Mkuu hapa umekengeuka kabisa nimepata ukakasi sana haswa kwenye maneno yako ya awali hapo ...Ungeweza kutumia namna ingine na ujumbe ungemfikia mlengwa tena kistaarabu sana...Tusikubali kabisa kufanja undugu na ujamaa tulioujenga kupitia hapa kwani hata members wa hapa KAPUKU tukikutana kwenye majukwaa mengine tunakuwa na ile feeling ya undugu....Na nikushauri kitu Prezda labda hata na mimi kuna mtu nimemkwaza hapa kwa namna moja au nyingine bila mimi kujua mtu huyu kwanza yapasa aniambie mimi hata kwa PM kuwa unanikwaza na sipendi 1,2,3..Akiona sisikii anaweza kureport ishu kwako..Na wewe lazima ukalie kiti na nafasi yako kwa hekima na busara iingia huko PM niambie kuna 1,2 ,3 hakika nitakuwa msikivu maana lengo hapa si kukwazana kwa namna yeyote ile ni kijiwe cha kufanya tucheke tufarahi wakati maisha ya upande mwingine yanaendelea...So please itakuwa vizuri na Member wengine waache uwoga ama unafiki nikikuuzi niambie straight forward tu ili kuepusha mpasuko hapa kijiweni..Naomba nenda PM na Jambilo mwambie 1,2,3 kuwa ni member yupi huyo amelalamika then mmalize na maisha yaendelee kama kawa ida hapa..