Makapuku Forum

Makapuku Forum

df146a0a8b78debfffa2e6a4c295ee01.jpg
 
Nimeokota tu share
Akiwa na miaka 5 Alifiwa na Baba yake,
Akiwa na miaka 16 aliamua kuacha shule,
Akiwa na miaka 17 tayari alikua kapoteza ajira 4,
Akiwa na miaka 18 aliamua kuoa,
Akiwa na miaka kati ya 18-22, alikua msimazi wa
njia za reli lakini alishindwa,
Alijiunga na Jeshi lakini aliondolewa,
Akatuma maombi shule ya sheria ila hakupata
nafasi,
Akawa muuzaji wa Bima lakini alishindwa pia,
Akiwa na miaka 19, alifanikiwa kuwa Baba,
Akiwa na miaka 20, Mke aliamua kuondoka na
mtoto,
Hatimaye Akawa mpishi na mwosha vyombo wa
mgahawa mdogo,
Alishindwa hata katika jaribio la kumteka mwanae,
na kuamua kumshawishi mkewe kurejea nyumbani,
Akiwa na miaka 65 alistaafu,
Siku moja baada ya kustaafu alipata mafao yake
kutoka serikalini kama Tsh 231000 (105$),
Alidhani serikali imemuona kama hajiwezi kabisa,
Akafanya jaribio la kujiua, akiamini hakuna thamani
ya kuishi tena, na kwamba ameshashindwa sana,
Akaamua kukaa chini ya mti na kuandika matarajio
yake, Ila aliona ayaandike yale aliyoyakamilisha
tayari,
Akagundua kuna mambo mengi hakuyafanya bado,
Akagundua lipo jambo moja ambalo anaweza
kulifanya zaidi kuliko mtu yeyote yule
anayemfahamu,
Na Ilikua ni namna gani ya Kupika,
Akaamua kuchukua Tsh 191400 (87$) kutoka
kwenye Hundi yake na kununua kuku na
kuwakaanga akiwachanganya na mchanganyiko wa
aina yake,
Akaamua kupita mlango kwa mlango kuwauza kwa
majirani zake huko Kentucky,
Kumbuka akiwa na miaka 65 alikua tayari kujiua
lakini akiwa na miaka 88 Colonel Sanders,
Mwanzilishi wa Kentucky Fried Chicken ( KFC)
Alikua tayari ni Billionaire ($)
Haujakawia kuanza Upya bado.... Kitu kikubwa ni
"Mtazamo" ( Attitude).
Usikate tamaa .... Haijalishi mambo ni magumu kiasi
gani.
Una kila kitu cha kukufanya Ufanikiwe, Amua
kubadilisha mtazamo ili kubadili Stori yako.

pure mathematician

Sema kaka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom