulekha akaweka kiganja chake cha mkono wa kulia katika kitu kama kioo kilichokuwa mlangoni hapo, kisha akasogeza zura yake, mwanga mwekundu ukapita kati ya macho yake, akatamka jina lake na kisha kubofya tarakimu Fulani Fulani ule mlango ukafunguka, wakaingia wote wane na ule mlango ukajifunga nyuma yake.
Ngazi ndefu ilionekana kuteremka chini wakaifuata na walipofika chini kama mita ishirini hivi, kulikuwa na njia pacha tatu. Zulekha akasimama.
“Ukienda kushoto, unaenda kwenye nyumba ya mzee, kulia unaenda kwenye idara ya usalama na sisi tunakwenda moja kwa moja,” akamwambia kisha akaongoza njia ile na Amata akamfuata.
Wakatokea kwenye jumba kubwa la kifahari, lenye kila samani inayostahili kuitwa ‘samani ya ndani’. Kamanda Amata aliitazama ile sebule ya kifahari, iliyozungukwa na kuta za aina yake huku upande mmoja kukiwa na ukuta wa kioo unaoruhusu kuona mandhari ya chini ya maji.
“Kinywaji tafadhali,” mwanadada mrembo wa kadiri ya miaka ishirini na tano hivi alimkaribisha kinywaji cha matunda kilichojaa kwenye bilauri.
“Asante sana mrembo, sharubati tu au kuna kingine?” akauliza huku akia kamshika.
“Oh, sio hivyo, mgeni hawezi kuwa mwenyeji namna hiyo,” Zulekha alimwambia Amata huku akimwondoa Yule binti katika himaya yake.
“Sasa jumba kama hilo umewezaje kulijenga hapa?” Amata akauliza.
“Kawaida tu, mafundi kutoka Japan waliifanya kazi hii mchana na usiku baada ya kupata matatizo katika nyumba yetu ya Kerege,” Zulekha akaeleza.
“We na nani?”
“Mi’ na mume wangu Premji Kanoon, utamwona muda si mrefu kwani ametoka kwa kuwa kesho tunatarajia kuondoka,” Zulekha akajibu kwa ufasaha huku Amata akitikisa kichwa na saa yake ikifanya kazi ya kurekodi.
“Unaonekana ni kijana mtulivu, mdadisi, unayependa kujua mambo…”
“Na lingine umelisahau, napenda warembo kama wewe,” Amata akamalizia kusema.
“Warembo ni sumu, watakupeleka pabaya,” Zulekha akamwambia huku akiketi kitini na sigara yake kinywani.
“Mr….. Spark! Pale Oceanic Breeze umefika lini?”
“Nimefika siku tano zilizopita,” akajibu.
“Wewe unafanya kazi gani maana una maswali kama mpelelezi,” Zulekha akazidi kusaili.
“Mimi ni mwandishi wa habari, huwa naandika habari za mazingira na uchunguzi,” akajibu jibu la uongo kabisa.
“Aaaaa ha ha ha haspo nitakubaliana na wewe, sasa Bagamoyo kuna habari gani iliyokuleta?” Zulekha aliketi sawia katika kaiti chake akimtazama mwanadada huyo.
“Inasemekana kuna ndege ndogo imepotea upande huu wa Bagamoyo hiyo sasa ndiyo iliyonileta kuandika hiyo juu ya hilo tukio,”
“Unashirikiana nani?”
“Mimi kutoka shirika la habari la Afrika Mashariki, lakini wapo wengine kutoka idara mbalimbali za serikali,” Amata akaeleza.
“Oh, good kazi nzuri sana,” Zulekha akamwambia Amata na wakati huohuo simu ya ukutani ikaita, akanyanyuka na kuiendea akaipokea.
“…Ndiyo, sasa hivi?... ok!” akaitazama saa kubwa ya ukutani ilikuwa ikimwambia kuwa muda huo ilikuwa ni saa kumi na moja jioni. Akarudi pale mezani na kumalizia kinywaji chake.
“Mume wangu karibu anaingia, unapenda kuungana nami kumlaki?” Zulekha akamwambia Amata.
“Ya, bila shaka,” akajibu.
Wote wawili wakaongozana mpaka nje kwa upande wa pili wa kisiwa hicho, pale walikuta wanaume watatu walionyoa ndevu zao kama Rick Ross, kutokana na ukimya wao naye hakuwasalimia, bali aliungana na Zulekha kutulia kusubiri.
Helkopta moja kubwa ya kifahari iliteremka katika pwani hiyo iliyojengwa kinamna, n ilipozima injini yake, mtu tajiri aliyekuwemo ndani ya chombo hicho akateremka pamoja na watu wengine wawili ambao moja kwa moja Kamanda Amata aliwatambua kwa kuwa ni watu wa juu serikalini. Pancho alipogongana macho na Amata akatamani kuanguka lakini akajikaza kisabuni. Zulekha akamwendea na kumkumbatia kisha akambusu.
“Mgeni, nimekutana naye Ocean Breeze nikamkaribisha nyumbani, ana manufaa sana kwetu kwa mazungumzo mafupi niliyozungumza naye, anaitwa Mr. Spark,” Zulekha akatambulisha kisha akageukia kwa Amata.
“Kutana na mume wangu mpenzi Mr. Premji Kanoon,” akamalizia. Pancho alikutana macho yake nay ale ya Amata ambayo yalifichwa kwenye miwani ya rangi ya udongo, miwani iliyokuwa ikirekodi video matukio yote hayo ambayo yalikuwa yakitukia mbele yake.
“Karibu sana, jisikie nyumbani,” Pancho akamkaribisha Amata, pale alipotaka kupewa mkono alijifanya kutokuona akapita na kisha wengine wakafuatia nyuma yake. Kichwa cha Pancho kilianza kuchanganyikiwa kwa kumwona mtu huyo hatari kwa maisha yake akiwa hapo, hakuelewa kama Zulekha kamleta hapo kwa nia ya kuwa kamteka au ndiyo amelaghaiwa kwa mapenzi, lilikuwa swali lisilo na jibu.
“Naomba niacheni peke yangu kisha mniitie Zulekha nahitaji kupumzika kidogo,” Pancho akwaambia vijana wake na wale wageni, wakaondoka eneo lile.
† † †
“Unamjua mgeni uliyemleta humu ndani ni nani?” Pancho alimuuliza Zulekha.
“Ni mwandishi wa habari aliyevutiwa sana na hiki kisiwa, nikaona nimkaribishe kama fursa ya kujitangaza. Na ni wewe mwenye we uliniambia hayo,” Zulekha akajibu.
Kofi moja la kulia lilitua shavuni mwake akadondokea kitandani.
“Huna akili mwanamke! Huna akili kabisa, unaweza kuleta mashetani ndani ya nyumba hii, we hujiulizi kwa nini nyumba hii imejengwa chini ya ardhi?” Pancho akang’aka.
“Sasa mimi kosa langu nini?” Zulekha akaamka kitandani na kupiga kelele huku akiuliza, hasira zikamshika mishipa ikamtoka.
“Wewe mwenye we ndiye uliyeniambia hayo leo hii unanigeuka? Nimepigiwa simu na Nassoro kijana wako mtiifu wa Ocean Breeze nikaenda na bahati nakutana na mtu huyu kwa nini nisimlete nyumbani ili aone kwa macho kila anachotaka, mara ngapi wewe umewaleta watu humu ndani na kunitambulisha kuwa ni watalii na wafanyabisahara?”
“Naona unanipanda kichwani sasa sivyo?” Pancho akachomoa bastola na kumwoneshea Zulekha.
“Nenda kwa huyo mgeni wako kamwulize yeye ni nani akwambie kisha uniletete jibu haraka!!!”
Zulekha akatoka chumbani na kumwacha pancho akiwa kafura kwa hasira, akapita kwenye korido ndefu na kuingia katika sebule kubwa ambako mwanzo aliketi na Amata, hakumkuta, isipokuwa kijana mmoja aliyekuwa akiangalia usalama wa eneo lile.
Kamanda Amata alikuwa kasimama mbele ya dirisha moja kubwa sana akitazama nje na shughuli mbalimbali zinazoendelea za wafanyakazi wa himaya hiyo.
“Mr. Spark!” akaita. Amata akageuka na kumwendea pale aliposimama, Zulekha hakusema lolote, akainua chupa ya wine na kumimina kwenye bilauri iliyokuwa juu ya stuli na kumpa Amata kisha akainua nyingine na kujimiminia yeye.
“Wewe ni nani?” akauliza huku akionekana wazi sura yake kubadilika.
“Nimekwisha jitambulisha kwako ya kuwa mimi ni nani, bado unataka zaidi? Basi mwambie aliyekutuma akwambie mimi ni nani,” kisha akainyosha juu ile bilauri yake na kuinywa mfululizo.
“Naitwa, Amata, Kamanda Amata, Tanzania Secret Agency nambari moja; una lingine?” akamweleza mara tu baada ya kuiweka bilauri yake mezani. Na nukta hiyohiyo, alipojikuta amezungukwa na vijana wenye silaha kile upande. Aligeuka huku na huku na kukutana na sura zilizokunjamana kwa uchu wa kuua.
“Mikono juu tafadhali,” akaamriwa na ye akatii.
Kijana mwingine akampekua na kutoa bastola mbili ndogo mifukoni mwake, vizu vidogo vitatu na vitambulisho vingine vingine ikiwamo kadi za benki na kadhalika.
“Unaniambi wewe ni mwandishi wa habari kumbe ni jasusi?” Zulekha akamwuliza kisha akamnasa kofi na kusogea pembeni. Amata alivumilia maumivu huku akimtazama Zulekha kwa jicho baya sana, ‘utalipa tu,’ akajisemea moyoni. Pancho Panchilio akaingia sebuleni pale na kumkuta Amata akiwa chini ya ulinzi mkali.
“Ha! Ha! Ha! Ha! Amataaaa, leo umejileta mwenye we kwenye nyumba ya shetani. Uroho wako wa mapenzi ya wanawake umekukamatisha, huna maana kabisa, nashindwa kujua kwa nini serikali ikakuamini hata kukupa hicho cheo wakati wewe ni mpumbavu kati ya wapumbavu wa nchi hii! Karibu sana Kalebee, maada ulitaka kuja kupaona kama nilivyoelezwa na mke wangu Zulekha basi ngoja nikutembeze kidogo ili ufahamu mahali hapa. Pancho alimtembeza Amata huku vijana wake wakilinda msafara huo kwa bunduki nzito kila kona ya jingo hilo. Kila kitengo alimwonesha bila kumficha na kumwelezea lakini hakumruhusu kuuliza swali. Baada ya kuzunguka ndani ya jengo lote hilo wakasimama mbele ya mlango mmoja wa chuma.
“Kamanda Amata, na sasa nataka nikuoneshe kitengo hiki ambacho kila anayeingia lazima achnganyikiwe ka teknolojia iliyofungwa ndani yake,” aliposema hayo akabofya kitufe Fulani na lile lango likafunguka. Kilikuwa chumba tupu, hakukuwa na chochote ndani yake. Pancho akaingia ndani yake.
“Karibu ushuhudie kilichomo, usiogope,” Pancho alimwambia. Kengele za hatari zikalia kichwani mwa Amata, akaingia ndani ya kile chumba kipweke, nyuma yake wakaingia vijana wawili walioshiba kimazoezi. Kwenye maeneo kama haya huwa Amata hana subira zaidi ya kupigania uhai wake tu japo kwa sekunde ya mwisho. Alivuta hatua mbili mbele na kugeuka ghafla, akamchapa konde moja mmoja wa wale jamaa waliongia nyuma yake. Yule jamaa akayumba kidogo kwa kuwa hakutegemea dhopruba kama ile. Yule wa pili akaudaka mkono wa Amata lakini kabla hajafanya lolote, alipigwa kichwa kizito na kwenda chini. Kamanda Amata akruka hewani na kutawanya miguu yake, akawachapa mateke makali kila mmoja akaenda chini bila kipingamizi. Alipotua Amata akaruka sarakasi ya chini kwa chini na guu lake likatua katika koromeo la mmoja wao, akaguna kwa uchungu. Alipojigeuza alijikuta anatazamana na mtutu wa AK 47, akajizungusha na kumtia ngwala aliyeshika hiyo bunduki, akaenda chini huku bunduki ile ikimtoka mikononi, akaiwahi na kuikamata, bila huruma aliwatwanga wote wane wa kirasi na kuwaacha marehemu. Mlangoni hakukuwa na mtu, ‘uko wapi mwanaharamu?’ akajiuliza na kuchungulia kupitia ule mlango, nakasikia watu wanaoongea wakija upande huo, akarudi ndani na kujificha nyuma ya mlango akisubiei huku mkononi mwake akiwa kaikamatia ile AK 47 aliyoichukua kwa Yule jamaa.
“Ni hapa jamani, ingieni kwa makini,” sauti moja ikasema.
Kamanda Amata akaendelea kutulia palepale, wale jamaa wakamwingiza mmoja kama chambo, akaangaza angaza huku na huko akiazngalia maiti za wale jamaa watatu pale chini.
“Huyu jamaa hayupo bwana,” akawaambia wenzake.
“Basi msako uanze atakuwa humuhumu ndani, kumbuka hawezi kutoroka hapa ni kisiwani,” mwingine akahimiza huku wakitoka mle ndani na kupotelea huku na huko. Amata akatoka taratibu na kufuata korido moja kwa moja mpaka kwenye ile njia panda waliyopita na Zulekha wakati wakiingia kwenye jumba hilo. Akakunja kushoto na kuufikia mlango imara wa chuma, akajaribu kuufungua kwa kutmia zile namba alizozikariri pindi alipomwona Zulekha akifungua zikakubali lakini akadaiwa alama za vidole, akashindwa. Akatafakari cha kufanya akakosa jibu. Alipokuwa akijiandaa kubadilisha mbinu akasikia michakacho ya mtui anayetembea haraka haraka huku akiongea.
“Kawaua wote, wote watatu, huyu jamaa hafai, inabidi auawawe,” Yule mtu alionekana anaongea na kitu kama simu ya upepo. Amata akamvizia, alipotokezea tu eneo lile, akaruka na kutua shingoni mwake, akamkaba kabala ya maana.
“Tulia,” akamwambia. Ile redio pale chini ikawa inaendelea kuita,
“Jota! Jota! Umepatwa na nini?” sauti ya upande wa pii ikauliza. Kamanda Amata akaitazama ile redio na kuivuta kwa mguu wake.
“Fungua mlango!” akamwambia Yule jamaa ambaye sasa alimfahamu kwa jina la Jota.
“Mi sijui, “ akajibu kwa shida kutokana na ile kabala aliyopigwa na Amata, akamwachia na kumsukumizia mlangoni.
“Fungua,” Amata alimwambia huku AK 47 ikimtazama mtu huyo, akapapasa namaba hii na ile na kuweka alama zake za vidole kisha macho, mlango ukafunguka. Kamanda Amata akamrukia teke la kusukuma Yule jamaa akaangukia ndani, kisha yeye akafuata na kufyatua risasi zilizowaangusha watu wawili na kumwacga mmoja tena wa kike akiwa kasimama.
“Kamanda Amata,” Zulekha akaita.
“Umeniharibia ndoa yangu,” akaongeza kusema.
“Nioneshe mumeo, serikali inamtafuta kwa udi na uvumba,” Amata akamwambia.
“Wewe ni mbaya sana sivyo nilivyofikiria,” Zulekha akaongea huku chozi likimtoka.
“Nilitaka nifike hapa na sasa ninavyokwambi, namhitaji mumeo, Pancho Panchilio na sio Premji Kanoon kama unavyomjua. Jasusi aliyefunzwa na KGB, ametoroka mikono ya serikali kibabe, sasa siku zake zimekwisha. Nioneshe alipo kabla na wewe ssijakumaliza,” Amata aliongea huku akiwa kakunja sura kwa hasira.
“Sasa mbona unakunja sura namna hiyo, kijana mzuri hatakiwi kujizeesha mwili wake,” Zulekha alisema hayo huku akimfuata taratibu.
“Tulia hivyohivyo kabla sijakuua kwa bastola yako mwenyewe,” sauti ikasikika kutoka nyuma yake. Kutokea katika dorosha kubwa lililokuwa mbele yake aliweza kumwona mtu Yule vizuri sana. Amata hakuwa na muda wa kupoteza katika eneo hilo ambalo lingeyagharimu maisha yake muda wowote. Aligeuka na kumtandika Yule jamaa kwa kitako cha bunduki, akaaangukia juu ya meza huku bastola ikimtoka mikononi, Amata akachumpa kwa ustadi na kuinyakuwa huku mkono mwingine akiwa tayari na saa yake ya mkono ambayo bwana huyo aliichukua pamoja na bastola. Yule bwana akaamka na kusimama wima huku mbele akimtazama Amata aliyekuwa akiibonya ile saa hapa na pale.
“Mnaweza kuja sasa, kazi imeanza,” akaongea huku akiitazama ile saa kisha akaivaa mkononi mwake. Yule mjinga akatumia muda huohuo, akaruka tik tak kwa minajiri mguu yake ipige mikono na kidevu cha Amata lakini akakuta anapiga hewa kwani mwenzake alikwishaondoka eneo hilo na kutua upande mwingine mpaka kwa Zulekha aliyekuwa amebaki kaduwaa. Yule bwana alipotu na kukuta Amata hayupo, akajivuta kasi kumwendea, akaruka hewani akiitanguliza miguu yake mbele. Amata akaepa na kumpa pigo moja la karate mbavuni na kuvunja ubavu mmoja, Yule bwana akajibwaga chini kwa maumivu alipojaribu kusimama alikutana na teke linguine katika ubavu wake wa pili, akaanguka chali na guu la Amata likatua kifuani mwake kwa kishindo.
“Aaaaaaiiiggghhh!!!” Yule jamaa akapiga yowe la maumivu huku akijaribu kwa nguvu zote kuuondoa mguu ule lakini alishindwa.
“Boss wako yuko wapi?” akamuuliza.
Akiwa katika kumuuliza akajikuta akahisi kitu kizito kikikifikia kisogo chake, akageuka haraka na kutua upande wa pili wa Yule mtu huku tayari mkono bastola yake imetulia, alipocheza na kifyatulio, kijana mmoja aliyekuwa na chuma kizito mikononi mwake alijibwaga chini na kuwa marehemu. Zulekha hakuwepo katika ile sebule, Amata akatazama hapa na pale hasimwone.
“Shit, kaenda wapi huyu mwanamke?” akajiuliza bila kupata jibu, akamgeukia tena Yule jamaa.
“Ha !ha !ha! ha! Umecheza pata potea, leo nakumaliza kwa risasi yangu,” Yule bwana akajibamba na kunyanyuka kwa taabu kutoka pale alipolala, wakati huo Amata bastola yeke ikiwa chini sakafuni, akaikanyaga kwa ncha ya mguu wake na kuibetua, ile bastola ikaruka hewani na Amata akaidaka kwa kono lake la kulia, sekunde hiyohiyo kifua cha Yule jamaa kilitobolewa mara mbili na risasi za Amata, akarudi chini kwa kishindo.
Kamanda Amata akasikia sauti ya kitu kama helikopta, akatoka ndani ya chumba kile na kutafuta njia ya kutokea nje, ngumu. Kutoka ndani ya chumba kile akajikuta kwenye zile korido, huku na kule ving’ora vya hatari vilikuwa vikilia, kimenuka. Akakimbilia upande wa kushoto na kukutana na vijana waliovalia kijeshi na kujining’inizia silaha nzito, kabla hawajakaa sawa, akawafumua kwa risasi na kuwabwaga, akachukua shotgun walizokuwa nazo, akanyofoa na grenade mbili walizokuwa nazo, akaendelea na safari. Moja ya milango mingi aliyoikuta hapo ni ule aliyokuwa anautaka. Akabonya kikengele na ule mlango ukafunguka, ndani yake kulikuwa na vijana wane waliokuwa wamekaa kwenye luninga nne tofauti wakiongoza mitambo yeote ya jengo hilo kuanzia rada, kamera za usalama na silaha zilizofungwa ardhini.
“Mtulie hivyo hivyo! Bosi wenu yuko wapi?” akawauliza huku akiondoa pini kwenye moja ya bomu la mkono (grenade) alilokuwa nalo mkononi, wale jamaa wakatazamana na kukosa jibu.
“Najua ninyi mnafahamu, haya, mmoja baada ya mwingine, mniambie bosi wenu yuko wapi ama la, nateketeza chumba kizima na kwangu si hasara,” akawaambia tena huku akiwa amelishika lile bomu kwa mkono wake.
“Boss yupo na sasa anaondoka,” mmoja akajibu kwa kitetemeshi.
“Nioneshe alipo,” akamwambia na Yule kijana akazungusha kitu Fulani na kwenye luninga ya mbele yake kukaonekana helkopta iliyokwisha washa injini tayari kuondoka, rubani na watu wengine wawili walikuwa tayari ndani yake huku nje kukionekana watu kama watano wenye silaha wakiwa wameweka ulinzi.
“Umeshamkosa boss, anaondoka na mkewe,” kijana mwingine akaongea kwa nyodo wakati alipoona taa ya kuomba kufunguliwa mlango huo wan je ikiwaka, akaponyeza kinobu cha kijani na kule nje ule mlango ukafunguka. Amata aliinua bunduki na kumfumua risasi ya mgongo.
“Aaaaaiiiiihhhhh umeniua mshenzi wewe,” Yule bwana alilalama huku damu zikimvuja.
“Kufa tu, kwani we ulivyotaka kuniua kwenye ndege majuzi ulifikiri sikuoni,” akaiendea moja ya swichi kubwa iliyokuwa mezani hapo ambayo ambayo ilifanana na mkono wa gia ya gari, akabonyeza kitufe cha pembeni yake na runinga kubwa ikawaka mbele yake.
“Unataka kufanya nini wewe!” mmoja nakapiga kelele.
“Tulia mseng* wewe!” akamtoliza huku akimwonesha bastola. Kwenye kile kioo akaiona ile helkopta inayomsubiri Pancho nay eye na mke wake wakielekea kupanda tayari kuondoka.
“Ha ha ha ha, haondoki mtu hapa,” akasema kwa sauti na kuitembeza ile ‘gia’ mpaka alipohakikisha ameiweka sawa ile helikopta.
Mlipuko mkubwa ukatokea, ile helkopta ikalipuka na kuteketea kabisa ikamwacha Pancho na akiwa hana ujanja, akarudishwa ndani na walinzi wake.
Kamanda Amata akabaki anashangaa kwani yeye bado alikuwa hajafanya ulipuzi ule.
† † †
Chiba na Gina waliibuka katika kichaka cha mikoko, kila mmoja akiwa na silaha yenye akili. Chiba akamwonesha Gina ishara ya kuwa afungue mlango, Gina akaweka begani bunduki kubwa na kuufumua mlango wa chuma uliokuwa hapo, kisha wakaelea huko huku wakimwaga risasi kila upande anapoonekana adui. Wakaingia ndani na kuazna kupita kila korido na mlango wakiwapa kipigo adui zao huku wakishinikiza wapi Pancho atapatikana.
Kelele za vilio na mirindimo ya risasi viligubika mle ndani vikisindikizwa na moshi wa baruti. Gina akashusha barakoa yake na kuuficha uso wake dhidi ya moshi huo uliokuwa ukimuumiza macho, na Chiba akafanya vivyo hivyo.
“Tumsake mwnaharamu,” Chiba akamwambia Gina, wakaanza kubomoa mlango mmoja baada ya mwingine wakipekua ndani kote wasimwone.
† † †
Kamanda Amata alipotaka kuondoka ndani ya kile chumba aliona taa Fulani ikiwaka kama ile ya kwanza, akaiendea na kutazama iliandikwa ‘Escape Chamber’ akajua kwa vyovyote Pancho yupo upande huo.
“Control room, Control room!” moja ya redio ndani ya chumba hicho iliita, Amata akainyakua.
“Control Room is under attack,” akajibu na kuhisi kigugumizi upande wa pili.
“We ni nani unayeongea?” ile sauti ikamuuliza.
“Mimi ni Kamanda Amata, TSA namba 1, na sasa niko njiani kuja hukohuko uliko,” akajibu na kuiweka mezani ile redio kisha akaliachia lile bomu nay eye kutoka kasi. Kilichotokea nyuma yake ni mlipuko ambao uliharibu mitambo yote ya lile jengo. Amata alitupwa mbali na kuanguka vibaya kutokana na nguvu ya ule mlipuko, akajiinua lakini mara hii alianza kusikia maumivu makali katika sehemu yake ya ubavu.
Akanyanyuka kwa taabu na kutembea huku akijiegemeshea ukutani kwa mkono mmoja na mwingine akijishika ubavuni kwenye jeraha lake.
“Kamanda!” akasikia akiitwa nyuma yake alipogeuka akakutana na mtu aliyevaa barakoa usoni mwake lakini kwa mwendo tu alimgundua kuwa ni Gina.
“Gina!”
“Yap! Pole sana Kamanda, nikuondoe eneo hili,”
“No! no! tafuta escape chamber ndipo alipo mtu wetu,” Kamanda akamwambia Gina, naye akainua akaongea na Chiba kwenye chombo chao cha mawasiliano na kumpa ujumbe huo huku akimpa taarifa Scoba na Jasmine kuingia kazini.
Haikupita muda waliungana na Chiba na kuufikia mlango huo, mlango wa chuma uliofungwa ukafungika.
“Watakuwepo hadi sasa? Maana hii ni ‘escape’” Chiba akaeleza.
“Nimeharibu system nahisi watakuwa humo ndani kwani kwa sasa hakuna mlango unaoweza kufunguka kirahisi,” Amata akawaeleza.
Gina akinua tena ule mbunduki na kuuweka begani, bonyezo moja tu, ule mlango ulifumuka vibaya, na Chiba akajitosa ndani muda huohuo, Gina akafuatia na Amata akawa wa mwisho, saka nikusake. Kilikuwa chumba kikubwa ambacho ndani yake kulikuwa na boti iendayo kasi, Amata alipoitazama akajua wazi kuwa ile boti kwa muundo wake ina uwezo wa kupita chini ya maji.
“Wapo humuhumu,” akawaeleza wenzake.
“Vaeni barakoa zenu!” Kamanda akawaambia na wote wakavaa.
“Gina,” akaita na kumpa ishara. Gina akainua bunduki moja fupi na kufyatu kitu kama bomu kilichotoa moshi mkali sana kisha wakaendelea kutazama hapa na pale. Haikupita muda wakasikia mtu akikohoa. Gina akawahi na kufungua mlango mdogo uliokuwa mahala hapo.
“Toka mwenyewe!” alimwambia Zulekha aliyekuwa kajificha hapo, “Na mumeo yuko wapi?” akauliza.
“Ushasema mume wangu we wa nini?” akajibu huku akikohoa sana. Gina akageuza ile bunduki na kumpiga nayo shavuni, ikampeleka chini Zulekha, akamshika mguu na kumburuza mpaka karibu na mlango, Amata akamkanyaga mgongoni.
“Tulia mrembo, tulia hivyohivyo,” Amata akamwambia Zulekha.
† † †
Helkopta kubwa lenye magurudumu lilikanyaga ardhi ya kisiwa cha kalebbe, wa kwanza kuteremka alikuwa Madam S, akafuatiwa na Jasmine kila mmoja alikuwa na bastola mkononi mwake. Dakika hiyohiyo, helkopta nyingine ya polisi nayo ikafika eneo hilo a kuteremsha vijana kama kumi hivi waliotimia, kikosi maalumu cha kupambana na ujambazi chini ya Kamanda Tossi. Wakazunguka eneo kwa uhodari kabisa wakihakikisha kila anayepatikana anawekwa chini ya ulinzi na kufungwa pingu.
Madam S na Jasmine waliingia ndani huku vijana wachache wa polisi wakiwasindikiwa nyuma na mbele. Nje ikafika boti iendayo kasi ‘GHOST’ aiakteremsha vijana wengine wenye silaha wakifuatana na Inpekta Simbeye, idara imekamilika. Wale vijana wakaingia ndani na wengine wakabaki nje kama kawaida.
Kwa mawasiliano yao waliweza kujua Gina, Chiba na Amata wako upande gani, wakaenda huko.
8
Kamanda Amata aliliangalia moja ya kabati kubwa katika chumba walichoingia mara hii, kabati hilo lilimtia wasiwasi kwa jisi lilivyokaa na mahala lililowekwa, akaliendea na kulipapasa huku na kule, akashika kitasa na kujaribu kukivuta, hakuna mlango uliofunguka.
“We mwanamke eleza mumeo alipo kabla sijkuhadhibu vikali,” akamwambia Zulekha.
Zulekha hakujibu isipokuwa mikono yake ilikuwa kinyani mwake kama mtu anayeshangaa jambo. Kwa hali hiyo Amata alijua wazi kuwa amtafutaye yupo eneo hilo. Juu ya kitasa kile kulikua na kitu kama jiwe la yaspi ili kuongeza nakshi ya kabati hilo, akaliminya lile jiwe na kabati zima likasogea kando, ndani yake kulikuwa na uwazi ambao bila kificho Pancho alionekana ndani yake. Kutoka ndani mle, akatoka kwa kasi kwa minajiri ya kumvamia Amata lakini kabla hajamfikia, alikutana na konde zito lililomfanya ateme damu, la pili lilitu shavuni na kuacha meno kadhaa sakafuni la tatu lilimpeleka chini mzima mzima.
“Mwanaharamu mkubwa wewe, leo nimekutia mkononi kwa mara ya mwisho,” Amata aliunguruma huku bado akijishika ubavu wake.
“Simama,” akamwamuru lakini Pancho hakufanya hivyo. Akasahau maumivu yake na kumnyanyua kisha akamsimamisha mbele yake na kumkwida shati, akampiga kichwa kimoja kizito mpaka Pancho akaona nyota za ajabu zikimzunguka.
“Wewe unaweza kutusumbua sisi?” akamwuliza.
“Mwacheee!” Zulekha akajirusha kumvamia Amata huku mkononi akiwa na kisu, hakuna aliyejua wapi kakipata kisu hicho lakini hata hivyo hakuna aliyekumbuka kumpekuwa pindi walipomkamata.
Gina kwa wepesi wa ajabu, alaiinua bastola lake na kumfumua Zulekha kabla hajaufikia mwili wa Amata na kumbwaga chini akiwa hana uhai.
“Kwaheri malkia wa Kalebbe!” akasema kwa sauti ya chini huku akishusha mikono wenye bastola chini. Pancho akapagawa kwa kitendo hicho, akajitoa kwa Amata na kumfuata Gina.
“Umemuua mke wangu!” akapiga kelele.
“Na wewe nakuua,” Gina aliongea. Amata alipoitazama sura ya Gina aliona wazi hakuna mswalie Mtume, alijirusha na kumpiga teke la mbavu Pancho akajibwaga upande wa pili na risasi ya Gina akapita peupe na kukiteremsha kioo kikubwa kikubwa ambacho kiliyaruhusu maji ya bahari kuingia ndani, mshike mshike. Wakamnyanyua Pancho na kutoka naye ndani ya chumba kile wakikimbia.
† † †
“Umekamatika mwanaharamu!” Madam S alimwambia Pancho ambaye alikuwa akifungwa pingu na vijana wa polisi. Wakataka kumwingiza kwenye helikopta, Kamanda Amata akamwambia Madam S kuwa hilo sio wazo zuri hata kidogo, Pancho akaingizwa kwenye ile boti, akifuatana na Amata na Chiba wakaondoka na mtu wao kuelekea Dar es salaam.
Boti ile iendayo kasi ilikuwa ikipita chini ya maji na haikuchukua muda kuwasili katika ofisi yao iliyo ndani ya meli mbovu meneo ya Kurasini. Wakamshusha na kumuingiza ndani ya meli hiyo, Pancho aliketishwa kwenye stuli ya chuma, huku Chiba na Amata wakisimama pembeni.
“Mtawafunga wengine lakini si mimi,” pancho aliwaambia vijana hao.
“Aliyekwambi sisi tunakufunga nani? Leo hii tunakuua,” Amata akajibu.
“Ha! Ha! Ha! Nani aliyekwambia mtu hufa kijinga hivyo?” Pancho akaongeza swali la kuuzi.
“Kama alivyokufa mkeo Zulekha kwa mkono wa mwanamke, na wewe utakufa hivyohivyo kwa mkono wa mwanamke,” Chiba akamwambia.
Mara mlango wa chumba hicho ukafunguliwa na Madam S akaingia pamoja na Inspekta Simbeye wakifuatana na Gina na Jasmine.
“Chagua kifo chako haraka!” Madam S akamwambia Pancho.
“We Kibibi, kukukosa kule Kelege usikiri nimekusamehe, ninyi ni waaribifu wa mipango ya watu, nitakuua ndani ya dakika hii,” Pancho aliongea na sekunde hiyohiyo alijinyanyua kwa kasi na kuchomoa bastola ya Simbeye, kabla watu hawaja kaa vizuri alikwishamgeukia Madam S.
“Paaaaaahhh!!!!, Paaaaahhhhh!, Paaaaaahhhh!” kila mtu ndani ya chumba kile alivipa masikio na kuinama chini. Pancho alijibwaga ardhini huku kichwa na kifua chake vikiwa vimetobolewa kwa risasi.
Gina alaiteremsha mkono wenye bastola taratibu na kuurudisha mahala pake huku akitoa sonyo refu.
“Hakuna madhara, TSA 5 katekeleza wajibu wake wa leo,” Gina aliongea na ndipo watu walipotazama na kumwona msichana huyo akiwa anapumua kwa nguvu.
“Asante Gina, leo umefanya kazi yako hasa,” Madam S akamkumbatia Gina kisha wakatoka kuelekea mahala pengine.
† † †
OFISI NDOGO
“Kazi iliyotuumiza kichwa imekamilika, kila mmoja wenu kafanya vizuri kwa upande wake, natoa pole kwa Amata kwa majeraha aliyopata lakini ndiyo kazi yetu,” madam S aliongea akiwa kasimama wima mbele ya meza yake ambayo nyuma yake kulikuwa na bendera ya Taifa na ile beji kubwa ya TSA. Upande wa pili kulikuwa na vijana watano wakike wawili na wakiume watatu, waliosimama kwa ukakamavu huku kila mmoja akiwa na beji yake ya kazi katika mkanda wake.
“Mtakwenda likizo wawili wawili kwa muda wa wiki mbili kila mmoja. Wataanza Gina na Amata kisha Jasmin na Chiba, Scoba atakuwa wa mwisho kwa sababu maalum. Lakini kumbukeni hii ni likizo kazini, muda wowote nikiwahitaji mtafika hapa”.
Gina akamtazama Amata na kutoa tabasamu. Baada ya Madam S kumaliza kauli yake, wakaketi na kupata vinywaji huku wakibadilishana mawazo ya hapa na pale juu ya kazi yao.
HOTELI YA RED STAR
“Mmmmmm Kamanda Amata, you are so sweet!” Gina alilalama huku akimpapasa Amata kifuani.
“Nashukuru kwa kuniokoa,”
“Ndiyo kazi yangu kukulinda mpenzi, nisipokulinda mimi nani atafanya hilo?” Gina akaongea kwa sauti ya kivivu, “Unazeeka Amata hata mtoto huna,” akaongeza.
“Unataka kunizalia mmoja?”
“Sio mmoja tu, hata ishirini…” Gina akajibu.
“Ooooh Gina,” kamanda akajiinua na kuitazama saa yake, ilikuwa saa nne asubuhi.
“Unaenda wapi?”
“Twende tukaoge,”
“Oh, no! bado Kamanda mi nataka tena,”
“Mmmmh beibi,”
“Mmmm nini, nipe cha asubuhi bwana,”
Kamanda akarudi kitandani na kuanza kumbusu Gina kimahaba huku wote wakiwa hivyohivyo bila nguo, mchezo ukaanza upya kama si kuendelea.
Mara simu ya mkononi ya Amata ikaanza kuita kwa fujo, mlio huo haukumpa tabu kujua ni nani anayepiga.
Akaitazama kwenye kioo na kuona kuwa hakukosea. ‘Madam S’ iliandika.

† † † TAMATI † † †
Story by: Richard MWAMBE
0766974865
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…